Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 6,376
- 6,720
Mwanangu una hoja yenye mashiko. Wakati wa kuajiri vihiyo umekwishapita.Mara nyingi Huwa napendelea kuonekana mjinga ( being underated/ underestimated). Napendelea kujiweka muonekano usiolingana na uwezo wa akili yangu, kipato changu na elimu yangu.
Wiki iliyopita nilijaza fomu la online loss report Kisha nikaenda kituo cha police kuthibitishiwa hiyo loss report ili niende stationery ku print. Yule polisi mhusika akanidai TZS 5,000 ilihali huduma ni bure ukishalipia ile TZS 500 kwa control number. Tangu siku ile (na matukio mengine kwa nyakati tofauti tofauti) polisi nawachukulia ni watu wa hovyo hovyo na nawashauri wamama wasiwe wanawazaa watu wa hovyo hovyo kama polisi wa nchi hii, kama bwana Zero anavyomchukulia Hamza kuwa ni mtu wa hovyo hovyo na kuwashauri wamama wasiwe wanawazaa watu wa hovyo hovyo kama Hamza.
Ushauri:
Serikali kwa upande Wake, inapaswa kuipa thamani stahili idara ya polisi kwa kuwaajiri watu wenye elimu nzuri na utimamu wa akili na siyo miguvu tu bila akili ( power without knowledge is globally agreed to be useless). Kuna maelfu ya graduates wanazitaka hizo kazi nawana uwezo mzuri tu.
Serikali wapeni graduates kozi ya JKT angalau ya miezi mitatu Kisha muwapeleke shule ya polisi, muone mapinduzi chanya katika idara hii muhimu iliyoigeuza taswira ya Tazanzania kuwa Taifa la walalamikaji kando na wao kuishi maisha ya kihayawani.