Ushauri wa bure kwa Wapinzani Uchaguzi Mkuu wa 2025

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,554
44,725
1. Vyama vyote vya upinzani unganeni muunde chama kimoja vunjeni vyote ubaki ushirika wa chama kimoja na kisiitwe chadema au cuf au act kitafutiwe jina lingine na hata bendera nyingine rangi na nembo nyingine kabisa.

2. Vijana wahamasishwe kujitokeza kupiga kura. Nasema hivi kwa sababu Mimi nilikuwa msimamizi wa kituo cha kupiga kura japo tuliapa hatutatoa siri lakini nawaeleza ukweli mchungu ndugu zangu wapenda mabadiliko siku hiyo orodha ya kituo changu ni watu 450 lakini walifika watu chini ya 150 na wote walikuwa wanasalimiana na wakala wa CCM, means wanajuana. Yaani CCM kina wapiga kura wake wa uhakika.

Wakala wa Chadema yeye katokea mtaa mwingine hamfahamu mpiga kura hata mmoja sasa imagine kwa hali kama hio kweli utakishinda chama cha CCM. Ndugu zangu hamasisheni Watu wapige kura kwa wingi we angalia hata marekani wasingejitokeza watu wengi Biden asingeshinda.

3. Msipige kampeni sana kwani maisha yenyewe ya sisi wabongo ni kampeni tosha; cha msingi nyie kuweni ma demokrasia kwenye vyama vyenu sio mnataka mkae nyie tu miaka yote Mbowe na Lipumba. Kama CCM wanaweka mwenyekiti miaka kumi nyie fanyeni hata mitano mitano mnachagua mwingine hii mbinu itawapa matokeo.
 
Utakuwa unaishi nje ya nchi wewe kiaisi hujuhi hat nini kilitokea mwaka huu na ni nini jibu lake. Hiki unachoandika hakisaidii kitu.
 
Umenena vema na ujumbe huu uwafikie Zitto na Mbowe!

Bila kuwa na chama kimoja chenye nguvu,katiba mpya na tume huru!

I will never vote again!
 
Back
Top Bottom