Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Nimekuwa nikifuatilia sana siasa za Chama kikuu cha upinzani na kuweza kuona mambo yafuatayo.
1. Inaonyesha viongozi wa chama hawana msukumo kisiasa na kidiplomasia kwa kuwa uamuzi wao mwingi unaelekezwa na watu wa kwenye forums hasa JF. Chukulia mfano swala la Zitto na wabunge walioandikiwa barua za kujieleza. Ukifuatilia maoni ya wanachama wa JF utaona kuwa Chama kimewaitikia maelekezo yao na kuonyesha hawakuwa na habari kama kuna wabunge 10 hawakuingia bungeni siku ile mpaka iliposemwa na HR.
2. Ni ukweli usiopingika kuwa Chadema haina wanasiasa bali wengi wao ni wana harakati wanaotoka kwenye asasi zisizo za kiserikali na ndio maana hawawezi kufikia maamuzi kupitia itifaki badala yake wanasikiliza kina JF wanasemaje. Mfano wa asasi zisizo za kiserikali ni kama TNGP ( Naomi Kaihula), Chama cha wanasheria wao simamia haki za wachimba madini, na viongozi wa mashirika ya dini mfano mbunge aliepingwa hivi juzi na monica mbega.
3. Chadema hawajakomaa kisiasa, hawachukui kukosolewa kama changamoto na kufanyia kazi mapungufu. Ila facts zinazoikosoa zitachukuliwa kwa jazba na wafuasi wake.
4. Chadema hakuna demokrasia, ukifuatilia viti maalum vya chama utaona kuna watu wamejenga mazoea wao lazima wapitishwe, hakuna utaratibu wa kidemokrasia wa kuteua wabunge wa viti maalum badala yake kuna mtu anaewachakugua kupata huo ubunge wa upendeleo ni Mwanaume (hapo bwana kama ikitokea yale mambo yetu mtu akayamind halafu ukakataa ujue huna chako).
Udhaifu wa nafsi ya binadamu unaeleweka na ushahidi upo jinsi mama Musori alivyowekewa zengwe. Hii ni kuwa hakukuwa na utaratibu wa kupigiana kura ila kulikuwa kunautaratibu wa kupeana.
5. Ni chama kinachoendesha maswala kwa jazba na kusahau kuwa uongozi ni busara, ikiwa kiongozi anakuwa na jazba mara nyingi anaweza kuleta machafuko especial kwenye kundi linaloona halitendewi haki na anaweza kutoa maamuzi yake kwa jazba bila kuangalia sheria inasemaje.
6. Viongozi na Wanachama wamejawa chuki na fitina, badala ya kukuza chama na demokrasia ikiwa pamoja na kuandika katiba itakayo toa demokrasia mapaka namna ya uchaguzi wa wabunge wa viti maalum. Wao wanajadili nani afukuzwe kwenye chama.
Chadema kwa kuwa Chama kwa kiasi kikubwa kinaendeshwa na sisi wanaJF ni matumaini yangu mtaichukua hii changamoto na kuifanyia kazi ili chama kiwe imara zaidi.
Kuna kila sababu ya Chadema kujitazama isije kikawa chama cha msimu watanzania wanawasoma miaka mitano si mingi msije mkaaibika.
Angalizo:
Kama una pont za kuchangia mada hii unakaribishwa ila kama unataka kutoa matusi badala ya hoja nadhani ni busara ukaacha kuchangia na kutafuta thread za mapenzi na mahusiano ukachangia.
Shukran.