Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

Status
Not open for further replies.
mi naamini katika Mungu mmoja na Muhammad ni mtume pia Yesu ni mwokozi. Je mi ni mkristo au muislam? Nitaandikishwa dini ipi? Sipendi kanisa wala msikiti
 
Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.

Sasa ndio umeandika nini? anyway kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake! UTAFITI/ukusanyaji wa takwimu zozote si halali isipokuwa uwe umepewa kibali na serikali kupitia mamlaka husika. kama ulikua hujui.
 
Hata utafiti wa tasnifu uwe na kibali cha serikali...........Utafiti kwenye elimu ya theology uwe na kibali cha serikali.............Hebu uwe unauangalia ukweli kwa mantiki yake, ukiwa unaangalia hoja kwa jicho la ushabiki utakuwa binadamu roboti
 
Najua kuna wanaalam kwasabab zao wanaanzisha mafukuto kama haya. Hao wanajiona wananufaika kwasasa lakin wajue kua hili wanaloliandaa yeye haliwatoka hivihivi. Wataadhibika kabla hata hawajaingia kaburin na manufaa wanayodhan wana/watayapata kwa kujarib kuchochea chuki za kidin hawatoyaona ya maana. Ni kama ndoto lakin siku yako haiko mbali.
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?

Wewe hujisomi udini utawamaliza juz juz hapa mkadai wakristo wanavyuo na shule nyingi mkataka mjengewe hebu funguken wenzenu walijipanga na wanamikakati, amken bado hamjachelewa alaf kuita wenzio kafir alaf badae unakutana nao, unapanda nao daladala moja,, unaonyesha jins gan ulivyopungukiwa na maarifa wewe hebu fikiri b4 huja aandika,muone kwanza....
 
mi naamini katika Mungu mmoja na Muhammad ni mtume pia Yesu ni mwokozi. Je mi ni mkristo au muislam? Nitaandikishwa dini ipi? Sipendi kanisa wala msikiti
na ndio maana tunasema sensa ifanywe na wahusika ili kubaini waumini wao wa halisi na sio waumini jina tu.
 
Kwani ikijumuishwa na sensa ya Serikali na kuwa official wajulikane wagalatia wangapi na Waislaam wangapi na wasiokuwa huku wala kule wangapi, itakuwa nini?
 
Mimi nawashauri Waislamu mgomee hii sensa na wakati mipango ya maendeleo inapangwa na Serikali gomeeni na msishiriki kama huduma ya maji, umeme , miundombinu,elimu, afya nk. kwa kuwa mtakuwa mnawanyonya wenzenu walioshiriki kuhesabiwa hivyo waislamu wote mtakuwa wanyonyaji kwenye suala zima la maendeleo.

Kwani kuna ugumu gani kwenda mkapigwe shule na wakatoliki wanaojuana kwa kila hali na ni wengi lakini wanahesabiana si kwa miaka kumi tu bali kila mwaka bila kuomba msaada serikalini. Nendeni kwa Muadhama Kadinali Pengo ni mwenye upendo, uvumilivu na si mchoyo. Tatizo lenu hamtaki shule.
 
ndugu zng waislamu,hivi leo mkiambiwa nyinyi ni 75% ya watanzania wote,kitu gani kitabadilika?maamuzi obvious yanaongozwa kwa nguvu ya hoja na sio idadi?tafuteni sababu ya kwa nini hampo ktk nafasi nyingi za kimaamuzi km mnavyoamini nyie na sio kubase ktk hoja mufilisi na zisizo na mashiko km iyo mnayoing'ang'ania,mbona kila siku ni nyie tu ndio mnaonewa?watanzania lazima tujifunze kutafuta root causes na sio partial causes.
 
Taabu ya hawa wenzetu hata ukiwapa uongozi wa nchi,yaani Rais,makamu,waziri mkuu na mawaziri wote,makatibu wote,wakurugenzi wa idara wote,wakuu wa mikoa,wilaya wote,wakurugenzi wa mashirika ya umma wote na kadha wa kadha bado hawa jamaa zetu wataendelea kulalamika na kudai mfumo kristo unatawala,frankly is very hard to deal with these characters,they are funny and useless!
Well said! Mimi kitu ambacho siwaelewi hawa jamaa ni role ya wasomi wa kiislamu mchango wao uko wapi angalau wa kuwapa tu wenzao ufahamu mdogo tu juu ya complexity of religious issues.
 
Mimi nawashauri Waislamu mgomee hii sensa na wakati mipango ya maendeleo inapangwa na Serikali gomeeni na msishiriki kama huduma ya maji, umeme , miundombinu,elimu, afya nk. kwa kuwa mtakuwa mnawanyonya wenzenu walioshiriki kuhesabiwa hivyo waislamu wote mtakuwa wanyonyaji kwenye suala zima la maendeleo.

Kwani kuna ugumu gani kwenda mkapigwe shule na wakatoliki wanaojuana kwa kila hali na ni wengi lakini wanahesabiana si kwa miaka kumi tu bali kila mwaka bila kuomba msaada serikalini. Nendeni kwa Muadhama Kadinali Pengo ni mwenye upendo, uvumilivu na si mchoyo. Tatizo lenu hamtaki shule.
 
Well said! Mimi kitu ambacho siwaelewi hawa jamaa ni role ya wasomi wa kiislamu mchango wao uko wapi angalau wa kuwapa tu wenzao ufahamu mdogo tu juu ya complexity of religious issues.

ni elimu tu ndio itakayo wakomboa waislamu otherwise wanaelekea kuwa km luddite mvt(luddism) ambao hawakujua their real enemy,wanazuoni wakiislamu ni vyema wakaokoa jahazi.
 
Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.

Nionavyo mimi Wislam wako sensitive mno kwa karibu kila jambo wakidhani kuna mfumo wa siri wenye kiu ya kuua uislam. Hali hiyo ndio inayowapofua macho wasione hata kazi ya serikali, kwamba kwa kupitia mfumo wa sensa ndipo inapopata idadi ya raia wake kwa lengo la kupanga mipango ya maendeleo. Kunapopangwa mipango ya mendeleo sioni dini ya Mtanzania inamchango gani kwa maendeleo yake! Kwa mfano wislamu wakisusa kuhesabiwa watakuwa wamemkomoa nani?
 
[h=2]Wito wa toba[/h]12 “Lakini hata sasa,” nasema mimi Mwenyezi-Mungu, “Nirudieni kwa moyo wote, kwa kufunga, kulia na kuomboleza.
13 Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?
kwanza kikwete,bilal,kigoda,nape,zungu,zitto,makamba watakataa nao kuhesabiwa...? hakiamungu nasubiri sana nione kama nao wana akili ndogo... subiri muone alafu ndo muwateme....!
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?
Hizo asilimia zitasaidia nini? Mbona unazungumzia makundi mawili tu wakati kuna makabila km wasukuma ambao wengi wao hawaamini chochote kati ya hizo dini unazotaja hawalalamiki kubaguliwa? Halafu unaposema serikalini wamejaa wakristo unatufanya sisi vipofu au unazungumzia shughuli za kitalaamu km udaktari, injia nk unafikiri unaweza kuchukua mtu mtaani ukamfanya daktari bil kwenda shule? hebu toa mfano km kuna daktari kakosa kazi kwa sababu ya uislamu wake. Maana km ni ngazi za maamuzi jamaa yenu amejitahidi sana kuwaweka halafu hamridhiki mfn wakuu wa wilaya, mikoa, mabalozi nk mbona sisi tuko kimya pigeni shule acheni uzembe mtaishia kulalamika tu .
 
Kwanza nafikiri hoja hii haina umuhimu kwa sababu hoja hii sio ya waislam. Waislam kama wanataka kujua idadi yao wafanye sensa yao. Hii ni ya serikali ambayo dini sio kigezo. Tunataka kujuwa idadi ya watanzania sio wakristo, wapagani au waislam.
 
Waislam Hawaishi Kulalamika..LEO Rais wa Muungano ni MWISLAM..Makamu wa Rais ni MWISLAM..Kule Zanzibar Rais ni MWISLAM,Makamu wa Rais Nzanzibar ni MWISLAM..Halafu Mnalalamika eti Mfumo Kristo,hamupewi Nafasi..Hivi hizi nilizozitaja Si Ndiyo Nafasi TOP kuliko zote?..Mbona Wakristo Hawajalalamika kuwa Viongozi wa nchi ni waislam?..Halafu assume sensa ikachukuliwa pamoja na kipengele cha dini..Matokeo yakitoka Tofauti na Matarajio ya waislam(kwa mfano wakristo wakawa wako wengi kitakwimu),Kesho yake tu Waislam watakuwa barabarani Kupinga Matokeo na Kuandamana..JAMANI HEBU FANYENI SENSA YENU WENYEWE HAKUNA ANAYEWAKATAZA..Full Stop
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom