Ushauri wa haraka: Mpenzi wangu anachepuka sana, nifanyeje na bado nampenda?

xtaper

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
3,320
4,696
Habari zenu wakuu,

Naandika huu uzi wakati tone la chozi lanitoka,
Kila nikifikiria na nikikumbuka tulipotoka,
Mimi na huyu nimwitae mpenzi wangu,
Ni karibu miaka 5 sasa amekuwa wangu,
Lakini muda wote huo ni yamejitokeza mengi,
Amenisaliti mara nyingi na kwa wanaume wengi,
Kwakuwa nampenda huyu binti, nilimwambia sana sana kuwa abadilike,
Lakini sasa nahisi nimeingia choo cha kike,
Amekuwa ni mtu wa tamaa kumtamani kila mwanaume,
Sijui ni dhiki ya pesa au hamu ya mashine!
Japo najitahidi kila tendo kumk.ojoza,
Ila mwenzangu anajitahid sana kuniliza,
Ni karibu mara ya 6 au 7 sasa,
Kwa yeye kwa wanaume wengine kunasa,
Naombeni ushauri wenu wadau nifanyaje na bado nampenda?
Nimtulizeje?
 
Ts like unalo jibu then unaliogopa

Hiv hamjui sio kila mahusiano yataishia ndoa? Kwangu utakua mwanaume pekee kuona bado uko na mwanamke pamoja na kusalitiwa kote huko mara zote hizo hongera sana una moyo wa kipekee

Unachokisubiri ni either ukimwi au any sexual transmitted diseases au kusingiziwa mtoto kama mimba itatokea

Pengine una lack kitu, mana mapenzi sio kutekeleza kitendo cha kujaaamiana tu,

Tatizo kubwa tunalokosea ni kukaa kwenye mahusiano yasio na afya kwa mda mrefu, ts simple hauko happy just leave

Hujaamua tu hakuna kishindikanacho chini ya jua fanya maamuzi sahihi
 
Mtulize kwa kumuacha, na ww nafsi yako itatulia pia!

Mara 7 bado tu upo? Ulitakiwa uishi kizazi cha kina yohana mbatizaji...
Dah mkuu hata sielewi kila nikijaribu niachane naye moyo kabisa unagoma,
Sijui labda kaniende kufanya mambo kwa Sangoma
 
Mkuu, wake up and face the facts. Huyo mwanamke hakufai.

From the looks of it, huyo mwanamke hana mpango wa kuacha hiyo tabia anytime soon.

Yes it'll be painful and will hurt like hell, since unampenda, but huna jinsi zaidi ya ku-break up nae tu.

Do it for your own peace of mind!
 
Dah mkuu hata sielewi kila nikijaribu niachane naye moyo kabisa unagoma,
Sijui labda kaniende kufanya mambo kwa Sangoma
Achana na mawazo potofu, hujarogwa bali umejiroga mwenyewe kupenda siko,

Kuna wanawake wengi hukoo, tena wenye kila sifa nzur, uliekua naye n sawa na kukata kitunguu huku unalia

Hujaamua tu, kua kama mwanaume bwana saa hizi kishakuona dhaif ndio mana haachi kuzuzua, kua jasiri kuukabil ukwel
 
Ts like unalo jibu then unaliogopa

Hiv hamjui sio kila mahusiano yataishia ndoa? Kwangu utakua mwanaume pekee kuona bado uko na mwanamke pamoja na kusalitiwa kote huko mara zote hizo hongera sana una moyo wa kipekee

Unachokisubiri ni either ukimwi au any sexual transmitted diseases au kusingiziwa mtoto kama mimba itatokea

Pengine una lack kitu, mana mapenzi sio kutekeleza kitendo cha kujaaamiana tu,

Tatizo kubwa tunalokosea ni kukaa kwenye mahusiano yasio na afya kwa mda mrefu, ts simple hauko happy just leave

Hujaamua tu hakuna kishindikanacho chini ya jua fanya maamuzi sahihi
Asante sana kwa ushauri Madame S yawezekana nalack kitu naelewa kama binadamu sio mkamilifu,

Nilishawahi kumuacha lakini huwa anarudi kubembeleza msamaha na kwa kuwa na mpenda inakuaga rahisi kumsamehe.

Sijui nifanyaje niweze kuachana naye mazima na kumsahau moyoni
 
na tatizo ndio hilo kishajua hupindui

Kua na msimamo, kama ndio iwe ndio hapana isomeke hapana, we mwanaume bwana jikaze
 
Haujipendi kimpenda wakayo yeye hakupendi.

Mwanamke akimpenda mwanaume hata fikra za kuchepuka hatakuwa nazo kabisaaa.. sasa wewe wote hao na bado upo.

Unasubiri wakimla na kumsaza ndio umuoe? Aisee hadi nimekuonea huruma kweli mapenzi ni kaa la moto wakati mwingine..

Kaa ufikirie kwanini haswa unataka kuwa naye huku unamsamehe kila wakati.. au wewe ndio unashida ambayo haujui unayo.

Na pia unasubiti kuletewa magonjwa ufe haraka na nini tena unasubiri au unataka upate kutoka kwake?

Hupendwi.. angekupenda pia asingeacha ujur anatenda hayo yote angekuwa kismati ila naona na akili zake zipo anakokujua yeye..

Halafu jua kuna wanawake hawapendi wanaume wanao kuwa maboya kila kitu sawa sawa.. hawatoi muda wa kuchezesha fikra za mwanamke..

Ungekuwa hata mgumu fulani wa kwanza tu angebadilika labda kwa kukupenda sanaaaa zaidi yako.. embu sepa au utajiju
 
Mkuu cocochanel asante lwa ushauri. Ingawa ni mgumu ila unanitia moyo napata ujasiri kiasi wa kufikia maamuzi magumu
 
na tatizo ndio hilo kishajua hupindui

Kua na msimamo, kama ndio iwe ndio hapana isomeke hapana, we mwanaume bwana jikaze
Dah asante sana. Mkuu ubarikiwe. Ushauri wako unanipa matumaini I can recover from this mess
 
Asante sana kwa ushauri Madame S yawezekana nalack kitu naelewa kama binadamu sio mkamilifu,

Nilishawahi kumuacha lakini huwa anarudi kubembeleza msamaha na kwa kuwa na mpenda inakuaga rahisi kumsamehe.

Sijui nifanyaje niweze kuachana naye mazima na kumsahau moyoni
Mbona unaweza aisee... muache then concentrate kwenye mambo yako ya kukuingizia kipato! Nasikia uchungu kuona kuna mwanaume mwenzangu uko katika hali ya kizembe kama hiyo! Piga chini songa mbele
 
Habari zenu wakuu,

Naandika huu uzi wakati tone la chozi lanitoka,
Kila nikifikiria na nikikumbuka tulipotoka,
Mimi na huyu nimwitae mpenzi wangu,
Ni karibu miaka 5 sasa amekuwa wangu,
Lakini muda wote huo ni yamejitokeza mengi,
Amenisaliti mara nyingi na kwa wanaume wengi,
Kwakuwa nampenda huyu binti, nilimwambia sana sana kuwa abadilike,
Lakini sasa nahisi nimeingia choo cha kike,
Amekuwa ni mtu wa tamaa kumtamani kila mwanaume,
Sijui ni dhiki ya pesa au hamu ya mashine!
Japo najitahidi kila tendo kumk.ojoza,
Ila mwenzangu anajitahid sana kuniliza,
Ni karibu mara ya 6 au 7 sasa,
Kwa yeye kwa wanaume wengine kunasa,
Naombeni ushauri wenu wadau nifanyaje na bado nampenda?
Nimtulizeje?
Wanaume wavumilivu hivi wamebaki kwenye tamthiliya !!!! 7x duuuh..... kwa tulio wengi only once inatosha .... tena mpenzi , bora angekuwa mke.....
 
Haujipendi kimpenda wakayo yeye hakupendi.

Mwanamke akimpenda mwanaume hata fikra za kuchepuka hatakuwa nazo kabisaaa.. sasa wewe wote hao na bado upo.

Unasubiri wakimla na kumsaza ndio umuoe? Aisee hadi nimekuonea huruma kweli mapenzi ni kaa la moto wakati mwingine..

Kaa ufikirie kwanini haswa unataka kuwa naye huku unamsamehe kila wakati.. au wewe ndio unashida ambayo haujui unayo.

Na pia unasubiti kuletewa magonjwa ufe haraka na nini tena unasubiri au unataka upate kutoka kwake?

Hupendwi.. angekupenda pia asingeacha ujur anatenda hayo yote angekuwa kismati ila naona na akili zake zipo anakokujua yeye..

Halafu jua kuna wanawake hawapendi wanaume wanao kuwa maboya kila kitu sawa sawa.. hawatoi muda wa kuchezesha fikra za mwanamke..

Ungekuwa hata mgumu fulani wa kwanza tu angebadilika labda kwa kukupenda sanaaaa zaidi yako.. embu sepa au utajiju
You have a point, na ndio wanawake wengi wako hivyo. Akiku outsmart tu ujue umekwisha. Mwanaume lazma uwe na msimamo kuwa hiki nataka hiki hapana. Failure to comply unaachana nae tu. Ingawa sio rahisi ukiwa umempenda sana mtu ila inabidi kufanya kitu sahihi!

Binafsi napitia huu mtihani pia, 5yrs gf ameanza cheating imefikia stage atu vibe tena. Tamaa zimemzidia ameanza kujiachia kama yupo single. People are hitting on her(anatongozwa) anaanzisha branches kimya kimya anaruhusu hio hali makusudi kabisa. Nshamstukia nikamchana ila seems haelewi. What i decided ni kumpotezea tu hamna namna
 
Back
Top Bottom