Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,

Hili jambo ninalolizungumza hapa, ni jambo very serious na la kweli, sio jambo la masikhara, kwa sababu mimi binafsi ni shuhuda na mhanga wa jambo kama hili kuwa ni jambo la kweli kabisa ambalo lipo for real!.

Kwa kuwasaidia tuu watu wasijua facts kuhusu nafasi ya urais, rais ni mtumishi wetu, yaani ni mtumishi wa watu, sisi Watanzania ndio mabosi wake, sisi ndio tumemuajiri ili atutumikie, na ni sisi ndio tunao mlipa mshahara na marupurupu yake yote kwa fedha zetu na jasho letu, hivyo hatupaswi kumuogopa, bali tunapaswa kumuheshimu, na kiukweli tunamuheshimu sana!.

Pamoja na heshima yote kwa rais wetu, mamlaka yote, na madaraka yote, rais wetu na yeye pia ni binadamu, sio Mungu na wala sio malaika, hivyo yeye kama binadamu anaweza kukosea tuu kama binadamu wengine wote!, tofauti ni kuwa, kwa vile urais ndio nafasi ya juu kuliko nafasi zote za uongozi, rais anachukuliwa kuwa ndio yuko juu kuliko mtu mwingine yoyote, na wengine wote waliomzunguka, hujiona wako chini yake, hali inayopelekea hata akifanya makosa ya kibinaadamu, hakuna mtu wa kumwambia rais hapa ulikosea!.

Kwa vile mimi ni mmoja wa raia wake, ninajua kuna kosa fulani limendeka kumhusu Edward Lowassa, wakati wa kipindi chake, hivyo kwa heshima na taadhima na kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana, namshauri Rais wetu Mheshimiwa sana, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye kiukweli yuko juu, ajinyenyekeshe, aende kumuomba msamaha wa dhati Edward Lowassa kwa kosa awamu yake ililomtendea, kabla ya October 25!.

Msamaha huo sio lazima uwe wa public, anaweza tuu kupanga vile ambavyo ataona inafaa, akutane na Lowassa na kumuomba msamaha kwa kosa hilo lililotendeka, wakasameheana, tarehe 25 October, Watanzania tukaingia kwenye uchaguzi kwa upendo na amani, ili hata ikitokea, Watanzania kwa ridhaa yetu wenyewe, tukiamua kuipumzisha CCM kwa kuiweka pembeni, tuipumzishe kwa upendo na amani, na sio kwa chuki na visasi!.

Jee Kosa lenyewe ni lipi linalompasa Rais Wetu Jakaya Kikwete kumuomba msamaha Edward Lowassa?!.
Hapa sasa ndipo heshima, akili, busara, unyenyekevu, ustaarabu, uungwana, ustahimilivu wa hali wa juu unapotakiwa kutumika, kama ilivyo katika familia zetu, Baba ndie Mkuu wa nyumba, hata akikosea, kuna namna ya kumjulisha kuwa hapa baba umekosea, tena anayemwambia hayo baba sio mtoto na sio mama bali ni wazee wenzie wa rika lake, hivyo kwa ruhusa ya mwana jf huyu, naomba kumleta mzee wa rika la JK,
Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995.

Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995.

Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kubwa na muono mpya.


Juma Volter Mwapachu

Source: Ibrahim Kibopile

Namalizia kwa kulitaja jambo lenyewe iwapo JK ataamua kuwa hakuna kosa lolote la kumuomba msamaha Edward Lowassa, then naomba kutoa ushuhuda wangu wa kitu kinachoitwa 'karma' kwa vile mimi karma naijua na iliishanikuta, hivyo baada ya October 25 mimi ndio nitakuwa muhabarishaji wa jf every time 'karma' takes its toll!.

Ushauri wa bure kwa wana jf ambao hamjui kuhusu 'karma', nawasihi jisomeeni tuu uzi huu na kujipitia zenu, msije kujitia kimbelembele kumjibia JK unless you are certain and absolute sure what was the name of the game!, and also you know what 'karma' is and its quosequenses.

Kuna watu watajiapiza hadi maneno kama 'over my dead body' hakuna msamaha wowote wa kuombwa kwa Lowassa, then subirieni baada ya October 25, nitawakumbusha kuhusu uzi huu!.

Kwa ajili tuu ya kukuwekea references niliwahi kusema nini na hatimaye nini kilitokea, nashauri, msibeze au kupuuzia ushauri wowote wa bure hata ukitoka kwa chizi, bali pima hoja za kwenye ushauri huo!.

Kwa wageni wasiomfahamu Pasco wa jf, wanaweza kufikiri hii ndio maea yake ya kwanza kushauri, au kulizungumzia jambo halafu likatokea. Naomba niwatembeze kido mitaa hii kwa wale wenye nafasi, muangalie nilisema nini na nini kikata kikatokea!.

  1. Wengi wanadhani mgombea wa CCM, JPM amejiibukia tuu from no where!, or just by chance!, no way, Magufuli hajaibuka for a chance, there are serious reasons, sisi wengine tulibahatika tukaelezwa hizo sababu na tukazileta humu jf tangu 15th August 2014 niliwaeleza watu hivi Mgombea wa CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!
  2. Wakati wa uchaguzi wa Arumeru nilimshauri kitu Lowassa, hakusikia na angalieni kilichotokea.
    Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
  3. Wakati wa harakati za kuutafuta urais, wengi wakitumai ni Lowassa atapitishwa, nilisema hivi na angalieni nini kilitokea!.
    [h=3]Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC! [/h]Pia nimetoa shauri nyingine mbalimbali za bure.
[h=3]CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga![/h]
Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humou

Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim! -

Rais Wetu "Mchelea Mwana Kulia, Endelea Kuwachekea, Ny

Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report:

Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!,

Ushauri wa bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared

Ushauri wa Bure kwa CCM Zanzibar: Kumuepushia Aibu

Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli,

Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko

Ushauri wa Bure Kwa ZZK, "Shika Lako!" Ya Wengine

Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)

Pasco
 
Mkuu pasco ushauri wako ni mzuri sana na muhimu kwa kutanguliza mama yetu tanzania, ila kama ulivyosema hapo juu kuna watu watakuja hapa jukwaani kukupinga na kukubeza bila uhakika wa nini wanakichangia
 
Angempitisha bado ingesemwa kamwachia rafiki yake!!
Lakini nchi hili sio ya Jk peke yake ni ya watanzania wote, Jk ana kura moja tu kwenye kuchagua rais

Tukiruhusu hili ya rais anayemaliza muda wake kutuchagulia mrithi wake itatuletea shida,ipo siku mwanae atarithi.
 
Hakika. Na zaidi ya yote,binafsi naamini hakuna kosa lisilostahili msamaha. Hata kama msameheaji hataki,lakini wewe uliyekosea karma haitakuwa juu yako tena.
Hivyo ingelikuwa heri kwake to seek peace now,or never.
Kwa nyongeza tu,naona Jakaya Kikwete amekuwa mvivu kufikiri,ama kibri kimemjaa. Na katu kwa kibri hii hawezi kum-confront El Primier,Rais mtarajiwa (hutaki unaacha,ila ndo yatakayo tokea).
 
Maandiko yote ya Pasco always sio ya kubeza.... Nakumbuka sana andiko lake kabla ya Dodoma, na kweli yalitokea.... Tafadhali sana kwa wale walio karibu na Jakaya kama kweli mnampenda mwambieni akaombe msamaha asije akapata machungu baada ya oktoba 25
 
Nimezaliwa na kukulia hapa hapa Bongo TanZania hii imenipa uwezo mkubwa wa kuwaelewa Watz wenzangu kwa jinsi walivyo hasa tabia zetu!

Moja ya tabia kubwa ya MtanZania ni kwamba siku zote ni Muongo, Mtz wa kawaida ni lazima atakudanganya tu hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo, sijui ni kwa nini lkn tuko hivyo, wewe mpigie simu rafiki yako yoyote yule sasa hivi muulize uko wapi ni lazima atakudanganya, Mtz akinunua gari la Milioni tatu ukimuuliza lzm atakudaganya amenunua milioni 4, ukimwona na mwanamke ukimuuliza atakwambia yule nimetembea naye wakati ni Muongo!

Watanzania siku zote huongea kinyume hivyo kwa kuwa huyu aliyeandika hii mada ni Mtanzania basi naamini kabisa kwamba ni muongo na anachomaanisha ni kinyume chake kwa kifupi anamuombea fisadi Lowasa poo kwa maana mambo yameshakaba na fisadi Lowasa hana pa kutokea, fisadi Lowasa ameshatambua kwamba hawezi kushinda huu uchaguzi hata iweje na ndiyo maana wameshaanza kuongelea kuibiwa kura sasa tume imewabana kila mahali visingizio vyao vyote tume imevifanyia kazi na kuvirekebisha kuanzia sijui kalamu ya kupigia kura mpaka matokeo kubandikwa Kituoni yote yamerekebishwa kila wanaloomba tume inawapa na haya yote yapo kwenye rekord kama ni kushitakiwa Mahakama ya Kimataifa ICC (The Hague) video na audio za ushahidi zipo ambazo akina Tundu Lisu, Mbowe, fisadi Lowasa &Co. wakihamasisha fujo hivyo kwa kifupi wamebanwa, tafiti za Kimataifa za Twaweza zimeonyesha fisadi Lowasa hana chake mpaka leo hii kulingana na tafiti hata wafuasi wa fisadi Lowasa wala hawajui tofauti ya UKAWA na chadema achilia mbali fisadi Lowasa na na Mbowe kwanza wengine wanafikiri Slaa atakuwepo kwenye karatasi ya kura, muda umekwisha Magufuli ameshafika sehemu kubwa ya vijiji wakati fisadi Lowasa wala hajaaanza!

Hivyo namuelewa mleta mada ni kwamba anawatayarisha wafuasi wa fisadi Lowasa kisaikolojia kwani ni kweli Magufuli atamfunga fisadi Lowasa na hilo fisadi Lowasa analijua!

CCM ni Chama Dola na kuna Sababu kinaitwa hivyo!
 
Pasco aka Msimila (Ilboru time), kwa upande wangu sioni uwezekano wa mzee wa Monduli kuingia Ikulu hata kama akishinda uchaguzi kwa kura nyingi kuliko CCM.

Kauli mbalimbali zimeshatamkwa kwamba "Wenye Serikali hawako tayari kukabidhi madaraka kwa wapinzani".
 
Ina shangaaza kuona raisi ulie muajiri ana pesa kukuliko, na ukileta ujinga anakufunga wewe huyo huyo ulie muajiri, kama haitoshi na yeye ana ajiri watu anao wataka bila ruhusa yako wewe, na mbona ana kwenda nje ya nchi sanaaa kuliko mwajiri wake... nani kaajiriwa hapa raisi au wewe mwananchi???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom