Prince Naseem
Member
- Apr 2, 2012
- 15
- 107
baada ya kutoka safarini nikiwa mchovu sana, nilijikaza mpaka kufanikiwa kuhudhuria mazishi ya baba wa rafiki yangu ambaye ni luteni kanali mstaafu wa jwtz (upande wa jkt) yaliyofanyika katika makaburi ya chang'ombe maduka mawili jana 24-04 2016, ndipo likanijia wazo hili la "kwa nini wanajeshi wote wasizikwe kwenye kambi za jeshi zilizopo karibu" kama wanavyofanya marekani na nchi zingine zilizoendelea na kuachana na huu utaratibu wa zamani wa kutowapa heshima za kutosha wapiganaji wetu.
hizo kambi zenu zinapaswa kutengewa eneo maalumu la makaburi ya mashujaa (garden of the missing soldiers) wetu hawa ili iwe rahisi hata kufanikisha suala zima la usafi wa eneo husika na pia kubaki kama kumbukumbu kwa askari waliopo.
kama baadhi ya makanisa yanaweza kupumzisha watumishi na viongozi wao katika maeneo maalumu ya maziko, kwa nini hili jeshi letu tukufu lishindwe??? na siku hizi makaburi almost yote ya hapa mjini dar yamejaa hivyo watu wanayafukuwa na kuzikwa mtu mwingine mwenye dau la juu zaidi.
"tafakari, chukua hatua"