USHAURI WA BURE:Swala Kuhusu Ufugaji wa Mifugo aina yoyote, Uliza hapa utapata Jibu bure

ushauri please mimi nahitaji kuanzisha mladi wa kufuga kuku wa mayai na nyama, ila ndio kwanza nafikiria utengenezaji wa banda ni changamoto gani nitakayoikabili
 
1. Mimi nafuga mbuzi wa kienyeji. Nina mbuzi 24. Nina matumaini makubwa ya kuwa huko mbeleni mfugo huu uje unisaidie, lakini sijui nifanyeje ili kuufanya uwe more productive and profitable
2. Kuna mgonwa gani ambayo mara nyingi huwa yanasumbua mbuzi, dalili zake nadawa za kutib magonjwa hayo?

Ahsante.
 
asante kwa kutupa nafasi sisi wafugaji tukuulize,mimi nataka kukuuliza mimi nahitaji mbegu bora ya kuku wa kienyeji naweza pata wapi, inayo zaa sana,inahimili magojwa na kuku wanakuwa na uzito mkubwa kuanzia kg3.5
 
Mimi naomba unichanganulie jinsi ya kuchanganya chakula cha kuku wa nyama mwenyewe kwani wauzaji wa hivyo vyakula huwa hawatabiriki bei zao na kutuweka wakati mgumu sisi wafugaji. Naomba kwa kutumia mfano wa gunia moja la chakula cha kuku 100
 
Kaka habari ya majuku, mimi nina tatizo la VICHECHE na NYOKA wanaokula sana mayai wa kuku wangu na kuhatarisha maisha ya vifaranga, naomba ushauri nifanye nini?
 
Kuku wangu wana tatizo la kutokwa na utumbo makalioni hali inayosababisha vifo kwa kuku wengi hasa anapoanza kuugua mmoja.Kuku wangu ni wa kienyeji na mpaka leo sijajua huo ni ugonjwa gani na hata kama nikitaka kuwapa chanjo,sijui ni chanjo ya aina gani natakiwa kuwapa!Msada wako tafadhali..
 
jamani mimi nahtaji kujua jinsi ya kupata soko la matikiti kwani karbuni nitavuna bado wiki mbili tu
 
Hivi mkuu nichakula gani kinafaa kumpa mbwa anenepe na kukua vizuri maana unawapa chakula na dawa ya minyoo lakini anakua mrefu tu mwili unakua sio sana, au kunadawa za kuwafanya wawe wakubwa?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom