Ushauri wa bure kwa Mbunge Musukuma(CCM)

Ndo tatizo la CCM kutowapa kitchen Party watu wa aina ya Msukuma (Mb) Kwamba kuna utengano mkubwa kati ya chama na dola na kwamba hata agekuwa Mwenyekiti mwandamizi wa walioshindikana katika mkoa ila anapaswa kuheshimu mamlaka ya kisheria kwa mujibu wa taratibu zilizopo...
 
Nyerere alituambia binadamu wote ni sawa hivyo si kubagua watu ktk kutoa ushauri maana kijana Petro pamoja na kupewa mkopo kama kasomo wakati wa mikopo bado walipa kodi walichangia ilimu yake yaani pamoja na Msukuma
Nani kakuambia binadamu wote ni sawa?
Unaweza kuwa sawa na Magufuli wewe?
Achana na kauli za kisiasa hizo mkuu!!
 
Ingawa nipo safarini kuelekea Arusha katika Mkutano wa nusu mwaka wa TLS,nimewiwa kumshauri jambo Mbunge wa Geita Vijijini,Ndugu Joseph Kasheku 'Msukuma'. Ushauri wangu unafuatia kadhia iliyompata ya kukamatwa na kushtakiwa kwa kuhujumu miundombinu ya maji

Ndugu Msukuma amekuwa na juhudi za kumsema na 'kumtisha' Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita,kabla na baada ya kukamatwa kwake. Amekuwa akimzungumzia RPC wa Geita kana kwamba ni raia wa kawaida anayeweza kumsema kisiasa atakavyo. Pia,Msukuma,kwa uelewa wangu,analenga 'kumchongea' RPC wa Geita kwa wateule wake.

Nataka kumpa taarifa Msukuma,na kumshauri. Kwanza,polisi si raia. Polisi hawana chama. Polisi ni chombo cha dola;chombo cha Serikali na wananchi kwa ujumla. Polisi wanapaswa kuheshimiwa kwakuwa wanafanya kazi kubwa kwa ulinzi wetu na ulinzi wa mali zetu. Msukuma anapaswa kuwaheshimu polisi na kuwaweka mbali na mikwara yake ya kisiasa.

Serikali ni yetu sote. CCM si watanzania wote na hivyo Msukuma asitambie. Kwakuwa tayari jambo lake liko mahakamani,anapaswa kunyamaza kimya na kushughulika na jambo lake. Kumsema na kumtisha RPC hakutamsaidia. Anaowategemea wamsaidie kichama wako kimya kwakuwa wameona kuwa Msukuma hana hoja!

Chadema madai yao ni kwamba Jeshi la Polisi ni la CCM ndiyo maana wanaliita, sana sana humu, PoliCCM...uwaambie hilo kuhusu Polisi.

Pili chadema wanadai hawana imani na Serikali...unawashauri nini?
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada. Hivi ndugu yetu Lizaboni kapotelea wapi. Nauliza. Na mnisamehe kwa kutoka nje ya mada.
 
Endelea na safari hili mwachie msukuma
Hujui chochote kuhusu hii inchi na kipi kinachoendelea baina ya msukuma na arapisiii
 
Polisi ofcoz ni kitengo cha usalama cha lumumba......rpc ukimkagua lazima anayo kadi ya magamba
 
Na kama msukuma ni mtu safi kwa nn hajayaanika mabaya ya RPC huyo siku zote?hadi awekwe ndani ndio aseme?
 
Mimi sina ubaguzi wa kivyama uwe ccm uwe cdm uwe cuf uwe huna chama ukienda nje ya mstari utawajibika tuu,HAPA KAZI TUU.
 
Nani kakuambia binadamu wote ni sawa?
Unaweza kuwa sawa na Magufuli wewe?
Achana na kauli za kisiasa hizo mkuu!!
Mbele ya Mungu nadhani tupo sawa. Ukichukulia kisiasa hatupo sawa si na Magufuli tu hata na Mbowe na hata mgonjwa wetu Lissu hayuko sawa na mimi. Lakini mbele ya Mungu wote ni sawa
 
Tuacheni kwanza tuitafakari hali ya Lissu kama ilivyoripotiwa leo na mh.Mbowe,hayo mambo ya Msukuma mwache apambane nayo mwenyewe,nyoka si wamemfuga wenyewe,iweje walalamika kuwang'ata?
 
kudharauliwa kwa huyo RPC ni matokeo ya wao polisi kukubali kutumiwa kisiasa na ccm.
na bila shaka huyo RPC atakuwa amepewa maagizo kutoka ngazi
za juu.
Sawa la kudharauliwa kwa polisi lipo kwa vyama vyote vya siasa mkuu.
 
Ukitoka Arusha nenda Geita kamsaidie uwakilishi ama sivyo ataishia kule alikokua anawacheka kina Lema. JPM siyo kama wanamdhani. Mkutano mwema mtani
Musukuma anadhani tumesahau alivyoruka na chopa kwenda kumnadi EL, hakuwa kambi ya JPM huyu alikuwa mchana ccm usiku cdm. Hilo darasa la saba analojidharau nalo ndo linamfanya asione mbali. Eti RPC mtu mdogo hajui jeshi huyu.
 
Sababu kuu ya haya yote ni; bwana kashek alimfichia mhuri baba j wakati wa kutafuta wadhamin mkoa wa geita Sasa ngoja nae avune alichopanda
 
Back
Top Bottom