Ushauri wa bure kwa Warumi waliokatwa mikia na wengineo

infinite_

Senior Member
Sep 10, 2013
127
125
Roma ya leo si ile Roma ya zamani, tawala ambayo ilikuwa na nguvu kubwa sana duniani yenye kuweza kutawala na kuendeleza Ustaarabu wa Kirumi kwa miaka na miaka hapa Ulimwenguni.

Sifa kubwa za Warumi walikuwa na Jeshi imara lenye nguvu kuweza kupigana vita na kupata ushindi kwenye falme na tawala mbalimbali duniani kwa miaka na miaka.

Ukristo ulienea kwenye Dola ya Kirumi na hatimaye ulipata hali/hati ya kisheria na kukubalika na Mfalme Constantine mnamo mwaka wa 313 CE, Mnamo mwaka 380 CE, Ukristo ulipata ushawishi mkubwa zaidi wakati ilipokuwa dini rasmi ya Dola ya Kirumi, hivyo basi wanaoujua ukristo kwa undani zaidi ni Warumi.

Pale mtu fulani alipoambiwa jana asijaribu kuwa More Christian than the Romans, ni kwamba asijifanye kuwa Mkristo sana zaidi ya Romans wanaoujua ukristo zaidi maana wakati huo Christins walipoingia kipindi hicho ilikuwa imejikita ndani ya dola ya Kirumi na ikawa dini rasmi ya Dola ya Kirumi.

Swali la Msingi hapa, Je kwenye hii Statement "ASIJARIBU KUWA MORE CHRISTIAN THAN THE ROMANS", Ni watu gani haswa ambao ndio wamejinasibu kwamba wao ndio the Romans??? Je kuna kundi kubwa nyuma ya pazia wanaojifananisha na Warumi?? na kama ndio hivyo basi Warumi hawa wetu wameonesha waziwazi bila ya kificho kwamba wamejipanga with tactics kupata ushindi (conquering) kurudisha dola yao ya zamani kama sifa kubwa ya Warumi ilivyo.

Pia kuonesha kwamba ni wazi pasipo na shaka au ni kweli yale yanayosemwa kwamba Mh. Membe anapanga kuwania kupata tiketi ya Urais kupitia CCM mwaka 2020 ni pale aliposema "Kwanini Uchumi wetu upo hapa ulipo, Kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao", Hii Statement kwa mtazamo wake inaonesha waziwazi kutoridhishwa kwake binafsi kwa jinsi mambo yanavyokwenda hapa nchini na kutokubaliana na current policies.

Ushauri Kwa watawala wa sasa, Mjipange Strategically and tactically kupambana kisiasa kama mngependa kuendelea kutawala kwa awamu ya pili maana huyo Mh. Membe ameonesha waziwazi nia hiyo ya kugombea Urais kupitia tiketi ya CCM na wala si kificho tena na pia mtambue ya kwamba nyuma yake kuna kundi kubwa la Warumi nao wamejipanga haswa haswa ifikapo 2020 na sifa ya Warumi ni kushinda na nia yao ni kurudisha utawala wao madarakani na wanachukizwa na kinachoendelea hivi sasa kutokana na mitazamo yao.

Pia ningependa kuwashauri mjipange haswa haswa mkiwa na watu wenye caliber za Kirumi ili kuwashinda Warumi na hakikisheni watu hao kweli wapo loyalty kwenye kundi lenu ili wasije wakawageuka na kuleta damage au kusababisha anguko lenu, na mwisho muwaondoe watu kama kina Musiba sababu hawana la maana na muongeze vijana wanaojua fitina kama Warumi.

Ushauri kwa Mh. Membe na Warumi wengine, Kipindi hiki kaeni mbali na Media, msioneshe yaliyo moyoni mwenu, msioneshe siri zenu na mbinu zenu kwa maana mnawapa adui zenu wa kisiasa sababu za kujipanga kuweza kuwashinda nia zenu za Kisiasa, na kwa Sifa ulizonazo Mh. Membe kama Mwanadiplomasia pamoja na zile sifa nyinginezo, nimeshangazwa sana sana kuona umeweza kuongea hizo Statements na ku-alert wapinzani wenu wa kisiasa. Binafsi kwenye hizo dk 2 ulizoziongea hakika umewaamsha wapinzani wako wa Kisiasa, umeonesha weakness yako kwa maana ungekaa kimya ungepungukiwa na nini na sasa wataanza kujipanga kuondoa nguvu zako za Kisiasa kwa njia zozote so anzeni kuzijipanga mapema with countermeasures.

Endapo Mh. Membe atafanikiwa anachokitaka, basi ndie atakuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM (ni swala gumu sana sana ingawa strategically linawezekana), na endapo akishindwa anachokitaka basi itakuwa ndio mwisho wake wa Kisiasa kwake au ndio utakuwa mwanzo wa kuwa Mpizani mkubwa nje ya CCM na uenda wakaamia upande wa pili na kama likitokea hili basi Wapinzani wajipange kumpokea Mh. Membe na Warumi wenzake na kumteua kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Upinzani, na endapo Mh. Membe na Warumi wenzake kama wakihama kuelekea Upinzani na wakati huohuo CCM itakayobakia haitojipanga sawasawa basi uenda ndio ikawa kwa mara ya kwanza Serikali ya Tanzania itaendeshwa na Wapinzani na sio CCM kwa maana wapinzani uenda watashinda; na endapo Warumi hawa waliokatwa mikia wakishindwa tena kwa mara ya pili kwenye Uchaguzi mkuu wa Urais basi wajipange kuelekea Zimbabwe maana hawatokatwa mikia tena na kitachofuata ni kuchunwa ngozi kisiasa.

------------------------------------------

Angalizo: Uchambuzi huu upo neutral na hauegemei upande wowote, Ikumbukwe mimi sio Mwanasiasa wa chama chochote cha Siasa na siku zote mimi kazi yangu ni kushauri na nipo hapa kutoa ushauri kwenye mambo mbalimbali muhimu hapa nchini kwa faida ya Taifa la Tanzania na Watanzania.
 
Binafsi napenda jiwe akae hata miaka 70 madarakani ili tuone sera zake za uchumi zitatutoaje kwa mfano
 
Good to know...Ila Kikatiba 10 ndio inatosha au unasemaje?

Wakina sisi yoyote yule kwetu ni sawa ili mradi tu aiweke Tanzania (National interest) na Watanzania mbele na Taifa letu lizidi kusonga mbele...


Binafsi napenda jiwe akae hata miaka 70 madarakani ili tuone sera zake za uchumi zitatutoaje kwa mfano
 
Sinunuliwi, Sijawahi kununuliwa na mtu yoyote wala sina chama chochote cha siasa wala sina upande wowote, hapa nilichofanya ni kufanya Calculations na kuona possible outcomes then kushauri pande zote mbili...Na hapo bado sijaongelea possible outcomes za kuitwa kwenye kamati za Udhibiti na nidhamu au kuvuliwa uanachama au fitina nyinginezo...

...Ndio maana nikashauri ni bora kukaa kimya mpaka dakika za mwisho kama kweli anataka kuipata hiyo nafasi then kumshtukiza mpinzani wako wa kisiasa dakika za mwisho...Alichofanya jana kwa kutoa ile Statement kwenye zile dakika mbili kwakweli bado siamini kama ni yule ninayemjua kiundani, Siamini kama ni yule Mwanadiplomasia ninayemjua au ni yule mwenye sifa kedede muhimu nazozijua...Sifa za mtu kama yeye ni kukaa kimya na mengine ufuata, hapo amekosea na ameonesha weakness.

...Let your plans be dark and impenetrable as night, and when you move, fall like a thunderbolt.

Umepewa bei gani?. (Eti atahamia upinzani na ateuliwe kugombea). Mgombea wetu tunamjua na hatuyumbishwi safari hiu
 
Moja ya tatizo kubwa hata ndani ya kanisa katoliki ni kutohangaika kujua syllabus ya seminary zao na hatimaye watu wanaishia kudhani kila aliyepita seminari ameiva mnavyodanganyana.

Hakuna tofauti kati ya Magufuli na Membe katika usomaji wao wa seminari. Wote wawili wamesoma zinazoitwa Minor Seminary, kwa kiswahili Seminari Ndogo.

Hizi seminari ndogo ni kama Nyegezi (Mwanza), St. Peter (Morogoro), Visiga (D'Salaam). Kimsingi hizi seminary ni Secondary school kama zingine tofauti yake kuna somo la dini na ratiba ya kusali.

Tena ni seminari za majimbo na siyo kama Maua Seminary ya wakapuchini inayosifika kutoa vipanga nchini kama John Mnyika.

Seminari hizi (za majimbo) hazina kitu cha kutisha na mtoto akitoka kule hana alichobadilika.

Hivyo kama Membe kaongea basi katumia physiology aliyojifuza kwingine lakini siyo Seminari unayodhani ambayo hata Magufuli kaipitia.

Utatambua tu kuwa Membe alisoma seminary kwa kauli zake.
 
Utaratibu ni miaka kumi Magu tu labda anaogopa kivuli chake mwenyewe ndio madhara ya kupokea ushauri wa Kagame anaishia kujihami na vitu ambavyo havipo.

Kama anamuogopa Membe ivyo (ambae tetesi hata passport washachukua asisafiri) CCM ndio ataiweza kama wakiamua kuachana nae 2020.

Watu washamuwakishia ni miaka 10 ya utaratibu awaachie mafundi ndani ya chama wapambane na vihere here wakijitokeza kama ilivyo desturi yao pia.
 
...Soma polepole, tulia alafu tumia akili kutafakari kupata utambuzi kwa kile kilichoandikwa.

...haki anayo na ndio katiba ya chama chao inasema hivyo sio?? tatizo ni taratibu zao zilizopo na Kinyang'anyiro walichonacho maana wahenga wanasema a custom is like a law (Kawaida ni kama sheria)...na ndio uchambuzi huu ulipojikita, Je atafanikiwa au hatofanikiwa?? and other possible outcomes , etc

Infinite_
Umeongea sana lakini topic nzima imejaa kuonyesha maguvu, ama ya Membe yanayoshindana na maguvu ya JPM.

Nimetafuta walau sentensi inayoonyesha kama Membe hana haki hiyo nikaona hakuna hata moja.

Hivyo, tamko lako halina maana.
 
Back
Top Bottom