Ushauri wa bure kwa CCM na UKAWA..

BIG RESULTS NOW

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
673
36
Ndugu wanabodi habari. Salamu ndio msingi wa maisha. Nipitilize kwenye mada moja kwa moja, ni kwamba kwa kuwa sasa hivi taifa letu lipo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya na kwakuwa mchakato huo unapaswa kuwa wa maridhiano ili kuhakikisha tunapata katiba iliyo bora kwa miaka mingi ijayo, ni wazi kwa sasa maridhiano hayapo tena hasa baada ya wajumbe kutokubaliana ama kuridhiana kwenye muundo wa serikali.

Kimsingi masuala mengine yote hayawezi kujadiliwa pasipo kwanza kujadili muundo wa serikali. Sasa kwakuwa wajumbe wameshindwa kufikia muafaka kwenye suala la muundo wa serikali, nashauri hili suala liletwe kwa wananchi kwanza ili tulipigie kura kuamua twende na muundo gani.

Baada ya hapo ikishajulikana ni muundo upi tunaoutaka sisi wananchi suala hili lirudishwe tena kwenye bunge maalum la katiba kwaajili ya kujadili vipengele vilivyobaki na kisha utaratibu wa kura za maoni ufuate.

Wapo watakaohoji gharama za mchakato wa upigaji kura kuchagua muundo wa serikali. Niwatoe hofu kwamba kupanga ni kuchagua, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu tunaweza kuongeza kipengele huru cha kuchagua muundo wa serikali mbali na uchaguzi wa viongozi wa mitaa. Yaani mwananchi mbali na kuchagua viongozi wa serikali ya mitaa atapiga kura maalum pia ya kuchagua muundo wa muungano. Matokeo ya uchaguzi yanapotangazwa tutakuwa tumewajua viongozi wetu wa mitaa pamoja na muundo wanaoutaka wananchi.

Kwa mantiki hiyo nashauri Bunge maalum la katiba liendelee kuahirishwa mpaka pale uchaguzi wa serikali za mitaa utakapoitishwa na kuongezwa kipengele cha muundo wa muungano....

Mungu ibariki Tanzania...!!!!
 
Asilimia 90 ya vitongoji na vijiji ni CCM inaongoza, unafikiri watachagua serikali ngapi?
 
uma unataka s3 kwa mujibu wa tuliye mtuma mzee mtukufu JOSEFU SINDE WARIOBA
Angalia vijana toka zanzibar wanakuja bara na ujumbe huu.
image.jpg image.jpg
 
Mkuu ukimaliza kuangalia post yangu namba nne tukutane au nitafute nikujuze tena.
 
Ni mawazo mazuri ya kujikwamua tulipokwama! Lakini hakuna mbunge wa ccm anayeweza kuunga mkono hoja hii kamwe! Kwa wabunge wa ccm, kwao ni maslahi ya chama kwanza, maslahi ya taifa baadae!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom