Ushauri wa Bure: Wamiliki wa Radio Clouds FM ya Dar es salaam

Yaani mkuu unaeleza kweli kuna mpuuzi mmoja hapo juu anapinga sijui huwa anafurahiaje matusi hayo? jaman kuna watu wengine wamejaa mawazo mabaya tu!
Wengi ni chuki, roho mbaya na wivu ndio vinavyowa nyegeranyegera. Kila kukicha thread za clouds na kibonde tu, hii inaonesha walivyo juu. Pamoja na kuponda kwenu bado mnaendelea kuisikiliza tu kama vile hakuna redio nyingine. Si sikilizeni WAPO iliyokuwa upande wenu? Kwa taarifa zenu Clouds ndio baba wa burudani hapa Tanzania na mtaipenda tu kwa moyo au kwa chuki.
 
Weka clip moja kali ya production zako. haa tukusikie na wewe. sometme theory ni rahisi sana kuliko practical ndio maana unaona watu wanakiimbilia kwenye siasa. Sababu siasa ni therory tu.

Poa mkuu! mimi huwa nawafanyia kazi sawa na uhitaji wako! Nambie kama unahitaji kufanyiwa kitu kazi cha radio nikusukie program matata!
 
Habari yako msomaji!

KWA WAMILIKI WA RADIO CLOUDS FM.

Mimi Radio Producer napenda kuandika ushauri wangu kwako/kwenu wamiliki wa clouds Fm. Ni ushauri tu ukiupenda karibu, ukiona kawaida hakuna shida, silipwi wala sikulipi!

1. Nawapongeza sana Clouds fm kwa kujipanua na kusikika sehemu nyingi za nchi yetu ya Tanzania. Usikivu wenu ni mzuri kabisa, na mna kitu unique kabisa katika muonekano wa radio yenu. Nawapongeza sana kwa hili kwa sababu kila tunapotune radio hii huwa tunaipata bila shida kabisa! Hongereni pia kwa kujitahidi kutafuta wafanyakazi wenye uwezo wa kazi na ubunifu wa hali ya juu, ukweli wapo wafanyakazi katika radio yenu wanafanyakazi vizuri sana!

2. Pili napenda kuzungumzia vitu hivi (Format, Goal and Targeted Audience) ya radio yenu. Kwa harakahara bado natatizwa sana na format ya radio yenu, je ni music format au? hapa bado napata shida kulingana na mpangilio wa vipindi! Ninachoshauri hapa jaribuni kuiangalia format na muitumie kuprogram vipindi vyenu itasaidia sana. Goal yenu ni ipi hasa? je, mnaitumia kama ipasavyo? Tatu walengwa wenu (Targeted audience) ni akina nani? Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu wakati mwingine nimeambiwa walengwa ni Vijana. Kama ni vijana je. format mnayotumia inapendwa na vijana? kama ni music format inaweza kuwa yes, lakini je goal yenu inafika sawasawa? (HAPA NDIO RADIO CLOUDS INAPOSABABISHA MAMBO YASOMEKE TOFAUTI KWA WASIKILIZAJI) kwanini??

3. Kwa sababu 1. Lugha- mara nyingi lugha inayotumika hasa kiswahili cha wadada hao na wakaka hao hakiendani na na wala hakiwezi kusimamia goal iende sawa. Kama mna malengo mfano ya kuielimisha vijana, unadhani kwa hali ya lugha inayotumika unajenga nini? Uharibifu mkubwa wa utamaduni wa mtanzania kwa matumizi mabaya ya lugha ya kiswahili. Nyinyi kama chombo cha habari mlitakiwa kuwa mstari wa mbele kuwafundisha vijana kutumia lugha vizuri zaidi ili tuwe na taifa lenye nguvu na utamaduni wa kupendeza!

4. Kwasababu 2. Uwezo wa baadhi ya watangazji. Kuna baadhi ya watangazaji wanashindwa kuitendea haki clouds fm kwa kushusha sifa na maadili ya radio. Si unajua mtangazaji akiharibu ameharibu jina la radio husika?? Wengine hawana uwezo mkubwa na wa kufikiri lakini hao ndio wanakuwa wategemewa wa kuchangia mijadala mbalimbali matokeo yake wanachangia kwa hisia zao wenyewe, ni hatari sana! Narudia tena ni hatari sana kwa mtangazaji kuruhusu hisia zake anapokuwa kwenye kipindi.

5. Kwa sababu 3. Vipindi vyenu- Jaribuni kuviangalia vipindi vyenu upya! vyaweza kuwa vizuri sana lakini format yake ndiyo inaharibu! angalieni maadili ya mtanzania pia! Hasa kwenye hivyo vipindi vya mapenzi na mahusiano jaribuni kuviprogram upya vikae katika hali ya kufundisha na kuelimisha jamii siyo tu kuburudisha! Tumieni lugha nzuri kwenye vipindi hivi ili atu waone userious wa kipindi. Wekeni vitu vizuri kwa walengwa, isije kuwa ka kuwa walengwa ni vijana kwa hiyo muwaandalie vipindi vya mtindo huo ili wafurahi, hiyo itakuwa ni hasara! Hata kama vijana ndio walengwa nia mathubuti ni kwamba wao wajifunze kutoka radio yenu siyo wajifunze lugha mbaya, matusi na mambo ya kiajabuajabu!

6. Kwa sababu 4. Balance- hata kama walengwa ni vijana waangalieni hata bonus audience! Kuweni na balance wapendwa media zinawatu wengi hata kama ni wa namna tofauti ila wote hujumuika pamoja na kusikiliza au kutazama! Sasa mmeandaa kipindi cha mapenzi kwa ajili ya kijana, watangazaji wenyewe tu wanaonekana wamelewa na mahaba unadhani kipindi hiki kitaangaliwa ma familia yote? kitamfundisha kijana au kumchochea kwenye hisia mbaya?

7. Mwisho, angalieni sana watangazaji wenye majina, wasifanyekazi kwa kuangalia majina yao! Wanaharibu lazima wafuate utaratibu kwa kituo husika! mtapata pesa sana lakini kama maadili yanapotea pesa hiyo haitawasaidia kitu kwa sababu mtakuwa manapotosha jamii! Jaribuni kuuangalia uongozi wenu hasa PROGRAM MANAGER! huyu bwana angekuwa serious hayo yote yasingetokea! Hapo ndio ikulu, kama PM yuko vizuri mambo yote yatakuwa safi tu upande wa programming!

Acheni kutumia lugha mbaya/mtaani/chafu/uchochezi, acheni kutumia hisia zenu mnapokuwa hewani, angalieni format yenu, goal yenu na targeted audience wenu, angalieni uwezo wa watangazaji wenu hakika mtajenga taifa!

Asanteni kwa kusoma.
Radio Producer
UK.
Siongezi kitu!
 
Wengi ni chuki, roho mbaya na wivu ndio vinavyowa nyegeranyegera. Kila kukicha thread za clouds na kibonde tu, hii inaonesha walivyo juu. Pamoja na kuponda kwenu bado mnaendelea kuisikiliza tu kama vile hakuna redio nyingine. Si sikilizeni WAPO iliyokuwa upande wenu? Kwa taarifa zenu Clouds ndio baba wa burudani hapa Tanzania na mtaipenda tu kwa moyo au kwa chuki.

Umesema vizuri sana mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi!
 
Mwenyew nshaachaga kuisikilza hiyo radio station long time ago!hata'sikumbuk tena sauti zao!manake ni kichefuchefu
 
Kuna kila sababu ya Regulator ambaye ni TCRA kujua kuwa zaidi ya kutoa leseni anao wajibu wa kufuatilia na kuona kuwa mienendo na maadili ya Radio ipo sambamba na sheria, miiko na utamaduni wa Mtanzania pamoja na tasnia nzima ya uhabarishaji kupitia radio. Clouds wana mengi ya kujifunza na kujirekebisha. Chukueni hatua...
 
Umesema vizuri sana mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi!

Mapenzi mema na nchi wapi pelekeni huko umbeya wenu, mafanikio ya wenzenu kwenu imekuwa ni kero. Hamuwezi kuwaacha vijana wafanye kazi zao kila siku Clouds hivi Kibonde vile. Hovyo radio producer unakaa kuproduce umbeya tu siku utavalishwa shanga hapa mjini, na hiyo roho yako utaendelea kusota hadi unakufa masikini wa roho mkubwa. Wewe huo ushauri wako kwa nini usojipe mwenyewe njoo hapa fungua redio tuone maana huo mtaji wenyewe kwa wewe mbeba mabox haukushindi. Yaani mijitu kama wewe hata siku haiwezi kufanikiwa.
 
kibonde bana!
 
Maoni ya mwandishi yamesomeka, lakini yako juu juu tu, hajaweka mapendekezo ya waziwazi nini kifanyike, yeye kama producer alitakiwa kila kosa aliloliona atoe mapendekezo yake bila kuwaachia Clouds assignment. Sema nini kifanyike kwa mtazamo wako.

Kwa baadhi ya wachangiaji, kumbe tunapenda kusikiliza, mmoja amewaponda Hando na kibonde lakini anasema anasikiliza kila asubuhi na jioni. Sasa kama upendi matangazo yao kwanini unasikiliza... moja kwa moja unawapenda!
 
Mwenyew nshaachaga kuisikilza hiyo radio station long time ago!hata'sikumbuk tena sauti zao!manake ni kichefuchefu

Huu ni mfano mzuri mtu tayari kishaacha kuisikiliza redio kwa sababu ya hayo yanayotangazwa! Lazima wajiulize na watende mema hapa!
 
Maoni ya mwandishi yamesomeka, lakini yako juu juu tu, hajaweka mapendekezo ya waziwazi nini kifanyike, yeye kama producer alitakiwa kila kosa aliloliona atoe mapendekezo yake bila kuwaachia Clouds assignment. Sema nini kifanyike kwa mtazamo wako.

Kwa baadhi ya wachangiaji, kumbe tunapenda kusikiliza, mmoja amewaponda Hando na kibonde lakini anasema anasikiliza kila asubuhi na jioni. Sasa kama upendi matangazo yao kwanini unasikiliza... moja kwa moja unawapenda!

Mkuu mapendekezo yako summarized kwenye red color mwisho wa hiyo thread! Na kwa mtu anayehusika hapa hahitaji mapendekezo kwa ukjweli upo wazi kama lugha chafu inatumika studioni hujui solution yake wewe?
 
Kuna kila sababu ya Regulator ambaye ni TCRA kujua kuwa zaidi ya kutoa leseni anao wajibu wa kufuatilia na kuona kuwa mienendo na maadili ya Radio ipo sambamba na sheria, miiko na utamaduni wa Mtanzania pamoja na tasnia nzima ya uhabarishaji kupitia radio. Clouds wana mengi ya kujifunza na kujirekebisha. Chukueni hatua...

Kweli kabisa mkuu! umetoa mtazamo mzuri sana!
 
Mapenzi mema na nchi wapi pelekeni huko umbeya wenu, mafanikio ya wenzenu kwenu imekuwa ni kero. Hamuwezi kuwaacha vijana wafanye kazi zao kila siku Clouds hivi Kibonde vile. Hovyo radio producer unakaa kuproduce umbeya tu siku utavalishwa shanga hapa mjini, na hiyo roho yako utaendelea kusota hadi unakufa masikini wa roho mkubwa. Wewe huo ushauri wako kwa nini usojipe mwenyewe njoo hapa fungua redio tuone maana huo mtaji wenyewe kwa wewe mbeba mabox haukushindi. Yaani mijitu kama wewe hata siku haiwezi kufanikiwa.
Mkuu hayo unayoyasema hayajengi jiangalie kama unasema kweli
 
Mkuu hayo unayoyasema hayajengi jiangalie kama unasema kweli

Hata wewe huna nia ya kujenga bali ni chuki iliyosababishwa na madonda ya uchaguzi. Unataka tuamini Clouds ni redio mbaya eti kwa kuwa hawafuati seti fulani ya standards ulizo ziweka wakati ni dhahiri kati ya radio zaidi ya arobaini hapa nchini wao wanaongoza kwa kila kitu. Waambie na hao unaowatumikia hata wangekuwa ni malaika bado wasingekubalika na watu wote, mawazo hayo ya kutaka kumtusi au kumpa sifa mbaya kila aliyetofauti na mitazamo yao ni ya kidikteta na hayawezi kuvumiliwa na ndio maana watu waliwakataa na wataendelea kuwa kataa milele amina.
 
Naamini Clouds bado ni redio nzuri,kama wakitoka baadhi ya watangazaji ambao hawana la maana zaidi ya kutafuta umaarufu,kuna baadh ya vipindi nasikiliza lakin havina mvuto kama zamani,mf.power breakfast,jahazi,sport extra..only that.
 
Back
Top Bottom