Ushauri wa bure kwa makampuni ya simu kuhusu wizi wa pesa kwa njia ya simu

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,449
9,372
Habari zenu

Kutokana na kushamili wizi wa pesa kwa kupitia huduma za kipesa kwa simu za mkononi, na kuwepo na malamiko mengi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama lakini bado wizi upo na unaendelea basi naomba nitoe ushauri wa bure kwa vyombo husika

Ushauri wangu hii huu kampuni za simu anzisheni utaratibu pindi utu atumiwapo pesa basi asiwe na uwezo wa kuitoa mpaka masaa matatu yapite hii itasaidia wale watu wanaoibiwa kutoa tarifa kwa huduma kwa wateja na kurudishiwa pesa yao endapo wamefanya muhamala ambao hawautambui au wamegundua wameibiwa.
 
Sasa kma upo hospital na mgonjwa hali mbaya inasubiriwa fedha je,tuanzie hapo sio kutoa ushauri tu
 
Mkuu, nadhani kikubwa ni kuongeza umakini tu kwenye mambo ya mobile money. Unaposema swala la kusubiri masaa kadhaa, nadhani unapaswa kutafakari upya hili wazo lako la hovyohovyo. Kwasasa Dunia inakwenda kwa kasi ya ajabu, na teknolojia inazidi kuongezeka kwa mbio nyingi hata Dunia inajitahidi kuokoa kila dakika isipotee, then wewe unakuja na wazo la kupoteza dakika hizi ambazo tunakimbizana nanozo.
Mkuu, naomba kusisitiza kwamba ebu pata walau kifungua kinywa then ukuje usome upya ulicho kiandika hapa... tehteehhh
 
Back
Top Bottom