Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Wanabodi,

Politics is a game like any other games, that people plays, it has its rules and regulations, ukikiuka unaweka pembeni. Yaani mchezo wa siasa pia ni mchezo kama mchezo mwingine wowote, una sheria zake, taratibu na kanuni, ukikiuka, unapewa kadi nyekundu unawekwa pembeni.

Serikali ya Zanzibar, ni serikali ya mseto, inaendeshwa na vyama viwili, CCM na ACT, ila watu wa ACT ndani ya GNU wanapaswa kutekeleza sera za CCM.

Serikali ya GNU japo ni serikali ya mseto, lakini inaongozwa na Ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo ACT ndani ya GNU ama wanatakiwa kuhubiri ilani ya uchaguzi ya CCM, na sera za CCM ama wanyamaze kimya, halafu wale ACT wengine nje ya GNU ndio wanaweza kuendelea kupiga siasa za ilani ya ACT!.

Ndani ya Serikali, kuna kitu kinaitwa a collective responsibilities, ukiishakuwa ndani ya serikali, huwezi kusema jambo lolote ambalo ni kinyume cha sera na ilani inayotawala ukabaki salama.

Maalim Seif alipokuwa ndani ya GNU, alinyamaza, hivyo Masoud Othman Masoud ama naye anyamaze, ama atoke nje ndio akaendelee kuhubiri kuuvunja huu muungano wetu adhimu!

Mtu aliyemo ndani ya serikali, hawezi kuyasema maneno kama haya
Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.
Msikilize Othman Masoud hapa chini.

Kwa maoni yangu, huyu mtu anatakiwa awekwe pembeni, apate muda wa kutosha ajishughulishe na siasa, kwasababu ACT ndani ya GNU wanatakiwa kutekeleza Ilani na sera za CCM!

Ushauri kama huu kumhusu mtu huyu huyu niliwahi kuutoa kule nyuma na ukatekelezwa, Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Hili la kila uchao mtu huyu kuuchokoa muungano hakuanza leo, na hakuna ubaya wowote kuuzungumzia muungano kwa jambo lolote alimradi hilo linalozungumzwa ni liwe la ukweli kuna siku aliongopa kuhusu sovereignity Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Hata Mama Samia akiwa VP aliwahi kushauri watu waachwe wa vent kuhusu muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Kama watu waachwe huru kuujadili muungano ndiko huku kunakofanywa na huyu, na kunajumuisha kuwa huru kuujadili muungano negatively hara Kwa mtu uliye ndani ya GNU, then I doubt kama huku ni kuujadili muungano kwa nia ya kuuimarisha bali ni kuujadili muungano kwa nia ya kuuvunja.

Paskali
 
Maoni mbadala ndio yanaendeleza nchi, kumfuta kazi maana yake ni kujidumaza kiakili na matokeo yake ni kudumaza maendeleo ya nchi.

Chama kuwa kwenye serikali ya mseto sio kama mwanamke aliyechumbiwa na mwanaume, still hao walioko kwenye mseto wanatakiwa kuwa huru kimawazo, kujipendekeza kwa watawala ni ujinga.

Ninahisi huyo Othman anaweza kushughulikiwa na viongozi wa chama chake, kwasababu wenzie wote sasa ni walamba asali.

Wakati mwingine huwa najiuliza hivi mkiwa mnahubiri demokrasia huwa mnakuwa mmelewa au? kwasababu najua nyie ni madikteta, na wewe ni mfano mmojawapo wa madikteta tulionao, unapenda vya kukufurahisha machoni pako pekee.
 
Kaka Paskali, unataka maoni yako ya kumfukuza Bwana Othman yafanyiwe kazi...!! Lakini unataka maoni ya Othman yamfukuzishe kazi..!! Hutendi haki..

Hivi kwanini mtu akitoa maoni yanayokinzana na watawala anatakiwa afanyiwe jambo baya?

Mnataka taifa la NDIYO MZEE? Kwanini hoja zake zisijibiwe kwa hoja zenye nguvu zaidi?
 
Halafu akimfuta, na hao ACT wakajitenga na hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, huoni hivyo Visiwa vitarudi tena kwenye ule mkwamo wao wa kisiasa wa miaka nenda?

Mimi naona Serikali ya Tanganyika ingeheshimu maamuzi ya Wazanzibari. Kama wanataka kujitoa kwenye huu Muungano, watoke. Haya mambo ya kuwalazimisha kuwa sehemu ya Muungano, yamepitwa na wakati.
 
Maoni mbadala ndio yanaendeleza nchi, kumfuta kazi maana yake ni kujidumaza kiakili na matokeo yake ni kudumaza maendeleo ya nchi.

Chama kuwa kwenye serikali ya mseto sio kama mwanamke aliyechumbiwa na mwanaume, still hao walioko kwenye mseto wanatakiwa kuwa huru kimawazo, kujipendekeza kwa watawala ni ujinga.

Wakati mwingine huwa najiuliza hivi mkiwa mnahubiri demokrasia huwa mnakuwa mmelewa au? kwasababu najua nyie ni madikteta, na wewe ni mfano mmojawapo wa madikteta tulionao, unapenda vya kukufurahisha machoni pako pekee.
Huyu jama paschal kuna kipindi ananiangusha, kwanini hapendi mawazo mbadala, siasa sio wote lazima tufanane kifkira
 
Halafu akimfuta, na hao ACT wakajitenga na hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, huoni hivyo Visiwa vitarudi tena kwenye ule mkwamo wao wa kisiasa wa miaka nenda?

Mimi naona Serikali ya Tanganyika ingeheshimu maamuzi ya Wazanzibari. Kama wanataka kujitoa kwenye huu Muungano, watoke. Haya mambo ya kuwalazimisha kuwa sehemu ya Muungano, yamepitwa na wakati.
Sure mambo ya lulazimishana yashapitwa na wakati.

Kama wanataka kutoka waachwe waende.

Kwanza sioni faida ya hao watu
 
Back
Top Bottom