Ushauri wa bure kwa wadau wa FILAMU Bongo

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Mimi ni miongoni mwa waTanzania wengi tunaopenda kuangalia filamu zetu za hapa Bongo lakini wengi wetu tunakatishwa tamaa na maudhui ndani ya filamu hizo. Nyingi zimejaa mambo ya anasa, majumba na magari ya kifahari ambayo hayaleti taswira halisi ya Watanzania wa kawaida mabo tuko wengi.

Badala ya kuiga wenzetu wa kule Nigeria ni bora mngekuja na filamu zinazobeba maudhui ya maisha ya kawaida ya Mtanzania hivyo kupiga hatua kwa kupendwa na waTanzania wenyewe pamoja na hata nchi za jirani na ama kwa hakika tutafika mbali. Hebu badilikeni jamani twazipenda sana kazi zenu ila mnaelekea upande ambo si wenyewe la sivyo tutaendelea kuangalia series za nje na soka la Uingereza.

DSC01037.JPG
DSC01021.JPG
DSC01977.JPG

Picha kama hizi hazina mvuto wowote maana hazibebi uhalisia wa maisha yetu



Publication3.jpg

473651301_133123d44a.jpg

Maasai.JPG

Haya ndio maisha yetu halisi mwaweza tumia maudhi haya na mkauza sana kazi zetu
 
SOKO la filamu za Tanzania linaonekana kuchukua nafasi kwa kasi kubwa lakini imekuwa inaonekana kwamba huenda likaporomoka ndani ya kipindi kifupi kutokana na mfumo wa waigizaji kupenda kufanya mambo kwa urahisi zaidi.

Ulahisi huo umetokana na waigizaji kupenda kuigiza namna ambavyo waigizaji wa Nigeria wamekuwa wakifanya na mbaya zaidi hata waandikaji wa stori wamekuwa wakiigiza zile za Nigeria tu maarufu kama Nollywood.

Mwigizaji maarufu wa vichekesho nchini, Mzee Small ameiambia Mwanaspoti kwamba iwapo wasanii nchini watapunguza tabia ya kuiga hadi hadithi, Tanzania itafika mbali zaidi.

"Kuna wasanii wengi sana, nawaona tu Ray, Kanumba na wengine wengi. Lakini wadau wanawalaumu tabia ya kuigiza filamu ambazo tayari zimeonekana Nigeria au India.

"Tanzania wasanii wako na wenye uwezo wa juu, hakuna haja ya kuiga Nigeria na badala yake tunatakiwa kuwa na vitu vyetu wenyewe ili kuwapa changamoto hao washindani wetu," alisema.

Mwigizaji mwingine wa vichekesho, Mwinshehe Mzange maarufu kama Kingwendu alisema, tatizo kubwa ni uvivu na fedha ya haraka haraka.

"Kila mmoja anataka kufanya mambo haraka haraka basi, kama kweli hadi hadithi tunaona hatuwezi kutunga hauoni hilo ni tatizo. Bila ya kuiga tunaweza kufanya vizuri," alisema Kingwendu akisisitiza suala la kujiamini.

Lakini mmoja wa waongoza filamu maarufu nchini, Mrisho Mpoto alisisitiza suala la waigizaji, waandishi wa filamu na wanatakiwa kujiendeleza zaidi katika elimu ya sanaa hiyo kwa lengo la kuendeleza fani hiyo.

"Kweli kuna makosa ambayo yanaweza kupungua taratibu taratibu ingawa suala la kujiendeleza kielimu kuliko kutumia kipaji pekee ni muhimu sana," alisema Mpoto ambaye ameibuka na kuwa mmoja wa waongoza filamu mahiri.

Filamu za Tanzania zimepata umaarufu mkubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na pia kasi ya kuonyeshwa katika televisheni ya Afrika Magic Plus ambayo inaonyesha filamu nyingi za Nigeria maarufu kama Nollywood.

Nchi nyingine ambayo imejikusanyia umaarufu mkubwa kutokana na utengenezaji wa filamu ni Ghana ambayo waigizaji wake wengi wamekuwa wakishiri katika filamu mbalimbali za Nigeria.

Ingawa Tanzania imekuwa kati ya nchi zilizowahi kushirikiana na waigizaji wa Nigeria, suala la kuiga au kukopi kupindukia limeonekana kuwa moja ya tatizo sugu linalofanya kasi ya Tanzania ishindwe kuwa ya juu.

Kujitokeza kwa waigizaji wengi chipukizi wakiwamo wasichana kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jokate Mwegelo na wengine kumechangia kuongeza umaarufu wa filamu za Bongo ambazo hata hivyo zinaonyesha kwamba zinahitaji maboresho zaidi ili kufikia viwango vinavyoweza kuitwa vya kimataifa.
 
Mbali ya kuiga filamu za Kinigeri na maudhui ya mapenzi tu sijaona kitu kingine cha maana ni kama bongo fleva kila wimbo ni mapenzi tu hivi hii dunia ni mapenzi tu. Nafikiri mapenzi hayakuanza katika hii dunia maana Mungu alipomuumba Adamu alimweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza eva aliumbwa mwisho. Hivyo nafikiri Mungu alihimiza zaidi Kilimo Kwanza au kufanya kazi kwa bidii. then mapenzi baadae. Enyi wasanii punguzeni kuiga, pungunguzeni maudhui ya mapenzi tungeni vitu vinavyoendana na uhalisia kama ukeketaji, utunzaji wa mazingira na mengineyo mengi yafananayo nahayo au mwaona vitakosa soko?
 
Back
Top Bottom