illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,118
Naishi Dar ila familia yangu iko Muheza, kila mara nipatapo muda huwa nawatembelea kuwajulia hali, huwa natumia usafiri wa ratco kwani huwa ni wa uhakika, wanajali muda yaani wako serious kiukweli.
Ni muda mrefu sasa nimekosa muda wa kwenda kuwatembelea familia kutokana na pilika za hapa na pale hivyo huwa nikipata kitu kizuri nanunua kisha nawatumia kwenye basi hili hili la ratco kuna mapungufu kidogo nimeyaona ambayo ni vyema uongozi ukafuatilia hili ili isijiondolee sifa yake nzuri.
Nilituma mzigo wa nguo za mtoto pamoja na dawa niliyokuwa nimenunua, mzigo ule haukushuka Muheza kama makubaliano yalivyokuwa badala yake ukapelekwa Tanga mjini.
Baada ya kuwasumbua kwa kupiga simu ofisini mara kadhaa wakaurudisha tena Dar es salaam, kifupi mzigo ulikaa kwenye basi kwa muda wa siku kama nne hivi ndiyo ukaja kupatikana, mtoto alikuwa ameumwa mpaka basi.
Tukio la pili nilitumiwa computer kutoka Muheza siku ya kwenda kuichukua haikuonekana wasijue imepelekwa kwenye ofisi ipi, nilikuja kuiona baada ya siku tatu.
Jana tarehe 24 May nimetuma viatu vya mtoto tena nikasisitiza naomba vifike kwa wakati, mpaka naingia jamvini viatu havijulikani vilipo.
Kuna muhudumu wa kiume wa Tanga ambaye huwa anapokea simu ya mkononi huwa anatumia lugha kali sana, nakumbuka siku moja aliniambia "wewe ni mzembe na huyo unayemtumia mzigo pia ni mzembe mnataka mizigo yenu ipotee kisha mtudai hela nyingi"
Huduma ni nzuri kwa ujumla ila wakishughulia changamoto hii itakuwa nzuri zaidi.