Ushauri wa bure kwa rais kikwete na mizengo peter pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa rais kikwete na mizengo peter pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Jun 27, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Natoa ushauri huu kwa rais na waziri mkuu pinda juu ya migomo nchini, ubabe na kujivunia madaraka hakutasaidia kuleta utulivu nchini kinachotakiwa ni kukaa chini kutafakari nini cha kufanya. Ni kweli mna dola, usalama wa taifa na vyombo vingi vinavyowalinda. Lakini vyombo hivyo vnavyowalinda haviwezi kuwalinda siku ya kufa kwenu ikifika. Hivyo kwa maamuzi yoyote mwogopeni mungu kwanza.

  Nani asiyejua kuwa wanasiasa mnajipendelea kimaslahi kiasi kwamba mmepoteza mvuto kwa wananchi, kuna kazi gani mnayofanya ya kumzidi mwalimu, daktari yenye matokeo chanya hata kustahili yote mnayopata, nani kati yenu aliyefika hapo bila mwalimu, leo mwalimu ametelekezwa na kuonekana kituko. Wakigoma mnakimbilia mahakamani mahakama ambazo ni vikaragosi vyenu hazitendi haki bali ni uonevu tu. Mkiona msimamo mnatuma askari wenu ili wateke na kuua. Damu ya watetea haki itakuwa juu yenu. Itamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote lakini aje apate hasara ya nafsi yake.

  Nasikia mnataka kuwafukuza madaktari wote sawa wafukuzeni nchi si yenu milele mendelee kuiba, watetezi wa wanyonge mko tayari kuwanyonga fanyeni hivyo ipo siku moja mtalia lakini nanyi mtakosa msaada.

  Walimu watagoma hivi punde mtakimbilia mahakamani wakikaidi mtawafukuza, jeshi likiamua kugoma itakuwaje? Wanajeshi ni watanzania, hata mkuu wa majeshi anaona mateso wanayopata watanzania, hata kama mnamlipa pesa nyingi nafikiri kuna haja ya yeye pia kukataa uonevu huu, hospitali hazina dawa, bibi zake wanateseka kule kyela, ndugu na marafiki wanaumia. Jeshi mtaendelea kutii amri za serikali? Mahakama mtasitisha mgomo wa walimu ili mendelee kuishi vizuri huku walimu waliowafikisha hapo wakidhalilika, madaktari wanaowatibu wakihangaika. Ona ulimboka anataabika kwa ajili ya kuwasemea wengi.

  Endeleeni kutunyanyasa lakini hata wale madikiteta wengine walidhani vitisho vinasaidia siku ilipofika waliomba msaada haikusaidia, mali haziwezi kuwaokoa. Mungu yupo muogopeni si kwamba hayaoni mnayotenda ila anapenda mfikirie toba. Kama mambo yamewashinda si mkiri kujiuzuru tutawona majasiri.

  Nawathadharisharisha msiwafukuze madaktari kaeni nao fikieni muafaka. Wabunge acheni kushangilia na kuunga mkono kila upuuzi wa serikali unaoletwa kwenu fikirini kabla ya kutenda. Bunge likatae kuwafukuza madaktari baadala yake liiamuru serikali itafute suluhisho vinginevyo mmh!!!!!
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Umenena mkubwa, sidhan kama watakusikia, wakikusikia watasema ni UPEPOTU UTAPITA ana Liwalo na LIWE, na kwa hili Pinda hatoki
   
 3. a

  akelu kungisi Senior Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaumiza sana! Kwa hakika Ulimboka atapona kwa kuwa MUNGU yuko upande wake! Historia inatufunza kuwa hata serikali ikiua mtu haiwezi kuua fikra zake kwakuwa zitaendelea kurithishwa katika vizazi vingine! Naam, KEN SARO WIWA, MASHOOD ABIOLA nk waliuawa na serikali ya dikteta ABACHA lakini haikuendela mbele! CCM na serikali yake wako katika mchakato wa kujichimbia kaburi lao haraka, dalili zimeonyesha! Hata wakimuua Ulimboka fikra zake zitaishi daima! Watanzania tuungane pamoja kupinga unyama huu wa serikali hii kandamizi kwa raia wasio na hatia. Tunawaomba watanzania wote kwa umoja wao kuilaani serikali hii na matukio yake ya kinyama! SOLIDARITY FOREVER!
   
Loading...