Ushauri wa bure kwa mitandao ya simu

Mlayjr

JF-Expert Member
May 7, 2013
431
176
Nimetafakari kwa kina juu ya zoezi zima la kusajili laini za mitandao ya simu na kurejesha laini zilizopotea nakaona kuna mianya ambayo isipozibwa italeta matatizo makubwa sana huko mbeleni.

Ili uweze kusajili laini inakubidi uwe na namba ya kitambulisho cha taifa, iwe ni mteja mpya au unarejesha laini iliyopotea, namba ya kitambulisho cha taifa ndio kigezo kikubwa pekee kitakachokupa uhalali wa kupata laini ya simu.

Wasiwasi wangu ni kwamba sehemu ambazo tunaenda kupata loss report za polisi mara nyingi ni kwenye migahawa ya intaneti au kwenye vibanda visivyo rasmi, ukishapatiwa taarifa ya upotevu wa mali, soft copy wanabaki nayo kwenye compyuta zao. Je ile namba yako ya kitambulisho cha taifa haiwezi kusajilia namba nyingine bila mhusika kujua?

Na namba ile ikitumika kufanya uhalifu si mwenye namba atahusika moja kwa moja?

Ushauri wangu, jeshi la polisi nchini ambalo linafanya kazi yake kwa ueledi wa hali ya juu wakishirikiana na makampuni ya mitandao ya simu waanzishe vituo maalum vya kupata taarifa ya kupotelewa mali pamoja na kusajili laini za mitandao ya simu
la sivyo hizi meseji za "ile hela tuma kwenye namba hii" haziwezi kuisha na watu wengi wataingia matatani kwa makosa wasiyoyafanya wao.

Pia ndio muda wa kila mtu na simu yake, mambo ya naomba niazime simu yako kama ina hela nipige ndio yanafikia ukomo.

Mlay Jr
Kirua Vunjo
Moshi
 
Back
Top Bottom