Ushauri wa bure kwa mwenye biashara yoyote anayetaka kuteka soko lake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa mwenye biashara yoyote anayetaka kuteka soko lake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Michael Mkwanzania, Jan 30, 2017.

 1. Michael Mkwanzania

  Michael Mkwanzania Member

  #1
  Jan 30, 2017
  Joined: Jun 8, 2016
  Messages: 76
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 60
  Nikiwa kama mteja na at the same time nimepitia kazi za marketing nyingi, nashangaa sana kwa kuwa sijakutana na wafanyabiashara wanaotumia hii njia ili kupata wateja, especially kwenye karne hii. Ili kuielewa vizuri ngoja tuchukue scenario mbili tofauti zifuatazo:

  1) Hii hapa ni scenario ya kwanza ambayo ndiyo ipo kwenye asilimia 99 ya masoko yote Tanzania
  Tuseme mimi nimejipanga vizuri nikapata milioni zangu kumi hivi, alafu nataka kununua gari. Sina uhakika ninunue gari gani kwa budget yangu, ni nunue showroom au second hand au niagize. Sina uhakika nichukue toyota au suzuki, hata labda nikichagua brand ya toyota kwa kua kuna spare nyingi labda , sina uhakika nichague toyota gani ambayo itanifaa, factors zipo nyingi sana.

  Tuseme nikaamua nifanye research kwenye mtandao (online) sasa nione bei za magari na ni lipi linaweza kunifaa, niingie na website ya baadhi ya showrooms na nione list ya magari nichague budget yangu ilipo, bado selection zipo nyingi sanaaa. Kwa kuwa kwenye website zao wameandika bei tu na picha za magari, siwezi kujua kati ya toyota vits / ist / allex / allion / altezza na mengine yote, ni lipi ambalo nichukue? inabaki kuwa complicated mwisho wa siku naamua tu kwa kua mtu flani na yeye analo, au nimeshauriwa na rafiki, au preference yangu tu ya muonekano wa hilo gari lakini kuna factors nyingi sana za kuchagua gari ambazo ningepewa ningefanya maamuzi sahihi.

  Hivi ndivyo ambavyo ningekutana navyo kwenye search yangu

  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  2) Hii ni scenario ya pili : ambayo ndio ikitumiwa itamfanya mwenye biashara ateke soko
  Rewind<<<<<<<< okay, nimejipanga kama mwaka mzima hivi, nimesave milioni kumi na nataka kununua gari. naingia facebook nakutana na page inaitwa “magari pro’s tanzania” wameandika post inaitwa “magari kumi unayoweza kununua ukiwa na milioni 7 au chini ya hapo” naingia kwenye page yao, naona ni link, nabonyeza link inanipeleka kwenye website yake ambayo imeelezea vizuri magari 10 kama nina milioni saba, but mimi nina kumi i can do better than that, naangalia kwenye sidebar kwa pembeni naona kuna post ya “magari kumi yatayokufaa kama una budget ya milioni kumi” na click hapo naisoma vizuri kisha nachagua kama magari matatu hivi.

  Ila bado, gari ninalo taka mimi ni ambalo litaweza stahimili safari zangi za dar-dodoma, dar – tanga na kurudi, bila kusumbua barabarani, na search kwenye hiyo website ya “magari pro’s” then naona ipo post inayo elezea “magari 15 imara ya budget kwa ajili ya safari za kilo meter nyingi” , naingia humo then kati ya magari yote haya 15 naona gari ambayo niliyachagua mwanzo moja wapo lipo. and just like that nimepata gari linalo nifaa bila kuhangaika sana.

  naangali chini ya hilo gari kuna link imeandikwa “inquire about this car” au “nunua hili gari” nabonyeza nawasiliana na muuzaji then kesho yake naenda kuchukua gari langu.

  Mimi sina mtaji wa kufungua showroom kwa sahivi au kuagiza magari mengi, lakini nikija kuingia kwenye hili soko siku kama kuna mtu hajatumia hii njia nita teka soko zima, so just a heads up.

  Mfano mzuri sana wa hichi ninachoongelea
  nime search sana website za tanzania nione ni biashara gani inafanya hivi ila nimekosa, kama zipo tafadhali nijulishe niwapongeze, ila we need more of these kinds of business zitazotujilisha kwanini tuchague bidhaa wanazotaka kutuuzia na siyo kutu listia tu na kuandika bei sisi ndo tufanye maamuzi kila siku.

  Nikaingia kwenye tovuti za mbele na kukutana na hii website inaitwa autoblog

  autoblog wana uza magari na wanaandika post kama hizi kila siku za kusaidia watu wanunue gari gani, tuitembelee post hii hapa

  [​IMG]  Ni the same thing ninachoongelea, ni list ya magari ambayo yapo chini ya dollar za kimarekani 5000, au milioni 12 flani hivi za kitanzania. na ukicheki kwenye list yao kila gari wanalolitaja lina link ya kwenda kuinunua au kuiulizia hilo gari

  [​IMG]  SOKO GANI LINAWEZA KUTUMIA HII NJIA?
  Soko lolote, kuanzia vipodozi hadi simu za mkononi, brand za nywele za kike, furniture, mabegi ya mgongoni, viatu, nguo na soko lolote ambalo mtu inabidi achague ndio aweze kununua hii ndio marketing tip kubwa kuliko zote ku quadruple (mara nne) your customers ndani ya muda mfupi.

  Naona brand nyingi sana zina page za facebook na zinakua number kwa kasi sana lakini wanashindwa kutafuta mtu wa kuwaandikia post kama hizi ambazo ni muhimu sana kwa biashara, hii inaonesha kuwa sio tu unauza na kutaka watu wanunue kwaki ili upige hela tu, inaonesha unajua unachokiuza vizuri na wateja wana pata confidence ya kuja kununua hiyo bidhaa kwako na si kwa mshindani wako.

  KIPI UNACHOHITAJI ILI KUTEKA SOKO LAKO?
  1. facebook page / instagram page / twitter page na kote kwingine ambapo unaweza ingia
  2. Website ya kuandika post zako na kupost bidhaa zako
  3. Mtu muelewa wa undani wa bidhaa unayouza, siyo lazima iwe wewe,vijana wapo wengi sana
  Basi, hivyo ndiyo vitu vitatu unavyohitaji

  Isome post kamili na mengine hapa
   
 2. chief1

  chief1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2017
  Joined: May 4, 2015
  Messages: 1,197
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  Good idea,ila siyo kwa bidhaa zote
   
 3. STUNTER

  STUNTER JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2017
  Joined: Dec 15, 2015
  Messages: 13,019
  Likes Received: 14,743
  Trophy Points: 280
  Mkuu, nataka nikuajiri kwenye masuala fulani, upo tayari?
   
 4. The only

  The only JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2017
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 2,123
  Likes Received: 1,598
  Trophy Points: 280
  UNATAKA UMUAJIRI MKUU WAKO
   
 5. STUNTER

  STUNTER JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2017
  Joined: Dec 15, 2015
  Messages: 13,019
  Likes Received: 14,743
  Trophy Points: 280
  Hahahah kwani haiwezekani? Huenda malipo tukapiga pasu kwa pasu ikawa kama partnership
   
 6. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2017
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,870
  Likes Received: 2,717
  Trophy Points: 280
  Upo Sawa
   
 7. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2017
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 7,188
  Likes Received: 3,699
  Trophy Points: 280
  Kweli
   
 8. Michael Mkwanzania

  Michael Mkwanzania Member

  #8
  Feb 1, 2017
  Joined: Jun 8, 2016
  Messages: 76
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 60
  Partnership sawa mkuu.. ila ajira nina miaka kadhaa tangu ni "grow out of it", Ni PM maelezo.
   
 9. Michael Mkwanzania

  Michael Mkwanzania Member

  #9
  Feb 1, 2017
  Joined: Jun 8, 2016
  Messages: 76
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 60
  bidhaa yoyote ambayo mtu inabidi achague inaweza kutumia hii njia.. siyo hata lazima post za top 10, hata kuelezea faida ya hiyo bidhaa kwenye post. nipe mifano ya bidhaa ambayo haiwezi tumia hii njia, mi kila nkifikiria sioni.
   
 10. chief1

  chief1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2017
  Joined: May 4, 2015
  Messages: 1,197
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  Mchele,unga nk
   
 11. PATIGOO

  PATIGOO JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2017
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 10,633
  Likes Received: 8,922
  Trophy Points: 280
  Interesting
   
 12. Michael Mkwanzania

  Michael Mkwanzania Member

  #12
  Feb 6, 2017
  Joined: Jun 8, 2016
  Messages: 76
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 60
  It works pia. kuna michele kama aina 7 nikienda kununua mchele, i don knw which one is the best ila nachagua wenye bei kubwa kwa sababu ya bias zangu tu, ila sijawahi ijaribu mingine. Ukija na wewe na mchele wako uka uprice 2200 kwa kilo, ila mi nimezoea kununua 2400 ntaona na wako ileile tu. Ila nikikutana na sehemu umeniandikia faida za mchele wako na unapotoka, labda hali ya hewa huko na mengine, utanipa sababu ya mimi kuchagua mchele wako. point is hatuna as much information kwenye kuchagua bidhaa tunazonunua.
   
 13. Green_Touches

  Green_Touches Member

  #13
  Feb 7, 2017
  Joined: Dec 25, 2016
  Messages: 73
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  Hapo Inakua partnership sio kumwajiri tena.
   
 14. Green_Touches

  Green_Touches Member

  #14
  Feb 7, 2017
  Joined: Dec 25, 2016
  Messages: 73
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  It works almost kwa bidhaa zote.
   
 15. STUNTER

  STUNTER JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2017
  Joined: Dec 15, 2015
  Messages: 13,019
  Likes Received: 14,743
  Trophy Points: 280
  Mtaji ni wangu, Idea ni yangu, ofisi ni yangu, mshahara namlipa... Alafu unasema sijamuajiri?
   
 16. hearly

  hearly JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2018
  Joined: Jun 19, 2014
  Messages: 13,064
  Likes Received: 17,309
  Trophy Points: 280
  asante kwa hili darasa """
   
 17. kichakaa man

  kichakaa man JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2018
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 2,475
  Likes Received: 1,889
  Trophy Points: 280
  OK asante ipo vizur
   
 18. M

  Mapensho star JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2018
  Joined: Jun 30, 2016
  Messages: 1,613
  Likes Received: 1,199
  Trophy Points: 280
  Upo vizuri mkuu umenifungua japo kuna hii thread yako hii ulifungua mda mrefu ina mapungufu kidogo mtandao kama alibaba hauwezi ukaanza na mtaji wa laki moja
  Msaada: Hizi shipping cost za Alibaba bado sizielewi
  nilitaka kuagiza pipi box moja sikufanikiwa ndio nikapata habari kutoka kwa wadau humu natakiwa niwe na mtaji kwanzia dollar 2000 pia kuna changamoto nyingi sana kwenye mitandao mingine kwenye shipping

  Step 10: Nilivyowekeza laki moja hadi kuanza kutengeneza milioni moja kila siku 3 (step by step)
   
 19. Michael Mkwanzania

  Michael Mkwanzania Member

  #19
  Mar 28, 2018
  Joined: Jun 8, 2016
  Messages: 76
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 60
  Tumia aliexpress.. Ni haohao for smaller quantities.
   
 20. M

  Mapensho star JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2018
  Joined: Jun 30, 2016
  Messages: 1,613
  Likes Received: 1,199
  Trophy Points: 280
  Kwa bidhaa zangu nazo taka kununua zipo alibaba tu ni hizo toy candy kuna seller tulizungumza nae akaniambia anatuma box moja au tatu ni kama sample zinafika kwa siku 10 hadi 15 sasa ndio nataka nizungumze nae tena kama kuna uwezekano tukawa tunafanya biashara kwa bidhaa chache hivyo hivyo japo bei yake ukijumlisha na shipping nisawa na huku isipokuwa bidhaa zinakuwa bado hazijafika bongo
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...