Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Salaam wanaJF!
Jambo nitakalolizungumzia si mara ya kwanza kwa jambo hili kusemwa humu JF na wadau mbalimbali. CHADEMA, kama chama kinachozidi kukua na kupata umaarufu hapa TZ, kinapaswa kianze kujiweka katika mazingira ya chama maarufu na kinachokubalika kweli.
Mazingira haya ninayoyasema yamejikita katika suala la ofisi za chama zenye hadhi ya CHADEMA ya sasa na ya badae (kama chama tawala). Kwa kweli ofisi za chama, tena hata za mkoa bado hazina hadhi ya CHADEMA. Mfano, ofisi ya chama pale mkoani Dodoma, ni aibu kwa chama. Si vyema CHADEMA kuwa na ofisi kama ile, kwanza ipo ndani ya kijichumba kimoja (kama frame za maduka kwenye stand za mabasi au za biashara); hakuna office stationary; hakuna hata secretary zaidi ya jamaa mmoja ambae ndie uwa anakaa pale. Pia ofisi za makao makuu nazo zimeshaongelewa sana na wadau; nazo hazina hadhi ya chama kwa sasa.
Hapa chama kinabidi kifanye jitihada kweli; hata kama ni kwa kuomba michango toka kwa wanachama, wapenzi na wakereketwa chama kifanye, ili 2015 chama kiwe angalau na ofisi nzuri katika miji mikubwa hapa TZ.
Hili suala chama kinapaswa hisilichukulie kana kwamba ni dogo; muonekano wa kiofisi nao una matter katika masuala ya kisiasa.
Hivyo mimi ninakishauri chama kifanye jitihada za haraka katika hili. Niko tayari kuchangia kwa ajili ya kufanikinisha zoezi hili.
NB: Pia uongozi wa chama naomba mjitahidi katika suala la mawasiliano na utoaji wa taarifa mbalimbali za chama; website ya chama imedorora sana. System administrators wajitahidi kuwa active and alive.
Natumaini viongozi wa chama watasikia ushauri wangu na kuuzingatia.