Ushauri wa bure tu kwa serikali, waziri wa kazi na uongozi wa HESLB

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,892
16,413
Good morning.

Mimi huwa nikiamkaga na ideas nakimbilia jamiiforums kushauri, naombeni mnisamehe kama nitawaudhi watu humu leo, but I'm speaking my mind....

Kama sijakosea, ninadhana kuna sheria inayomuhitaji muajiri kwa hapa Tanzania kuwatambua waajiriwa wao waliosomeshwa na bodi ya mikopo kisha ku-withhold makato ya mishahara yao na kuyafikisha serikalini kila mwezi.

Sasa katika kuwapunguzia waajiri (ikiwemo serikali pamoja na taasisi zilizo chini yake) mzigo wa kuwatambua wadaiwa wa HESLB, nilikuwa ninashauri serikali kupitia uongozi wa HESLB wawe wanatoa "Loan Clearance Letter" kwa kila mtu anayeomba kazi aidha awe alisomeshwa na board ya mikopo ama la.

Hii inamaanisha kila application letter ya maombi ya kazi iwe inaambatanishwa na nakala ya kivuli ya clearance letter kutoka HESLB ambayo board itakuwa inatoa kwa kila applicant kwa fee isiyozidi shillings 5,000....

Sasa sijui maelezo yangu yameeleweka kwa wahusika?
 
We jamaa, ndoto zako za asubuhi zinavivuli, embu stuka kidogo akili ikukae zawa huenda una andika ili wakuone una mawazo ya kurahisisha ukusanyaji.
Unatambua kuwa watu wanasomeshwa wanapata ajira then wanalipa kodi? Unatambua kuwa watu wanasoma na kutumia elimu yao kijenga nchi?
 
asante mjanja. Mimi ninajipendekeza...
 
Ovyo kabisa, pesa za Escrow zimerudi? richmond? kagoda?
if not why unataka kutia umasikini wananchi wenzako? serikali hii ya Tz ni kama tembo aliyedondoka kila mtu mwenye kisu atajikatia nyama kulingana na makali na nafasi yake.
asante mjanja...
 
Good morning.

Mimi huwa nikiamkaga na ideas nakimbilia jamiiforums kushauri, naombeni mnisamehe kama nitawaudhi watu humu leo, but I'm speaking my mind....

Kama sijakosea, ninadhana kuna sheria inayomuhitaji muajiri kwa hapa Tanzania kuwatambua waajiriwa wao waliosomeshwa na bodi ya mikopo kisha ku-withhold makato ya mishahara yao na kuyafikisha serikalini kila mwezi.

Sasa katika kuwapunguzia waajiri (ikiwemo serikali pamoja na taasisi zilizo chini yake) mzigo wa kuwatambua wadaiwa wa HESLB, nilikuwa ninashauri serikali kupitia uongozi wa HESLB wawe wanatoa "Loan Clearance Letter" kwa kila mtu anayeomba kazi aidha awe alisomeshwa na board ya mikopo ama la.

Hii inamaanisha kila application letter ya maombi ya kazi iwe inaambatanishwa na nakala ya kivuli ya clearance letter kutoka HESLB ambayo board itakuwa inatoa kwa kila applicant kwa fee isiyozidi shillings 5,000....

Sasa sijui maelezo yangu yameeleweka kwa wahusika?
wazo lako ni zuri lakini sasa inamaana watakuwa wanatumia hiyo 5,000/= kwa kila application?
 
Ovyo kabisa, pesa za Escrow zimerudi? richmond? kagoda?
if not why unataka kutia umasikini wananchi wenzako? serikali hii ya Tz ni kama tembo aliyedondoka kila mtu mwenye kisu atajikatia nyama kulingana na makali na nafasi yake.
wewe ni mdaiwa sugu inaonekana
 
Kwenye transcript za vyuo kuna sehemu wameandika sponsor:HESLB kama huna mkopo sponsor: private, hivyo hamna haja ya unachokitaka.
 
Una mawazo mazuri mkuu, ila hapo kwenye malipo ya 5,000/= hapajakaa vizuri. Ukisema kila muombaji kazi alipe hiyo amount huoni km unaumiza watu!

Kumbuka sio wote walisomeshwa na board. Pia hapo huoni utakua umetengeneza kamradi kawatu kujipatia mamilioni ya pesa pasina toa jasho!
Labda ungekuja na wazo la kuishauri board (HESLB) watafute namna ya kukaa na waajiri waone jinsi gani watatengeneza form iwafikie waombaji kazi bureeeee kabisa hapo ningekuelewa.

Wazo nzuri ila linahitaji marekebisho. Otherwise sijakuelewa ulichomaanisha.
 
Back
Top Bottom