Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!

Siku Lowassa anatangaza nia pale Sheikh Amri Abeid Arusha niliwaambia jamaa zangu huyu ndio atakua Rais ajaye kama atapitishwa na CCM ingawa nisingempigia kura kwani kura yangu ingeenda kwa Slaa(Mgombea wa Ukawa).

Alivyotoswa kwenye tano bora Membe akabaki nikasema jamaa hatakubali Membe aingie tatu bora hivyo atafanya juu chini apitishwe mgombea yoyote isipokua Membe ili wakose wote na kosa alilofanya EL na Team yake kwakua alikua na mpango wa kahamia upinzani ni kumpigia kura Magufuli na kama angesoma post yangu humu noliyosema Lowassa bado anautaka Urais baada ya kukatwa angefanya juu chini wakampitisha yule Mama Amina wa Z'bar au Migiro kwani nilisema Nchi hii bado haijawa tayari kuongozwa na Rais mwanamke tena Mzanzibar.
Na kama wangefanya hivyo na akabaki CCM Slaa au mgombea yeyote wa Ukawa angetinga Ikulu mapema tu.

Sasa kwakua alikua na mpango wa kahamia upinzani yeye na Team yake wangempitisha Amina au Migiro na yeye asingepata hizi changamoto za sasa na CCM wangepata shida sana kuwashawishi Watanzania kumpigia kura Mwanamke kua Rais tena Mzanzibar kwani hata angepitishwa Mzanzibar mwanaume bado ingekua kazi kumnadi na kwa mfumo uliopo Rais wa JMT hawezi toka Z'bar (Rejea walichokifanya kwenye Katiba Pendekezwa)

Ila pamoja na yote Lowassa is our Next President.
 
Wewe kweli hamnazo yani ulitaka uarais arithishwe lowassa? Kwani nchi hii ya kifalme? Huna hoja ya maana.
Wewe mpuuzi sana. Wewe ni nani kuwaamulia mamilioni ya watanzania? Kitu gani special umefanya hadi lile unaloamini ulipe mamlaka? Tulia chini, mimi nina kura moja, na wewe katumie kura yako moja kumpigia umtakaye (kama umejiandikisha).
 
Heee Pasco, unafikri haka ka-Kwere katakuelewa kweli? Nina mashaka sana kama katakubaliana na ushauri wako, kenyewe katakwambia ni upepo tu utapita!!

Ila mimi nahisi haka kamjamaa huenda kametula kekundu kuvunga kwamba wamekorofishana kumbe wako wamoja, hivyo tusije tukashangaa kusikia kamekuwa ka kwanza kumpongeza kwa ushindi baada ya tarehe 25 Oktoba!!
 
Wewe mpuuzi sana. Wewe ni nani kuwaamulia mamilioni ya watanzania? Kitu gani special umefanya hadi lile unaloamini ulipe mamlaka? Tulia chini, mimi nina kura moja, na wewe katumie kura yako moja kumpigia umtakaye (kama umejiandikisha).

Rais Dr magufuli.kanywe sumu
 
Nimezaliwa na kukulia hapa hapa Bongo TanZania hii imenipa uwezo mkubwa wa kuwaelewa Watz wenzangu kwa jinsi walivyo hasa tabia zetu!

Moja ya tabia kubwa ya MtanZania ni kwamba siku zote ni Muongo, Mtz wa kawaida ni lazima atakudanganya tu hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo, sijui ni kwa nini lkn tuko hivyo, wewe mpigie simu rafiki yako yoyote yule sasa hivi muulize uko wapi ni lazima atakudanganya, Mtz akinunua gari la Milioni tatu ukimuuliza lzm atakudaganya amenunua milioni 4, ukimwona na mwanamke ukimuuliza atakwambia yule nimetembea naye wakati ni Muongo!

Watanzania siku zote huongea kinyume hivyo kwa kuwa huyu aliyeandika hii mada ni Mtanzania basi naamini kabisa kwamba ni muongo na anachomaanisha ni kinyume chake kwa kifupi anamuombea fisadi Lowasa poo kwa maana mambo yameshakaba na fisadi Lowasa hana pa kutokea, fisadi Lowasa ameshatambua kwamba hawezi kushinda huu uchaguzi hata iweje na ndiyo maana wameshaanza kuongelea kuibiwa kura sasa tume imewabana kila mahali visingizio vyao vyote tume imevifanyia kazi na kuvirekebisha kuanzia sijui kalamu ya kupigia kura mpaka matokeo kubandikwa Kituoni yote yamerekebishwa kila wanaloomba tume inawapa na haya yote yapo kwenye rekord kama ni kushitakiwa Mahakama ya Kimataifa ICC (The Hague) video na audio za ushahidi zipo ambazo akina Tundu Lisu, Mbowe, fisadi Lowasa &Co. wakihamasisha fujo hivyo kwa kifupi wamebanwa, tafiti za Kimataifa za Twaweza zimeonyesha fisadi Lowasa hana chake mpaka leo hii kulingana na tafiti hata wafuasi wa fisadi Lowasa wala hawajui tofauti ya UKAWA na chadema achilia mbali fisadi Lowasa na na Mbowe kwanza wengine wanafikiri Slaa atakuwepo kwenye karatasi ya kura, muda umekwisha Magufuli ameshafika sehemu kubwa ya vijiji wakati fisadi Lowasa wala hajaaanza!

Hivyo namuelewa mleta mada ni kwamba anawatayarisha wafuasi wa fisadi Lowasa kisaikolojia kwani ni kweli Magufuli atamfunga fisadi Lowasa na hilo fisadi Lowasa analijua!

CCM ni Chama Dola na kuna Sababu kinaitwa hivyo!
Kwakuwa wewe mwenyewe umetuaminisha kuwa watanzania ni waongo basi na wewe uliyoyaongea humu ni uongo mtupu ccm ni dola na yawezekana ni uongo kwanini ipo na waeza kuta wanalazimisha tu kuiita hivyo... na inawezekana Lowassa sio Fisadi sababu umeongopa
 
Yaani Kati ya vitu vinavyonisikitisha kwa wabongo ni kuchukulia mambo kijuu juu, hivi Jeikei amwombe Msamaha wa nini? Kama aliyoyafanya ilikuwa ni kwa maslahi ya taifa na sio kitu personal kuna haja ya kuomba msamaha? Hii nchi ni yetu sote, sasa mwandishi senior hivi anaandika Habari ya kuombana msamaha!!!! Tutafika kweli?
 
Ndani ya Jf mda mrefu niliutumia kuwasoma tuu. Hivyo kuna watu niliwaheshim sana kama Mkuu Pasco, Chief Mkwawa, Mzizi mkavu, Yeriko Nyerere na wengne wengi japo kila mtu na kitengo chake. Pia kuna mijitu niliipuuza ikiongozwa na bibi FF. Hongera sana Mkuu Pasco unatisha sana. Watu wengi sana kitaa wanafuatilia jf heshima ni mhimu sana kuliko buku 7 za Lumumba.
 
Heee Pasco, unafikri haka ka-Kwere katakuelewa kweli? Nina mashaka sana kama katakubaliana na ushauri wako, kenyewe katakwambia ni upepo tu utapita!!

Ila mimi nahisi haka kamjamaa huenda kametula kekundu kuvunga kwamba wamekorofishana kumbe wako wamoja, hivyo tusije tukashangaa kusikia kamekuwa ka kwanza kumpongeza kwa ushindi baada ya tarehe 25 Oktoba!!

that's true?
 
JK akampigie magoti tu Lowassa..mapemaaa...kiroho safi tu , Lowassa ndiye Rais ajaye.

Wanabodi,

Hili jambo ninalolizungumza hapa, ni jambo very serious na la kweli, sio jambo la masikhara, kwa sababu mimi binafsi ni shuhuda na mhanga wa jambo kama hili kuwa ni jambo la kweli kabisa ambalo lipo for real!.

Kwa kuwasaidia tuu watu wasijua facts kuhusu nafasi ya urais, rais ni mtumishi wetu, yaani ni mtumishi wa watu, sisi Watanzania ndio mabosi wake, sisi ndio tumemuajiri ili atutumikie, na ni sisi ndio tunao mlipa mshahara na marupurupu yake yote kwa fedha zetu na jasho letu, hivyo hatupaswi kumuogopa, bali tunapaswa kumuheshimu, na kiukweli tunamuheshimu sana!.

Pamoja na heshima yote kwa rais wetu, mamlaka yote, na madaraka yote, rais wetu na yeye pia ni binadamu, sio Mungu na wala sio malaika, hivyo yeye kama binadamu anaweza kukosea tuu kama binadamu wengine wote!, tofauti ni kuwa, kwa vile urais ndio nafasi ya juu kuliko nafasi zote za uongozi, rais anachukuliwa kuwa ndio yuko juu kuliko mtu mwingine yoyote, na wengine wote waliomzunguka, hujiona wako chini yake, hali inayopelekea hata akifanya makosa ya kibinaadamu, hakuna mtu wa kumwambia rais hapa ulikosea!.

Kwa vile mimi ni mmoja wa raia wake, ninajua kuna kosa fulani amelitenda kumhusu Edward Lowassa, hivyo kwa heshima na unyenyekevu wa hali ya juu sana, namshauri Rais wetu Mheshimiwa sana, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye kiukweli yuko juu, ajisheshe, aende kumuomba msamaha wa dhati Edward Lowassa kwa kosa alilomtendea, kabla ya October 25!.

Msamaha huo sio lazima uwe wa public, anaweza tuu kupanga vile ambavyo ataona inafaa, akutane na Lowassa na kumuomba msamaha kwa kosa hilo alilomtendea, wakasameheana, tarehe 25 October, Watanzania tukaingia kwenye uchaguzi kwa upendo na amani, ili hata ikitokea, Watanzania kwa ridhaa yetu wenyewe, tukiamua kuipumzisha CCM kwa kuiweka pembeni, tuipumzishe kwa upendo na amani,,, na sio kwa chuki na visasi!.

Jee Kosa lenyewe ni lipi linalompasa Rais Wetu Jakaya Kikwete kumuomba msamaha Edward Lowassa?!.
Hapa sasa ndipo heshima, akili, busara, unyenyekevu, ustaarabu, uungwana, ustahimilivu wa hali wa juu unapotakiwa kutumika, kama ilivyo katika familia zetu, Baba ndie Mkuu wa nyumba, hata akikosea, kuna namna ya kumjulisha kuwa hapa baba umekosea, tena anayemwambia hayo baba sio mtoto na sio mama bali ni wazee wenzie wa rika lake, hivyo kwa ruhusa ya mwana jf huyu, naomba kumleta mzee wa rika la JK,

Namalizia kwa kulitaja jambo lenyewe iwapo JK ataamua kuwa hakuna kosa lolote la kumuomba msamaha Edward Lowassa, then naomba kutoa ushuhuda wangu wa kitu kinachoitwa 'karma' kwa vile mimi karma naijua na iliishanikuta, hivyo baada ya October 25 mimi ndio nitakuwa muhabarishaji wa jf every time 'karma' takes its toll!.

Ushauri wa bure kwa wana jf ambao hamjui kuhusu 'karma', nawasihi jisomeeni tuu uzi huu na kujipitia zenu, msije kujitia kimbelembele kumjibia JK unless you are certain and absolute sure what was the name of the game!, and also you know what 'karma' is and its quosequenses.

Kuna watu watajiapiza hadi maneno kama 'over my dead body' hakuna msamaha wowote wa kuombwa kwa Lowassa, then subirieni baada ya October 25, nitawakumbusha kuhusu uzi huu!.

Kwa ajili tuu ya kukuwekea references niliwahi kusema nini na hatimaye nini kilitokea, nashauri, msibeze au kupuuzia ushauri wowote wa bure hata ukitoka kwa chizi, bali pima hoja za kwenye ushauri huo!.

Kwa wageni wasiomfahamu Pasco wa jf, wanaweza kufikiri hii ndio maea yake ya kwanza kushauri, au kulizungumzia jambo halafu likatokea. Naomba niwatembeze kido mitaa hii kwa wale wenye nafasi, muangalie nilisema nini na nini kikata kikatokea!.

  1. Wengi wanadhani mgombea wa CCM, JPM amejiibukia tuu from no where!, or just by chance!, no way, Magufuli hajaibuka for a chance, there are serious reasons, sisi wengine tulibahatika tukaelezwa hizo sababu na tukazileta humu jf tangu 15th August 2014 niliwaeleza watu hivi Mgombea wa CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!
  2. Wakati wa uchaguzi wa Arumeru nilimshauri kitu Lowassa, hakusikia na angalieni kilichotokea.
    Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
  3. Wakati wa harakati za kuutafuta urais, wengi wakitumai ni Lowassa atapitishwa, nilisema hivi na angalieni nini kilitokea!.
    Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

    Pia nimetoa shauri nyingine mbalimbali za bure.
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humou

Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim! -

Rais Wetu "Mchelea Mwana Kulia, Endelea Kuwachekea, Ny

Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report:

Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!,

Ushauri wa bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared

Ushauri wa Bure kwa CCM Zanzibar: Kumuepushia Aibu

Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli,

Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko

Ushauri wa Bure Kwa ZZK, "Shika Lako!" Ya Wengine

Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)

Pasco
 
Lowassa ni Rais tayari....!!!

JK ajiandae kukabidhi madaraka tu... kwani hata hakumbuki shukrani, bila Lowassa, JK asingekuwa RAIS...!!

Lowassa alijitoa kimasomaso, usiku na mchana kumsaidia JK.... JK kamgeuzia kibao, hataki hata kumsikia Lowassa, na Lowassa akaona isiwe SHIDA kamwacha JK na CCM yake, kamfanyia unyama sana huko CCM, wee acha tu... ila bado anapambana nae chini chini... yuko UKAWA, ila sasa ndio JK atamjua Lowassa ni the BEST Politician ever...!!!

Lowassa, ameumizwa sana sanaa...!!!

Sasa anakuwa Rais, hakika malipo ni hapa hapa Duniani...!!!

Mungu mwacheni aitwe Mungu...!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom