Ushauri wa bure kwa watoto wa viongozi wa nchi yetu ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa watoto wa viongozi wa nchi yetu ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JUST, Apr 4, 2012.

 1. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni vyema nyinyi watoto wa viongozi mfahamu kuwa sio kila binadamu anaweza kuwa kiongozi. uongozi ni tunu kutoka kwa mwenyezi mungu wengine hupata karama tufauti amabazo zikitumika vizuri jamii itafaidika. hivi niwaulize nyinyi watoto wa viongozi hamna taaluma au mambo mengine ya kufanya zaidi ya siasa za kutafuta uongozi, hamuwezi kubaki kuwa wanachama wa vyama vyenu na mkavitumikia kwa kuvipa ushauri ili kuleta manufaa katika taifa.

  Nyinyi watoto wa viongozi jaribuni kubadilika someni alama za nyakati, wako wapi watoto wa gadafi, yupo wapi mpinzani wa nasari arumeru, wananchi wa Tanzania wamebadilika, wamesoma, wanuelewa na wanaweza kuongoza bila ya ninyi. chukueni hatua mapema acheni siasa za kifalme, fanyeni mambo mengine ya taaluma zenu mapema kabla upepo wa kusi na kasi haujawazolea mbali na kuanza kujuta pasipo kupata majibu.
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Riz1,nape,emanuel nchimbi,kigoma malima,kawawa na mdogo wake,husen mwinyi,wilson malesela(nanga boy)sofia simba,sioi n.k
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Yaani mkuu wanakera hawa watoto wa vigogo wao tu ndio wanataka kutawala hata bbada ya baba/mama zao ku-prove failure!
   
 4. M

  Murukulazo JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 576
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  nadhani wameshaona hii ni nchi ya kifalme au hata hao wazazi wao wanawaambia kuwa wao ni wafalme hivyo wanapaswa kurithishana uongozi.....ila ipo siku yao!
   
 5. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna haja sasa ya kuwafundisha wananchi waache kuchagua watoto wa viongozi wanapogombea
   
 6. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani ushauri wako ni mzuri lakini ni mgumu kutekelezwa kwa sababu kuu mbili. Moja wazazi wao si wasafi ni wezi wa mali za uma, hivyo basi bila kurithishana madaraka wao watakua katika hali mbaya zaidi maana hawatakuwa na wakuwalinda.
  Pili hawa vijana elimu zao ni ndogo sana, wengine wanaonesha wana vyeti vyenye elimu kubwa lakini hawana kitu, yaani uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. Hawawezi wakapewa ofisi na efficieny ikaonekana.Nadhani wengi wanasoma vyuo visivyotambulika na hata kama vinatambulika hawazingatii masomo.
  Japo si wote, na wale wenye elimu zao nzuri kwa mfano angalia watoto wa malechela kama Mwele, willy na wengine, then walinganishe na akina siyoi, ridhiwani, vita, zainabu na lusinde nadhani majibu unayo. Hawa akina lusinde hawana uwezo wa kufanya kitu kingine zaidi ya siasa ambapo wanaweza kwenda bungeni na kulala tu kama wasira
   
 7. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu, Wao husomea uongozi tu !! hata mkisoma darasa moja wao waongeza masomo yaziada ya uongozi.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Si wote lakini na kuwa mtoto wa Kiongozi isiwe kigezo cha kuwahukumu.
   
 9. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu hoja yako ipo vyema. kwa kuongezea tuu napenda kuwashauri wajenge mazoea ya kujitathimini kabla ya kujipenyeza machoni mwa wananchi kwani wataishia kujiaibisha. maana yangu hapa ni kuwa watoto hawa licha ya kuwa ni watoto wa wale tunaowaita WAZITO KTK NCHI HII bado wanabakia kuwa wananchi kama tulivyo watanzania wakawaida. wasitake kutumia mwanya wa kuwa watoto wa wakubwa kujineemesha bali wanapaswa kufuata taratibu zile zile watumiazo watanzania wakawaida kushika uongozi. tanzania imebadilika sana sidhani kama upuuzi huu wa watoto wa viongozi kubebwa kama utavumiliwa! TANZANIA NI YETU SOTE!
   
 10. M

  MalikwaMali Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi ya kifalme tokea enzi na enzi. Hili linajulikana wazi. Viongozi wote wanarithishana mamlaka ya nchi kwa vizazi vyao. Tunasubiri nguvu ya umma, labda itakuwa ndio muokozi wetu. Peoplessssssss.
   
 11. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu umemsahau January.. Nguvu na fitina za baba yake akiwa kama Katibu Mkuu wa CCM ndizo zilizompitisha mwanawe na kumbwaga Mzee Shelukindo..
   
 12. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua wanategema nguvu za wazazi wao kupata madaraka, wote wamejichimbia CCM ili kupewa support ya wazazi wao. Wenye vipaji vya uongozi wanajitofautisha na kujichnganya na Watanznia nje ya CCM ni Makongoro Julius Nyerere (amewahi kuwa NCCR) na Vicent Kiboko Nyerere (CDM).
   
 13. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu.. kwangu mie kama mtoto wa kiongozi alikuwa na historia ya kuwa kiongozi toka anasoma secondary huko cina tatizo nae.. Tatizo asilimia kubwa ya hawa wanaoingizwa kwenye uongozi wa kisiasa na wazazi wao hawana historia hiyo.. Wengi hata kuwa monitor kwenye madarasa yao hawajawahi kupewa..! Unachogundua ni wazazi wao kutaka kujiwekea mfumo wa kisultani ili wawe salama pindi watakapostaaf.. Tukemee tabia hii.. Machafuko Arabuni yanaletwa na tabia hii ya kurithishana uongozi wa kisiasa.. Tanzania siyo kiciwa.. Yatafika tu na hapa ciku moja kama tutaukubali mfumo huu..
   
 14. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Katika wote wewe ndio umeongea, leo asubuhi nilikuwa nadiscuss hii issue, nasema afadhali watoto wa malecela wamesoma tofauti na wengine, na ndio maana wanakimbilia uchaguzi... lakini hata hivo huyu william nae amekaa kama sharobaro !
   
Loading...