i pad3
JF-Expert Member
- Mar 16, 2012
- 1,518
- 378
haya ni maoni nimeyachomoa kwenye baadhi ya post za Mkandara huyu jamaa nakubali sana michango yake hanaga mambo ya kuremba na huu mchango nimeupenda ..samahani sana Mkandara kwa kuchukua bandiko lako na kulifanya thread ila ni ujumbe mzuri sana kwa ndugu zetu
Ikiwa madai ya Wazanzibar ni haya Je wamewahi kuyawakilisha kwa wabunge na rais wao? na yapi yalikuwa majibu ya Karume au Shein kulingana na madai yote haya.
Pili ni mwaka juzi tu 2010 mlipiga kura za kutaka utawala wa mseto na mkasema ndio njia bora zaidi kwa Wanzanzibari walioungana, sasa leo imekuwaje hata mseto huo hamuutaki tena ilihali viongozi wote ni Wazanzibar na mlichagua wenyewe?. Na maadam kuna mfumo wa kiuchumi huru kwa Wazanzibnar kuagiza mali zao kutoka nje sidhani kama kuna sheria inayomzuia Mzanzibar kuleta mchele au ngano kutoka nje maana hata huku bara ni wafanyabiashara ndio huingiza vyakula nchini sio swala la serikali unless kuna uhaba na uwezo mdogo.
Toka mwaka 2000 kabla hata ya uchaguzi wa pili wa awamu ya Mkapa niliowahi kuwaambia badala ya kuanzisha machafuko Zanzibar na Pemba kwa nini msiombe referundum ili wananchi wapewe fursa ya kuchagua kubaki ktk muungano au watoke na zoezi zima lisimamiwe na vyombo vya kimataifa bila kuwabagua Wazanzibara. Na pia mfahamishwe wazi mazuri na mabaya ya kujitenga pindi ikitokea kujitenga isijekuja tukalaumiana. Lakini Maalim Seif kwa majibu yake alisema yeye kisha ifanya kazi alotumwa, hakutumwa kuomba referundum, nikawageukia Wazanzibar wenyewe na kusema huyu zuga tu kama kweli ana nia ya madai yenu basi asingejibu kirahisi hivyo. Toka 2000 hadi leo ndio nasikia mnaanza kudai referendum tena baada ya nyie wenyewe kuchagua serikali ya mseto kama ndio UMOJA wa Wazanzibar. Tuwaelewe vipi?
Kumbuikweni tu mlioko bara mtachukuliwa ka wageni na sidhani kama biashara zetu zitaweza kwenda mbele kwa kuomba kibali cha ajira au ukazi kila mwaka na hasa ukizingatia corruption iliyopo serikalini. Kujitenga kwenu na madai haya yasokuwa na maana kabisa mtajimaliza wenyewe.