Ushauri wa bure kwa mwenye biashara yoyote anayetaka kuteka soko lake

Jun 8, 2016
83
645
Nikiwa kama mteja na at the same time nimepitia kazi za marketing nyingi, nashangaa sana kwa kuwa sijakutana na wafanyabiashara wanaotumia hii njia ili kupata wateja, especially kwenye karne hii. Ili kuielewa vizuri ngoja tuchukue scenario mbili tofauti zifuatazo:

1) Hii hapa ni scenario ya kwanza ambayo ndiyo ipo kwenye asilimia 99 ya masoko yote Tanzania
Tuseme mimi nimejipanga vizuri nikapata milioni zangu kumi hivi, alafu nataka kununua gari. Sina uhakika ninunue gari gani kwa budget yangu, ni nunue showroom au second hand au niagize. Sina uhakika nichukue toyota au suzuki, hata labda nikichagua brand ya toyota kwa kua kuna spare nyingi labda , sina uhakika nichague toyota gani ambayo itanifaa, factors zipo nyingi sana.

Tuseme nikaamua nifanye research kwenye mtandao (online) sasa nione bei za magari na ni lipi linaweza kunifaa, niingie na website ya baadhi ya showrooms na nione list ya magari nichague budget yangu ilipo, bado selection zipo nyingi sanaaa. Kwa kuwa kwenye website zao wameandika bei tu na picha za magari, siwezi kujua kati ya toyota vits / ist / allex / allion / altezza na mengine yote, ni lipi ambalo nichukue? inabaki kuwa complicated mwisho wa siku naamua tu kwa kua mtu flani na yeye analo, au nimeshauriwa na rafiki, au preference yangu tu ya muonekano wa hilo gari lakini kuna factors nyingi sana za kuchagua gari ambazo ningepewa ningefanya maamuzi sahihi.

Hivi ndivyo ambavyo ningekutana navyo kwenye search yangu

1.jpg
2.jpg
3.jpg


2) Hii ni scenario ya pili : ambayo ndio ikitumiwa itamfanya mwenye biashara ateke soko
Rewind<<<<<<<< okay, nimejipanga kama mwaka mzima hivi, nimesave milioni kumi na nataka kununua gari. naingia facebook nakutana na page inaitwa “magari pro’s tanzania” wameandika post inaitwa “magari kumi unayoweza kununua ukiwa na milioni 7 au chini ya hapo” naingia kwenye page yao, naona ni link, nabonyeza link inanipeleka kwenye website yake ambayo imeelezea vizuri magari 10 kama nina milioni saba, but mimi nina kumi i can do better than that, naangalia kwenye sidebar kwa pembeni naona kuna post ya “magari kumi yatayokufaa kama una budget ya milioni kumi” na click hapo naisoma vizuri kisha nachagua kama magari matatu hivi.

Ila bado, gari ninalo taka mimi ni ambalo litaweza stahimili safari zangi za dar-dodoma, dar – tanga na kurudi, bila kusumbua barabarani, na search kwenye hiyo website ya “magari pro’s” then naona ipo post inayo elezea “magari 15 imara ya budget kwa ajili ya safari za kilo meter nyingi” , naingia humo then kati ya magari yote haya 15 naona gari ambayo niliyachagua mwanzo moja wapo lipo. and just like that nimepata gari linalo nifaa bila kuhangaika sana.

naangali chini ya hilo gari kuna link imeandikwa “inquire about this car” au “nunua hili gari” nabonyeza nawasiliana na muuzaji then kesho yake naenda kuchukua gari langu.

Mimi sina mtaji wa kufungua showroom kwa sahivi au kuagiza magari mengi, lakini nikija kuingia kwenye hili soko siku kama kuna mtu hajatumia hii njia nita teka soko zima, so just a heads up.

Mfano mzuri sana wa hichi ninachoongelea
nime search sana website za tanzania nione ni biashara gani inafanya hivi ila nimekosa, kama zipo tafadhali nijulishe niwapongeze, ila we need more of these kinds of business zitazotujilisha kwanini tuchague bidhaa wanazotaka kutuuzia na siyo kutu listia tu na kuandika bei sisi ndo tufanye maamuzi kila siku.

Nikaingia kwenye tovuti za mbele na kukutana na hii website inaitwa autoblog

autoblog wana uza magari na wanaandika post kama hizi kila siku za kusaidia watu wanunue gari gani, tuitembelee post hii hapa

5.jpg




Ni the same thing ninachoongelea, ni list ya magari ambayo yapo chini ya dollar za kimarekani 5000, au milioni 12 flani hivi za kitanzania. na ukicheki kwenye list yao kila gari wanalolitaja lina link ya kwenda kuinunua au kuiulizia hilo gari

6.jpg




SOKO GANI LINAWEZA KUTUMIA HII NJIA?
Soko lolote, kuanzia vipodozi hadi simu za mkononi, brand za nywele za kike, furniture, mabegi ya mgongoni, viatu, nguo na soko lolote ambalo mtu inabidi achague ndio aweze kununua hii ndio marketing tip kubwa kuliko zote ku quadruple (mara nne) your customers ndani ya muda mfupi.

Naona brand nyingi sana zina page za facebook na zinakua number kwa kasi sana lakini wanashindwa kutafuta mtu wa kuwaandikia post kama hizi ambazo ni muhimu sana kwa biashara, hii inaonesha kuwa sio tu unauza na kutaka watu wanunue kwaki ili upige hela tu, inaonesha unajua unachokiuza vizuri na wateja wana pata confidence ya kuja kununua hiyo bidhaa kwako na si kwa mshindani wako.

KIPI UNACHOHITAJI ILI KUTEKA SOKO LAKO?
  1. facebook page / instagram page / twitter page na kote kwingine ambapo unaweza ingia
  2. Website ya kuandika post zako na kupost bidhaa zako
  3. Mtu muelewa wa undani wa bidhaa unayouza, siyo lazima iwe wewe,vijana wapo wengi sana
Basi, hivyo ndiyo vitu vitatu unavyohitaji

Isome post kamili na mengine hapa
 
Good idea,ila siyo kwa bidhaa zote

bidhaa yoyote ambayo mtu inabidi achague inaweza kutumia hii njia.. siyo hata lazima post za top 10, hata kuelezea faida ya hiyo bidhaa kwenye post. nipe mifano ya bidhaa ambayo haiwezi tumia hii njia, mi kila nkifikiria sioni.
 
bidhaa yoyote ambayo mtu inabidi achague inaweza kutumia hii njia.. siyo hata lazima post za top 10, hata kuelezea faida ya hiyo bidhaa kwenye post. nipe mifano ya bidhaa ambayo haiwezi tumia hii njia, mi kila nkifikiria sioni.
Mchele,unga nk
 
Mchele,unga nk

It works pia. kuna michele kama aina 7 nikienda kununua mchele, i don knw which one is the best ila nachagua wenye bei kubwa kwa sababu ya bias zangu tu, ila sijawahi ijaribu mingine. Ukija na wewe na mchele wako uka uprice 2200 kwa kilo, ila mi nimezoea kununua 2400 ntaona na wako ileile tu. Ila nikikutana na sehemu umeniandikia faida za mchele wako na unapotoka, labda hali ya hewa huko na mengine, utanipa sababu ya mimi kuchagua mchele wako. point is hatuna as much information kwenye kuchagua bidhaa tunazonunua.
 
Upo vizuri mkuu umenifungua japo kuna hii thread yako hii ulifungua mda mrefu ina mapungufu kidogo mtandao kama alibaba hauwezi ukaanza na mtaji wa laki moja
Msaada: Hizi shipping cost za Alibaba bado sizielewi
nilitaka kuagiza pipi box moja sikufanikiwa ndio nikapata habari kutoka kwa wadau humu natakiwa niwe na mtaji kwanzia dollar 2000 pia kuna changamoto nyingi sana kwenye mitandao mingine kwenye shipping

Step 10: Nilivyowekeza laki moja hadi kuanza kutengeneza milioni moja kila siku 3 (step by step)
 
Upo vizuri mkuu umenifungua japo kuna hii thread yako hii ulifungua mda mrefu ina mapungufu kidogo mtandao kama alibaba hauwezi ukaanza na mtaji wa laki moja
Msaada: Hizi shipping cost za Alibaba bado sizielewi
nilitaka kuagiza pipi box moja sikufanikiwa ndio nikapata habari kutoka kwa wadau humu natakiwa niwe na mtaji kwanzia dollar 2000 pia kuna changamoto nyingi sana kwenye mitandao mingine kwenye shipping

Step 10: Nilivyowekeza laki moja hadi kuanza kutengeneza milioni moja kila siku 3 (step by step)
Tumia aliexpress.. Ni haohao for smaller quantities.
 
Tumia aliexpress.. Ni haohao for smaller quantities.
Kwa bidhaa zangu nazo taka kununua zipo alibaba tu ni hizo toy candy kuna seller tulizungumza nae akaniambia anatuma box moja au tatu ni kama sample zinafika kwa siku 10 hadi 15 sasa ndio nataka nizungumze nae tena kama kuna uwezekano tukawa tunafanya biashara kwa bidhaa chache hivyo hivyo japo bei yake ukijumlisha na shipping nisawa na huku isipokuwa bidhaa zinakuwa bado hazijafika bongo
 
Back
Top Bottom