Ushauri wa haraka na muhimu.! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa haraka na muhimu.!

Discussion in 'JF Doctor' started by Iza, Nov 2, 2010.

 1. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Heshima Kwenu!
  Imetokea (kwa mujibu wa daktari) kwamba miscarriage inapotekea haswa kwa mimba za umri wa chini ya miezi 3 lazima asafishwe.Naomba kufahamishwa je,

  Mosi,
  Inawezekana kusafishwa kwa kuingiziwa "machuma" au kuna dawa za kumeza ili kusafisha.?

  Pili,
  Mwanamke anaweza kuconsive tena baada ya kutumia hizo njia na nini sababu za miscarriage.?.

  Tatu,
  Ipi ni more riskier than the other.?

  Natanguliza shukrani zangu za dhati!


  NB:Tafadhalini msaidieni jamaa yangu..!
   
 2. Butterfly

  Butterfly Senior Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi siyo dr. lakini nitazungumzia kwa uzoefu wangu wa "kike" na mahusiano mazuri na madaktari nilionao.

  Baada ya kuharibika kwa mimba inabidi Kusafishwa kizazi kwa kutumia MVA kit au sharp curate ni procedure ya kuingizwa vifaa ukeni na inauma sana japo unaweza kuwekewa usingizi (though its not advisable)

  Mkeo atashika mimba tena ila inabidi umpe muda wa kupumzika ili angalai kizazi kipone na kuwa imara zaidi kwani ukimuwahisha sana inawezekana akawa tena kwenye hatari ya kuharibu mimba tena.

  Inawezekana pia akatumia vidonge kusafisha kizazi kama hakupoteza damu nyingi sana na hakupata madhara makubwa ya ndani ya kizazi.

  Njia zote hizi ni salama kama utakuwa na daktari mzuri.

  [​IMG] Hiki ndio kifaa kinachoitwa MVA (Manual Vacuum Aspirator) Hutumika kuterminate pregnancies na kusafisha kizazi pia.

  sijui kama nimekusaidia.:doh::doh:
   
Loading...