Ushauri wa Bure kwenu TABOA nanyi wamiliki daladala Dar: namna ya kushughulika na SUMATRA

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Hivi karibuni kumekuwa na mwelekeo wa kutokea mgomo ukiwahusisha TABOA na wamiliki daladala Dar. Punde tukasikia naibu waziri kaingilia kati na kusimamisha yaliyokuwa sheria mpya zisizohusisha wadau zilizokuwa zimepitishwa na SUMATRA ili kuwa rasmi. Mambo ya ajabu mtunga sheria hawahusishi watungiwa sheria. Ni jamii chache sana duniani zinaweza kufika kiwango hiki.

Kama haijatosha ilikuwa TABOA NA UWAMADA tukasikia nasi wasafiri tunatakiwa kuchunga midomo yetu. Hili na lile haturuhusiwi kuongea ndani ya mabasi vinginevyo sisi na hata madereva watakiona. Mhh! twaelekezwa wapi?

Ushauri wa bure kwa TABOA na UWAMADA baada ya waziri kuingilia kati kufuatilia kadhia iliyopo, mnapaswa kushirikisha wanasheria upande wenu ili kuhakikisha maslahi yenu na wateja wenu pia yanazingatiwa. Pamoja na umahiri mnaoweza kuwa nao katika mapambano yenu dhidi ya udhalimu wa hawa wenye mamlaka bila ya kuwa na mchango thabiti wa wanasheria jitihada zenu zitaishia ukingoni.

Kubalini gharama, husisheni wanasheria nguli katika mapambano yenu. Palipo na nia pana njia. Mtaukumbatia unyonge hadi lini? Kwa sababu ya unyonge wenu, hakuna sekta inayodhalilishwa na kusukumwa huku na kule kama sekta hii ya usafirishaji. Kila mtu anajua tokea polisi asiye miliki hata baiskeli hadi yule aliyekuwa mmiliki wa UDA na KAMATA japo yeye yalimshinda.

KIla la Kheri katika mapambano yenu. Alisema muungwana mmoja wakimalizana na wao watahamia kwenu. Wakasema waswahili "Ukiona mwenzio ananyolewa zako tia maji."
 
Chunga mdomo wako! Hayo sasa makubwa, waweke na kamera manake kuna watu wana chat mwanzo hadi mwisho wa safari
 
Kwingine kazi ya mamlaka kama hizi ni kufanya usafiri wa umma kuwa kimbilio la wote. Watu waache magari yao watumie magari ya umma. Kwetu usafiri wa umma ni source nzuri ya mapato kupitia faini zisizokuwa na kichwa wala miguu.

Ama kweli watanzania tumelogwa na aliyetuloga keshatangulia mbele za haki.
 
katazo halikuwa watu wasiongee mambo yao ktk mabasi hapana. walizuia wale wanaoingia na kuanza kuhubiri kila basi. utakuwa ulielewa vibaya.
 
Back
Top Bottom