Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!

umeandika kwa vitisho sana mkuu ila lengo lenu ni moja tu; kwakua by any means far mnakwenda kushindwa, kete ya mwisho mliyobaki nayo ni ya kuwaaninisha watanzania kua J.K anamuendorse mgombea wenu, ili sasa picha zikishapigwa mzisambaze kila mahali kuonesha kua jamaa wapo karibu, mnatafuta kuhalalisha movement yenu iliyoshindwa, tayari.

kamtego kadogo sana hako
 
Kuna siku JK alisema watu wamejitokeza kwa wiiingi kuomba kupitishwa na CCM kugombea urais...
Inawezekana kuna ambaye hajajitokeza, na tunamuona ana uwezo...tutamfuata na kumuomba achukue form...

Nakumbuka tulianza mjadala na hubby kuwa huyu anazuga au yuko serious....na alikuwa kama anawacheka wagombea hivi walivyo weengi...afu wanataka only 1.

Hapo Membe na wengine walishachukua form....
Isije kuwa JPM hakuwa accident...

Ukizingatia jamaa hana urohoo na uchu wa madaraka....asingeunga trela hivi hivi tu....tena mwishoooni....isijekuwa ndiye aliyefuatwa achukue form....

Japo mimi si CCM nimewavulia kofia...ni chama kubwa ndo maana ni unpredictable...wana hazina kubwa ya wenye sifa (na mafisadi...kwi kwi kwi) ni matter ya ku pick tu...
 
Wanabodi,

Hili jambo ninalolizungumza hapa, ni jambo very serious na la kweli, sio jambo la masikhara, kwa sababu mimi binafsi ni shuhuda na mhanga wa jambo kama hili kuwa ni jambo la kweli kabisa ambalo lipo for real!.

Kwa kuwasaidia tuu watu wasijua facts kuhusu nafasi ya urais, rais ni mtumishi wetu, yaani ni mtumishi wa watu, sisi Watanzania ndio mabosi wake, sisi ndio tumemuajiri ili atutumikie, na ni sisi ndio tunao mlipa mshahara na marupurupu yake yote kwa fedha zetu na jasho letu, hivyo hatupaswi kumuogopa, bali tunapaswa kumuheshimu, na kiukweli tunamuheshimu sana!.

Pamoja na heshima yote kwa rais wetu, mamlaka yote, na madaraka yote, rais wetu na yeye pia ni binadamu, sio Mungu na wala sio malaika, hivyo yeye kama binadamu anaweza kukosea tuu kama binadamu wengine wote!, tofauti ni kuwa, kwa vile urais ndio nafasi ya juu kuliko nafasi zote za uongozi, rais anachukuliwa kuwa ndio yuko juu kuliko mtu mwingine yoyote, na wengine wote waliomzunguka, hujiona wako chini yake, hali inayopelekea hata akifanya makosa ya kibinaadamu, hakuna mtu wa kumwambia rais hapa ulikosea!.

Kwa vile mimi ni mmoja wa raia wake, ninajua kuna kosa fulani amelitenda kumhusu Edward Lowassa, hivyo kwa heshima na unyenyekevu wa hali ya juu sana, namshauri Rais wetu Mheshimiwa sana, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye kiukweli yuko juu, ajisheshe, aende kumuomba msamaha wa dhati Edward Lowassa kwa kosa alilomtendea, kabla ya October 25!.

Msamaha huo sio lazima uwe wa public, anaweza tuu kupanga vile ambavyo ataona inafaa, akutane na Lowassa na kumuomba msamaha kwa kosa hilo alilomtendea, wakasameheana, tarehe 25 October, Watanzania tukaingia kwenye uchaguzi kwa upendo na amani, ili hata ikitokea, Watanzania kwa ridhaa yetu wenyewe, tukiamua kuipumzisha CCM kwa kuiweka pembeni, tuipumzishe kwa upendo na amani,,, na sio kwa chuki na visasi!.

Jee Kosa lenyewe ni lipi linalompasa Rais Wetu Jakaya Kikwete kumuomba msamaha Edward Lowassa?!.
Hapa sasa ndipo heshima, akili, busara, unyenyekevu, ustaarabu, uungwana, ustahimilivu wa hali wa juu unapotakiwa kutumika, kama ilivyo katika familia zetu, Baba ndie Mkuu wa nyumba, hata akikosea, kuna namna ya kumjulisha kuwa hapa baba umekosea, tena anayemwambia hayo baba sio mtoto na sio mama bali ni wazee wenzie wa rika lake, hivyo kwa ruhusa ya mwana jf huyu, naomba kumleta mzee wa rika la JK,

Namalizia kwa kulitaja jambo lenyewe iwapo JK ataamua kuwa hakuna kosa lolote la kumuomba msamaha Edward Lowassa, then naomba kutoa ushuhuda wangu wa kitu kinachoitwa 'karma' kwa vile mimi karma naijua na iliishanikuta, hivyo baada ya October 25 mimi ndio nitakuwa muhabarishaji wa jf every time 'karma' takes its toll!.

Ushauri wa bure kwa wana jf ambao hamjui kuhusu 'karma', nawasihi jisomeeni tuu uzi huu na kujipitia zenu, msije kujitia kimbelembele kumjibia JK unless you are certain and absolute sure what was the name of the game!, and also you know what 'karma' is and its quosequenses.

Kuna watu watajiapiza hadi maneno kama 'over my dead body' hakuna msamaha wowote wa kuombwa kwa Lowassa, then subirieni baada ya October 25, nitawakumbusha kuhusu uzi huu!.

Kwa ajili tuu ya kukuwekea references niliwahi kusema nini na hatimaye nini kilitokea, nashauri, msibeze au kupuuzia ushauri wowote wa bure hata ukitoka kwa chizi, bali pima hoja za kwenye ushauri huo!.

Kwa wageni wasiomfahamu Pasco wa jf, wanaweza kufikiri hii ndio maea yake ya kwanza kushauri, au kulizungumzia jambo halafu likatokea. Naomba niwatembeze kido mitaa hii kwa wale wenye nafasi, muangalie nilisema nini na nini kikata kikatokea!.

  1. Wengi wanadhani mgombea wa CCM, JPM amejiibukia tuu from no where!, or just by chance!, no way, Magufuli hajaibuka for a chance, there are serious reasons, sisi wengine tulibahatika tukaelezwa hizo sababu na tukazileta humu jf tangu 15th August 2014 niliwaeleza watu hivi Mgombea wa CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!
  2. Wakati wa uchaguzi wa Arumeru nilimshauri kitu Lowassa, hakusikia na angalieni kilichotokea.
    Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
  3. Wakati wa harakati za kuutafuta urais, wengi wakitumai ni Lowassa atapitishwa, nilisema hivi na angalieni nini kilitokea!.
    Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

    Pia nimetoa shauri nyingine mbalimbali za bure.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humou

Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim! -

Rais Wetu "Mchelea Mwana Kulia, Endelea Kuwachekea, Ny

Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report:

Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!,

Ushauri wa bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared

Ushauri wa Bure kwa CCM Zanzibar: Kumuepushia Aibu

Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli,

Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko

Ushauri wa Bure Kwa ZZK, "Shika Lako!" Ya Wengine

Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)

Pasco
With just two days to go, hapa nakumbushia tuu, ili yakija kutokea ya kutokea, kusiwepo excuse ya sikujua au sikutarajia kama hili lingeweza kutokea!, sasa ndio hili linakwenda kutokea, keshokutwa Jumapili!.

I respect you so much, but. . . . are you that influential??!??
 
ww mjinga sana wakubaliane kupeana madaraka kwani nchi ya kwao nchi ya watanzania woote.
kwani sioni umuhimu hii mada kuweka humu
 
Pasco umenisaidia kwelikweli kuwa mtu wa kupenda kujisomea na kutunza kumbukumbu. Tusubiri.
 
Nimezaliwa na kukulia hapa hapa Bongo TanZania hii imenipa uwezo mkubwa wa kuwaelewa Watz wenzangu kwa jinsi walivyo hasa tabia zetu!

Moja ya tabia kubwa ya MtanZania ni kwamba siku zote ni Muongo, Mtz wa kawaida ni lazima atakudanganya tu hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo, sijui ni kwa nini lkn tuko hivyo, wewe mpigie simu rafiki yako yoyote yule sasa hivi muulize uko wapi ni lazima atakudanganya, Mtz akinunua gari la Milioni tatu ukimuuliza lzm atakudaganya amenunua milioni 4, ukimwona na mwanamke ukimuuliza atakwambia yule nimetembea naye wakati ni Muongo!

Watanzania siku zote huongea kinyume hivyo kwa kuwa huyu aliyeandika hii mada ni Mtanzania basi naamini kabisa kwamba ni muongo na anachomaanisha ni kinyume chake kwa kifupi anamuombea fisadi Lowasa poo kwa maana mambo yameshakaba na fisadi Lowasa hana pa kutokea, fisadi Lowasa ameshatambua kwamba hawezi kushinda huu uchaguzi hata iweje na ndiyo maana wameshaanza kuongelea kuibiwa kura sasa tume imewabana kila mahali visingizio vyao vyote tume imevifanyia kazi na kuvirekebisha kuanzia sijui kalamu ya kupigia kura mpaka matokeo kubandikwa Kituoni yote yamerekebishwa kila wanaloomba tume inawapa na haya yote yapo kwenye rekord kama ni kushitakiwa Mahakama ya Kimataifa ICC (The Hague) video na audio za ushahidi zipo ambazo akina Tundu Lisu, Mbowe, fisadi Lowasa &Co. wakihamasisha fujo hivyo kwa kifupi wamebanwa, tafiti za Kimataifa za Twaweza zimeonyesha fisadi Lowasa hana chake mpaka leo hii kulingana na tafiti hata wafuasi wa fisadi Lowasa wala hawajui tofauti ya UKAWA na chadema achilia mbali fisadi Lowasa na na Mbowe kwanza wengine wanafikiri Slaa atakuwepo kwenye karatasi ya kura, muda umekwisha Magufuli ameshafika sehemu kubwa ya vijiji wakati fisadi Lowasa wala hajaaanza!

Hivyo namuelewa mleta mada ni kwamba anawatayarisha wafuasi wa fisadi Lowasa kisaikolojia kwani ni kweli Magufuli atamfunga fisadi Lowasa na hilo fisadi Lowasa analijua!

CCM ni Chama Dola na kuna Sababu kinaitwa hivyo!

Taratibu mzee povu hillo linatiririka!
 
Lowassa anakwenda kushinda uchaguzi huu whether we like it or not!

Hili liliandikwa na lazima iwe hivyo. Hivi vifo vya ajabu ajabu vya viongozi wa kisiasa hatuelewi tu maana yake jamani??
 
Urais ni utumishi wa umma, sio suala la makubaliano. Kama Kikwete aliona kwa maslahi ya taifa ni vema Lowassa asiwe Rais na iwe hivyo...
 
Nimezaliwa na kukulia hapa hapa Bongo TanZania hii imenipa uwezo mkubwa wa kuwaelewa Watz wenzangu kwa jinsi walivyo hasa tabia zetu!

Moja ya tabia kubwa ya MtanZania ni kwamba siku zote ni Muongo, Mtz wa kawaida ni lazima atakudanganya tu hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo, sijui ni kwa nini lkn tuko hivyo, wewe mpigie simu rafiki yako yoyote yule sasa hivi muulize uko wapi ni lazima atakudanganya, Mtz akinunua gari la Milioni tatu ukimuuliza lzm atakudaganya amenunua milioni 4, ukimwona na mwanamke ukimuuliza atakwambia yule nimetembea naye wakati ni Muongo!

Watanzania siku zote huongea kinyume hivyo kwa kuwa huyu aliyeandika hii mada ni Mtanzania basi naamini kabisa kwamba ni muongo na anachomaanisha ni kinyume chake kwa kifupi anamuombea fisadi Lowasa poo kwa maana mambo yameshakaba na fisadi Lowasa hana pa kutokea, fisadi Lowasa ameshatambua kwamba hawezi kushinda huu uchaguzi hata iweje na ndiyo maana wameshaanza kuongelea kuibiwa kura sasa tume imewabana kila mahali visingizio vyao vyote tume imevifanyia kazi na kuvirekebisha kuanzia sijui kalamu ya kupigia kura mpaka matokeo kubandikwa Kituoni yote yamerekebishwa kila wanaloomba tume inawapa na haya yote yapo kwenye rekord kama ni kushitakiwa Mahakama ya Kimataifa ICC (The Hague) video na audio za ushahidi zipo ambazo akina Tundu Lisu, Mbowe, fisadi Lowasa &Co. wakihamasisha fujo hivyo kwa kifupi wamebanwa, tafiti za Kimataifa za Twaweza zimeonyesha fisadi Lowasa hana chake mpaka leo hii kulingana na tafiti hata wafuasi wa fisadi Lowasa wala hawajui tofauti ya UKAWA na chadema achilia mbali fisadi Lowasa na na Mbowe kwanza wengine wanafikiri Slaa atakuwepo kwenye karatasi ya kura, muda umekwisha Magufuli ameshafika sehemu kubwa ya vijiji wakati fisadi Lowasa wala hajaaanza!

Hivyo namuelewa mleta mada ni kwamba anawatayarisha wafuasi wa fisadi Lowasa kisaikolojia kwani ni kweli Magufuli atamfunga fisadi Lowasa na hilo fisadi Lowasa analijua!

CCM ni Chama Dola na kuna Sababu kinaitwa hivyo!

Naomba wiki ijayo uje urudie kusoma ulichokiandika. I mean Ijumaa ijayo ndoo utakapoelewa kuwa hata Pasco ni wa hapahapa na sio CIA wala ALQAEDA. Yangu macho
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom