Ushauri wa bure kwa wanafunzi wa UDOM waliorejeshwa nyumbani (ushauri wa kisheria)

Dr Salla

Member
Aug 22, 2013
16
22
USHAURI WA BURE KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA MAALUM YA UALIMU WA SAYANSI AMBAO WAMERUDISHWA NYUMBANI KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA.

Kwanza ninachukua fursa hii kwa yaliyowakuta. Kwa ufupi ni kwamba mmeonewa. Sasa kuna kitu kinaitwa "Administrative Law" kwa kiswahili tunasema kuwa ni sheria ya kiutawala.

Misingi ya hii sheria ni kumtetea yule ambaye anakuwa ameonewa katika taasisi fulani iwe ni kazini, shuleni, chuoni n.k

Mnachopaswa kufanya ni ninyi kumtafuta mwanasheria au kuomba kuomba msaada wa kisheria ili muweze kufile mahakamani kitu kinachoitwa "Prerogative Orders" na kisha mahakama iweze kuingilia kati suala lenu!

Prerogative Orders ni amri za kimahakama ambazo hutengua maamuzi fulani ya taasisi au mahakama zilizopo chini ya hiyo mahakama. Kwa Mfano ukitaka kuomba prerogative orders hapa Tanzania unapaswa kwenda mahakama kuu kwa sababu mahakama kuu ndiyo yenye mamlaka ya kisheria ya kutoa hizo amri japokuwa hata mahakama ya hakimu mkazi inaweza kutoa hizo amri kulingana na aina ya kesi.

Mtakachokifanya ni kuanza kufile maombi ya kufile shauri kwa mfumo wa "representative suit" ambapo mtaorodhesha majina yenu wote ambao mnataka kufungua kesi kisha mtamchagua mwakilishi wenu na huyo mwakilishi wenu ndiye atakayekuwa akienda mahakamani kwa niaba yenu kwa sababu haiwezekani kwa wanafunzi wote 7,000 kwenda mahakani kusikiliza shauri kwa wakati mmoja kwa hiyo hiyo kesi yenu itasomwa kama ifuatavyo

Mf. Donati Salla and 6999 Others vs the University of Dodoma.
Mkishapeleka maombi ya representative suit ndipo sasa mfungue shauri lenu na muombe prerogative orders sasa kwa hali iliyopo itabidi muombe hati ya dharura mahakamani ili msikilizwe haraka.

Mimi nimewapa utangulizi tu ila mkipata mwanasheria hapo mlipo atawasaidia kwanza kuwasilikiza ili awezekutathmini uhalisia wa malalamiko yenu na kisha ataona ni nini kifanyike ili mpate msaada wa haraka lakini mkaa kuwasikiliza wanasiasa, mtabaki kuimbiwa ngonjera za pole lakini mwisho wa siku hamtotaua tatizo lenu! Ninyi mmempoteza muda wenu n.k sasa ni lazima mfidiwe kwa sababu hamkujipeleka UDOM wenyewe.

Akili za kuambiwa changanya na za kwako!
Kila la kheri katika kuipata haki yenu!!!
 
Tatizo ni kuwa wameshachangukana!
 
Kwa Nchi za wenzetu hilo linawezekana ila kwa hii yetu tutaishia kufeel sorry kwa hawa vijana, kiukweli wamepotezewa muda sana ata km kweli kuna baadhi yao ambao walikuwa hawana vigezo ila maamuzi ya serikali imekuwa km ni kuwakomoa, ss km mkuu wetu anasema alikuwa anasubili wanafunzi wa UDOM wagome then wafukuzwe wote ss unazani kwa hawa elfu 7 anajiskia chochote kweli km mzazi, na km wakifungua case ujue wakili wa serikali atakuwa dr tulia
 
Hili swala lingemalizwa kiofisi,ona sasa aibu kwa serikali,na kuwapotezea muda watoto wetu na divisheni zao za nguvu
 
Nimeona malalamiko mengi Sana kutoka kila kona ya nchi kuhusu wanafunzi wa UDOM kufukuzwa.
Swali langu ni kuwa kwanini Watanzania hatutaki kuamini kuwa serikali haiwezi kushtakiwa. Hata wanaharakati ambao tulikuwa tukiwasikia zamani wamenywea na hawasikiki
Nendeni mahakamani, muiombe Mahakama iwarudishe chuoni. Aliyewafukuza ni Uongozi wa Chuo na sio Ikulu, maana Ikulu hawana mamlaka kwa mujibu wa sheria iliyoiunda Chuo kutoa adhabu kwa wanafunzi. Hata wale wa TCU walilalamika Kama watoto kuwa wamefukuzwa kinyume cha sheria. Gazeti la Mwananchi sio Mahakama. Nendeni mahakamani muombe haki zenu.
Mkifanya hivi Mara mbili maamuzi ya kukurupuka yatapungua.
Ingekuwa Kenya, mna fikiri serikali ingekuwa na kesi ngapi za kujibu.
Poleni wadogo zang
 
Mkuu kwenye kichwa cha mada(uzi) umeanza na neno swali.
Hivi ni kweli hicho kichwa cha mada ni swali?
 
Mmeambiwa heshimu mamlaka zenu,huwezi shindana na anayekutungia mitihani na pia unayetegemea akupe cheti na kukuajiri pia.
 
magu katuchanganyia hbr ss kwenye program yetu hatukupata hzo d4 wala hatukuwa na fo walidahiliwa wanafunz waliokuwa na ufaulu wa daraja la kwanza, la pili na la tatu tu kwenda kusoma hiyo course udom, issue ya st.joseph kaicombain na ya kwetu kuwa tulipata fo wote. Lakin ukwel utaeleweka tu ss hatukubal kupotezewa muda namna hyo halafu wanatuacha hewan.
 
Mkuu kwenye kichwa cha mada(uzi) umeanza na neno swali.
Hivi ni kweli hicho kichwa cha mada ni swali?

Mzee hiyo ilikuwa typo mkuu. Lakini turudi kwenye mada Watanzania tunapenda Sana kulalamika lakini hatuna strategy za kutaka kuondoa malalamiko.
Wewe umeonewa unawaita waandishi wa habari really?
The same na wamasheria sijui wateja wa kesi zao wanawapata wapi, kwenye hii issue ndo promo hasa wanasheria ambao hawatambuliwi hapa anawakikisha bure halafu anawaaambia wanafunzi wote said mahakamani kwa amani wajaze viwanja vya mahakama ili TV nao wapate news
Da!
Kweli bongo tambarare
 
magu katuchanganyia hbr ss kwenye program yetu hatukupata hzo d4 wala hatukuwa na fo walidahiliwa wanafunz waliokuwa na ufaulu wa daraja la kwanza, la pili na la tatu tu kwenda kusoma hiyo course udom, issue ya st.joseph kaicombain na ya kwetu kuwa tulipata fo wote. Lakin ukwel utaeleweka tu ss hatukubal kupotezewa muda namna hyo halafu wanatuacha hewan.
pole sana mkuu...baba jesca atalipwa na mungu kwa alichowafanyia
 
Mzee hiyo ilikuwa typo mkuu. Lakini turudi kwenye mada Watanzania tunapenda Sana kulalamika lakini hatuna strategy za kutaka kuondoa malalamiko.
Wewe umeonewa unawaita waandishi wa habari really?
The same na wamasheria sijui wateja wa kesi zao wanawapata wapi, kwenye hii issue ndo promo hasa wanasheria ambao hawatambuliwi hapa anawakikisha bure halafu anawaaambia wanafunzi wote said mahakamani kwa amani wajaze viwanja vya mahakama ili TV nao wapate news
Da!
Kweli bongo tambarare

Ukifungua Law Suit dhidi ya mtu mbabe, ishirikishe media katika hatua fulani kama hutopenda kesi yako iishe ukiwa na hali mbaya. Acha umma ujue nini kinaendelea, kuliko kufanya kimya kimya ilhali unajua mshtakiwa nyani hakimu ngedere.
 
Back
Top Bottom