Ushauri wa Eng. Ngulangwa kwa wabunge wa Tanzania

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
SASA NAWASHAURI WABUNGE MPUMZISHENI MAGUFULI:

Nimetumia muda wa kutosha kumpa Ushauri wa Bure Ndugu John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) juu ya Kudumisha Utawala wa Sheria na Kulinda Demokrasia iliyopelekea yeye kuwa Kiongozi wa nchi hii. Nakumbuka Msajili wa Vyama vya Siasa alijaribu kutoa Tafsiri ya Kauli ya Rais ya Kupiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa mpaka 2020, siku moja baada ya mimi kuandika kwenye Ukurasa huu Kushangazwa kwangu na Ukimya wa Msajili wa Vyama juu ya Kauli hiyo ya Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM inayopingana na Kanuni za Vyama vya Siasa za Mwaka 2007 zilizotungwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Hata hivyo, Kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya Wakuu wa Mikoa juu ya Kupiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa katika Mikoa yao zinadhihirisha wazi kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa ndiye aliyeshindwa kumuelewa Rais Magufuli.

Ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa Kinga Rais kushitakiwa Mahakamani (Ibara ya 46), lakini Katiba inalipa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mamlaka ya “Kumng’oa” Rais kwenye Kiti Chake. Kwa mujibu wa Ibara ya 46A (2), Bunge linaweza kumlazimisha Rais kuachia ngazi, naye kulazimika kufanya hivyo Kupitia Azimio la Bunge, endapo atathibitika kufanya makosa yafuatayo:
(a) Ikiwa ametenda vitendo ambavyo kwa Ujumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) Ikiwa ametenda vitendo ambavyo vinakiuka Maadili yanayohusu Uandikishwaji wa Vyama vya Siasa yaliyotajwa katika Ibara ya 20(2) ya Katiba; au
(c) Ikiwa amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano…
Ukifuatilia Mwenendo tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie Madarakani, Rais amekuwa akilalamikiwa kwa Kukandamiza Demokrasia, kutumia Lugha za kudhalilisha kwa Vijana waliotimuliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (kwa kuwaita VILAZA) na mambo mengine yanayokwenda Kinyume na Katiba ya JMT na Lengo la Kuwepo kwa Katiba hiyo kama linavyobainishwa na Ibara ya 9 ya Katiba. Tazama 9(a), 9(f) na 9(h) kwa mfano, pia rejea Hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo aliyoitoa mbele ya Maelfu ya Wakaazi wa Dar es Salaam, kwenye Viwanja vya Zakhiem Mbagala 05/06/2016.

Katiba ya JMT imeeleza hatua ambazo katika Mazingira kama haya, Bunge linaweza kumfikisha Rais kwenye Kujiuzulu. Ibara ya 46A(3)(a) inaeleza kwamba Mchakato wa Kumng’oa John Pombe Magufuli (JPM) Ikulu unaweza kuanza kwa Taarifa ya Maandishi inayoungwa mkono na asilimia ishirini ya Wabunge wote Kuwasilishwa, ikieleza makosa yake. Naamini kupata asilimia ishirini ya wabunge kuanzisha huu Mchakato si suala zito, linawezekana ( Kumbuka Idadi ya Wabunge wa Upinzani).

Ingawa Mchakato huu unaweza ukapata ugumu kupitia Kamati Maalum ya Uchunguzi itakayoundwa katika mazingira haya ya Demokrasia finyu, naamini Kitendo cha Rais kulazimika kujieleza/kujitetea ni hatua muhimu sana katika Kurekebisha Nidhamu na kuwakumbusha Viongozi wa Umma kwamba HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA.

Kwa mujibu wa Ibara ya 46A (9):
“ Baada ya Taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa Ibara ndogo ya 8 ( yaani 46A (8)), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili za Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashitaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika Kiti cha Rais, au kuwa mashitaka hayo hayakuthibitika”.

Nitumie fursa hii kuwaondoa hofu wabunge wa Upinzani, wasihofie idadi kubwa ya wabunge wa CCM.

Wapo wabunge wanaochukizwa na baadhi ya makosa haya kwani Ubabe huu ukiachiwa hata atakapokuwa Mwenyekiti wa Chama chao, atakandamiza Demokrasia ndani ya CCM.

Kusambaratika kwa Ukomunist zama za Vita Baridi kuliwakutanisha Mahasimu Marekani na Osama Bin Laden katika dhamira moja, japo kwa Sababu na Malengo tofauti.

Si ajabu theluthi mbili ya Kura ikapatikana ili kulinda Maslahi mapana ya Taifa hili.

Hivyo naamini JPM atalazimika kujiuzulu ndani ya Siku 3 tangu kupitisha Azimio (Ibara 46A(10)) na kuweka Rekodi ya kuwa Rais wa Kwanza kuondolewa na Bunge kwa kujaribu kuichezea Demokrasia tunayoijenga kwa taabu na hatimaye apoteze Malipo yoyote ya Pensheni na Haki zingine (Ibara 46A(11)).

Kwa kuwa haki hii wamepewa Wabunge wa JMT na mimi si Mbunge, natumia fursa hii kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) ya Katiba ya JMT kuwashauri wabunge wakaweke Historia hii mpya kwenye Kikao kijacho cha Bunge.

Eng. Mohamed M. Ngulangwa
Katibu wa Uadilifu Taifa
ACT-Wazalendo(0713417707)
 
Enginer gani huyo hana akili. Atakuwa amefoji vyeti hakuna injiia mwenye fikra mbovu kama hizi
 
Duh, naona hoja zipo mwelekeo ule ule wa posho na uchu wa madaraka.

Mbona hamuweki hoja za ni kwa namna gani mapato ya serikali yaongezeke? Vipi uchumi ukue? Mmekalia hoja za madaraka tu.
 
Duh, naona hoja zipo mwelekeo ule ule wa posho na uchu wa madaraka.

Mbona hamuweki hoja za ni kwa namna gani mapato ya serikali yaongezeke? Vipi uchumi ukue? Mmekalia hoja za madaraka tu.
Ukitaka mapato ya serikali yaongezeke hakikisha kila senti unayoipata peleka benki kuu kwenye acc. ya serikali. Ulete mrejesho eeehh!!!
 
Duh, naona hoja zipo mwelekeo ule ule wa posho na uchu wa madaraka.

Mbona hamuweki hoja za ni kwa namna gani mapato ya serikali yaongezeke? Vipi uchumi ukue? Mmekalia hoja za madaraka tu.
Nenda ofisi ya TAIFA YA TAKWIMU yenye mamlaka kisheria ya kutoa taarifa sahihi kuhusu takwimu za serikali. Uchumi umesimama na utaporomoka kwa kasi ya mwendokasi si muda mrefu nchi inapogezwa kuwa shamba la bibi kwa wageni (Nina maana wazawa tumetengwa rasmi kwenye shughuli za uchumi).

1. Unanukuu kauli za propaganda za watawala waliobobea kudanganya hata kupora maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura. Kauli ya Maisha Bora bado ipo midomoni mwa watawala huku ukweli umebaki kuwa Bora Maisha.

2. Takwimu zako na unaowanukuu si sahihi nenda ofisi za Takwimu za Taifa upata takwimu sahihi na rasmi utuwekee hapa.

3. Nina hakika mtu ambaye hajawahi kupewa madaraka hana ladha wala sababu ya kuwa na uchu wa madaraka. Kinyume chake kung'ang'ania hata kufikia kupora madaraka toka kwa kauli ya wananchi kwenye sanduku la kura ni ushahidi tosha wa uchu wa madaraka. Mmpelekeeni dikteta wenu uchwara habari kuwa baadhi yetu tunajua kinachoendelea na hatutasalimu amri za kimla.
 
Enginer gani huyo hana akili. Atakuwa amefoji vyeti hakuna injiia mwenye fikra mbovu kama hizi
huu si utaratibu wa ki ungwana,huyo unae mwita injinia aliye foji vyeti na wewe na hakuna tofauti,yeye kaweka hoja mezani wewe unakuja na hisia zako tu na matusi juu.hoja hujibiwa kwa hoja ndo uungwana huo,yeye kanukuu hadi vifungu vya katiba wewe hata kifungu kimoja ja katiba hujaweka weka halafu unataka kutuaminisha kua wewe ndo una akili.
 
2some na kuelewa then 2jadili hoja 2simjadir injinia. 2jadil hoja yake kwa mapana
 
Nenda ofisi ya TAIFA YA TAKWIMU yenye mamlaka kisheria ya kutoa taarifa sahihi kuhusu takwimu za serikali. Uchumi umesimama na utaporomoka kwa kasi ya mwendokasi si muda mrefu nchi inapogezwa kuwa shamba la bibi kwa wageni (Nina maana wazawa tumetengwa rasmi kwenye shughuli za uchumi).

1. Unanukuu kauli za propaganda za watawala waliobobea kudanganya hata kupora maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura. Kauli ya Maisha Bora bado ipo midomoni mwa watawala huku ukweli umebaki kuwa Bora Maisha.

2. Takwimu zako na unaowanukuu si sahihi nenda ofisi za Takwimu za Taifa upata takwimu sahihi na rasmi utuwekee hapa.

3. Nina hakika mtu ambaye hajawahi kupewa madaraka hana ladha wala sababu ya kuwa na uchu wa madaraka. Kinyume chake kung'ang'ania hata kufikia kupora madaraka toka kwa kauli ya wananchi kwenye sanduku la kura ni ushahidi tosha wa uchu wa madaraka. Mmpelekeeni dikteta wenu uchwara habari kuwa baadhi yetu tunajua kinachoendelea na hatutasalimu amri za kimla.
1. Ungeweka hizo takwimu hapa, ili kusupport hoja yako.

2. Sijaongelea propaganda ya yeyote, isipokuwa nimeongelea kilichopo kwenye vichwa vya viongozi wa upande wa pili.

3. Soma hoja yangu uielewe vizuri, viongozi wa upande wa pili akiri zao zimebaki kuona kila kinachofanywa na hii serikali kuwa hakiwezekani, na wamebaki wanaangalia madaraka tu na si maendeleo
 
Tuondoe kwanza nguzo yake bungeni tulia kisha yeye,ufunguzi wa bunge kwani kiongozi wetu act alitoka nje?
 
kiujumla mtoa hoja yuko sahihi sana. hakuna kosa kubwa kwa kiongozi wa nchi kuvunja katiba aliyoapa kuilinda.mwalimu nyerere aliwahi tuasa.
 
kiujumla mtoa hoja yuko sahihi sana. hakuna kosa kubwa kwa kiongozi wa nchi kuvunja katiba aliyoapa kuilinda.mwalimu nyerere aliwahi tuasa.
It is very very true.

Ingekuwa nchi yetu inaendeshwa kweli kwa utawala wa sheria na siyo huu unaoitwa 'kinafiki' kuwa wa sheria, wakati watawala ndiyo walio mstari wa mbele katika kuivunja Katiba yetu ya nchi, ambayo ndiyo sheria mama ya sheria zote za nchi yetu .

Katiba yetu ya nchi Ibara ya 3 inatamka wazi kuwa nchi yetu itakuwa ya mfumo wa vyama vingi. Sasa Mkuu wa nchi anapata wapi ujasiri wa kutamka hadharani na kupiga marufuku vyama vya siasa vyote visifanye shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020, lakini wakati huo huo akitoa ruksa 'indirectly kwa chama chake kuendelea na shughuli zao za siasa bila 'kuguswa' na Polisi?!

Kwa tamko lake pekee alilolitoa Magufuli la kupiga marufuku shughuli zozote za kisiasa kufanyika nchini hadi mwaka 2020, na wakati huo huo kuruhusu chama chake kiendelee na shughuli za siasa bila kubughuziwa na Polisi, kwa kauli hiyo pekee, kama nchi yetu ingekuwa inaendeshwa na utawala wa kisheria wa kikwelikweli, basi Magu angekuwa tayari keshajiuzuru Urais na nchi yetu hivi sasa ingekuwa inajiandaa kwenye uchaguzi mkuu mwingine.

Kumbukeni hata Mwalimu Nyerere, katika hotuba zake alikuwa anasisitiza sana kuwa Rais wa nchi anatakiwa kuwa mtu wa kwanza katika kuitii na kuitekeleza Katiba ya nchi ambayo kabla ya kuingia madarakani aliapa kuilinda na kuitii.

Tatizo la nchi zetu nyingi hususani barani Afrika wanaamini kuwa wao wako above law na hakuna hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa na mamlaka nyingine nchini mwao dhidi yao.

Vile Vile kiburi kikubwa ambacho viongozi wengi wa kiafrika wanakuwa nacho ni kule kuamini kwao kuwa wao ndiyo 'wamiliki' wa vifaru na magari ya washawasha, na wakati wowote 'wanapojisikia' tu wana uwezo wa kuviamrisha vifaru hivyo na magari ya washawasha kwenda kuwasambaratisha raia wasio na hatia ambao ndiyo wamiliki halali wa vifaa hivyo, kwa kuwa vimenunuliwa kwa kodi zao .....
 
Hoja imetulia haswaa..

Tatizo la madikteta uchwara huwa pia ni vil/aza.. hawana uwezo wa kusoma na kuelewa hata mambo waliyoapa kwayo..
Huyu Rais yawezekana hajui anachokifanya au kama anajua basi haelewi ni jinsi gani ya kukifanya.. ndani ya miezi saba akiwa Ikulu amedhihirisha wazi kuwa hakuwa "presidential material" bali "victim of circumstances" baada ya kutokea factions ndani ya fisiem.

Jamaa anadhani uchumi utakua tu kivyovyote..au nchi inaweza kuwa na discipline kivyovyote, jambo ambalo haliwezekani. Ushauri ni kwa wenzangu ambao hamkujaaliwa akili ya kuona mambo katika 3D.. mnamchanganya rais kwa sababu mnashabikia uvunjifu wa Katiba ya nchi, kosa ambalo latosha kumtimua Ikulu.

Kwa upande mwingine si kwamba wananchi ni vila/za saana kama wale, siku fulani hivi atakuja kuomba achaguliwe tena.. aje na majibu sahihi.

Asubuhi njema
Sirte
 
Enginer gani huyo hana akili. Atakuwa amefoji vyeti hakuna injiia mwenye fikra mbovu kama hizi
ina maana ndio akili zako zilipoishia?maana wahenga walisema "ukitaka kujua akili ya mtu mpe nafasi ya kusema au kutenda".
 
Hakuna kosa kubwa kama kuvunja katiba na kutoiheshimu. Hilo ni zito kuliko hata kubaka au kuiba, na mtu yeyote anayetenda lazima awajibishwe. Ndio maana hata Rais pamoja na kinga yake lakini kwenye kuvunja katiba hajasamehewa hata kidogo.
Naunga mkono hoja hii kwamba kama wajibu wa kusimamia jambo hilo wamepewa wabunge basi waungane na kutimiza wajibu wao bila kujali itikadi zao ili hata ikibidi aitwe ajieleze itasaidia kumbadilisha na hiyo ni njia ya kumsaidia ajitambue.
Hii ni karne ya 21 sio zama za giza tena
 
kiujumla mtoa hoja yuko sahihi sana. hakuna kosa kubwa kwa kiongozi wa nchi kuvunja katiba aliyoapa kuilinda.mwalimu nyerere aliwahi tuasa.
Jitahidi kuielewa katiba yetu, Rais ana mamlaka makubwa hadi kuitisha bunge na kulivunja muda wowote, cha maana tuangalie katiba yetu, je imevunjwa?
Rais wetu hajavunja katiba, anachapa kazi.
Huyo Engeneer wenu ACT mchunguze vizuri, inawezekana ni wale akina...
 
Back
Top Bottom