Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

Status
Not open for further replies.
Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.

why Govt? Hakuna msaada wa serikali ambao unatolewa kwa imani ya dini. Kama ni nguruwe hata wasabato hawali
 
Nasema tena kama serikali itawasikiliza na ikaweka kipengele cha dini .Nasis wasukuma lazima tutaungana tukatae mapka kiwekwe kipengele cha ukabila ili na sisi tujue tuko wasukuma wangapi. kwani wafikiri sis ndo hatupendi kujua wasukuma ni wangapi hapa bongo ?

Na hizo kazi zauongozi zigawie kuendana na idadi asilimia ya makabila kila kabila lenye watu wengi kue na viongozi wengi

ala usione kimya hata sisi twapenda jua tupo wangapi :A S crown-2:

na sisi Waha twataka jua kama tunaongoza kwa kukimbia mkoa wetu wa Kigoma na kama tumewazidi wachaga kwenye biashara ndogo ndogo! Full stop
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?

mwanzo upi unaosemea wewe eti waislamu walikuwa wengi? Unaijua Tanzania wewe? Vijiji vya ndani kabisa hakuna uislam ila kanisa katoliki lipo. Unafikiri Tanzania ni Dar, Pwani, Tanga
 
Ndugu yangu, sensa, wala idadi ya watu si suluhu ya matatizo ya waislamu. Wala sensa si mkombozi wa waislamu. Hata kama tungekuwa wengi ambao tunawazidi wakristo mara sita au kumi. Kama hatuna elimu na wasomi wa kutosha katika dini yetu bado tutalalamika.

Cha msingi ni kuamka sasa na kuanza kutafuta tatizo lilianzia wapi, chanzo kilikuwa nini mpaka tumeathirika kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na elimu dunia.

Nadhani historia iko wazi tangu zamani watoto wa kislamu hawakushiriki kwa karibu sana elimu dunia. Yatupasa tubadilike sasa, elimu ya ahera kwa dunia ya sasa haimsaidii sana mtu. Tuangalie namna ya kubadili mfumo wa elimu yetu waislamu. Hiyo itatusaidia kwenda sambamba na dunia ya sasa bila kulalamika,

nadhani wanazuoni wa kiislamu wanasoma hapa. Ukweli thabiti
 
Mwisho mtataka sensa hiyo ionyeshe wa Sunni wangapi na Shia wangapi.Hamtaishia hapo bali mpaka idadi ya wenye madevu na wangapi wananyoa au waislamu wanawake wangapi hawavai hijab.Amkeni ndugu!mjue wako wenzenu wengi wanakereka sana na madai yenu yasiyo msingi huku mkijifanya mnawakilisha uislamu.
 
Waislam wana haki kama Watanzania na wanalipa kodi ni haki yao kuhesabiwa na serikali hakuna tatizo.

Sensa ya ukweli ni watu wamrudie muumba na kumheshimu katika maisha yao kama ni waislamu au wakristo. hata mtu akihesabiwa kama mwenye dini fulani lakini moyoni mwake yuko mbali na Mungu itasaidia nini?
 
Hivi hoja yao ya tatizo la mfumo kristo/katoliki imeishia wapi? Maana kama suala ni mfumo, suala la kujua idadi halitasaidia!
 
Mhh nina wasiwasi na uwezo wako wa kuangalia mambo na kupata uhalisia wake. Tatizo la waislamu si kutaka kupewa, Urais, au ukuu wa wilaya kama unavyosema, tatizo ni mfumo gani unamuweka mtu fulani mahali gani. Je ni mfumo wa haki??? Hili ndilo tatizo. Angalia kilichotokea juzijuzi tu baraza la mtihani, na aina ya majibu tuliyopata baada ya waislam kulalamikia matokeo ya mtihani, na baadaye majibu yaliyofuatia!!! Hii ni katika somo moja tu, je nani anajua nini kinaendelea katika masomo mengine???. Sioni kwa nini Serikali ikatae kuweka kipengele cha kumtambua mtu dini yake??

islamic knowledge au bible knowledge haimsaidii mtu kuingia chuo kikuu! Wala kwenda form 5
 
Nyakageni. Hawa jamaa hawaijui Tanzania. Ukiondoa mkoa wa Tabora na maeneo ya mijini huku bara ni maeneo kama Ujiji,Mwanga,Kondoa na sehemu chache vijijini utawakuta Waislamu wengi. Hiyo mikoa ya pwani ukiondoa Tanga na Dsm iliyobakia ni kati ya mikoa yenye wakaazi wachache ktk Tanzania. Sasa hao Waislamu wengi kuliko wakristo wako wapi?
mwanzo upi unaosemea wewe eti waislamu walikuwa wengi? Unaijua Tanzania wewe? Vijiji vya ndani kabisa hakuna uislam ila kanisa katoliki lipo. Unafikiri Tanzania ni Dar, Pwani, Tanga
 
Mmehangaika sana jamani kujibishana na watu wa hii Dini, moslems will not change till the second coming of jesus! unajua kwanini? lililoandikwa katika Biblia ni lazima litimie. Baba wa uslam ni ish-mael yule mtoto wa Ibrahimu aliyemzaa na mjakazi wake mmisri, HAJIRI. Mungu liandika hivi: KATIKA MWANZO 16:12[/FONT]

He will be a wild donkey of a man; his hand will be against everyone and everyone's hand against him, and he will live in hostility toward all his brothers." (QUOTED FROM ENGLISH STANDARD VERSION)

KWA BIBLIA ZA KISWAHILI ANASEMA: naye atakuwa kama punda mwitu kati ya watU, Mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote

sasa katika kiswahili Maana imepotea angalia neno lenye rangi nyekundu kwenye kingreza "hostility" kwa tafsiri nzuri ni 1. a hostile (very unfriendly) disposition 2. a state of deep-seated ill-will
3. the feeling of a hostile person 4. violent action that is hostile and usually unprovoked

Sasa kwa tafsri hizo unaweza usiwalaumu hawa waislam, neno la mungu ni lazima litimie, angalia mataifa ya kiislam yanavyoishi na mataifa wanayoyaita yana wakristo, matendo wayafanyayo duniani. NK
NISIWACHOSHE REFERENCE ZA BIBLE NI NYINGI WAACHENI WAISLAM WANAITIMIZA MISTARI YA BIBLIA

mbona hiyo nukuu yako haisemi kizazi cha Ishi-mael kitakuwa cha kiislamu?nadhani ulitakiwa kuweka mistari mingine zaidi otherwise kwa hapo umetudanganya..............
 
Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.

Shida nyinyi wenzetu mnachotaka ukorofi tu. Kila kukicha ukorofi. Rais akiwa mkristo mnagomba. Rais akiwa muislamu mnagomba. Je dini hii imetoka kwa Mungu? Duniani kote tabia ya kiislamu iko wazi wakiwa wachache wanadahi haki wakiwazidi wanawanyonga. Pkia mkitakampate kazi nzuri si muende shule mkasome? Hiyo idadi inawasaidia nini? Hata kwenye katiba mpya nyinyi hamzungumzii mambo ya taifa bali kaziyenu ni dini na kuonewa tu. Yahani nyinyi mnatisha.
 
nadhani wanazuoni wa kiislamu wanasoma hapa. Ukweli thabiti

Tuna bahati mbaya ya kutokukubaliana na ukweli kwa sababu ya imani ya dini na hofu ya kuchomwa moto ambao hatuna uhakika kama upo kweli au la. Shida nyingine inatokana na wale walioipokea dini, kwa bahati mbaya sana nao hawakuwa na elimu dunia hata kidogo. Wakawa wamekariri mambo ya ahera tu ambayo waliwarithisha na vizazi vyao vilivyofuata. Kuna nchi ambozo wamenza kusoma elimu dunia tangu kale, mfano Misri. Wako wapi leo ki maendeleo, wamepiga hatua. Irani ni mfano mzuri, ni nchi ya kiislamu lakini mfumo wa elimu dunia wameuthamini tangu kale. Leo wanatengeneza maroketi na zana za hatari. Bado akili zetu zina ukungu ndani yetu. Tunahitaji mageuzi thabiti.
 
dini mtu anaweza kubadilisha leo ni mwislam kesho akawa msabato mbona wengi tu wanabadili dini zao.kikubwa ni kulinda na kuheshimu utaifa wetu,amani na utulivu.kiongozi yeyote mwenye nia nzuri na waislamu atawahimi waqpende kusoma na kuitafuta elimu kwa nguvu zote ili siku moja watu wanaopata kazi serikalini wawe wengi.
 
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia dhulma bila bughdha
  1. Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
  2. kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
  3. Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
  4. Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?
Itaanza na waislamu wachache serikalini, baadae itakuja watu wa kusini ni wachache, itafuatia watu wa tanga na hatimae wasukuma, loo! matokeo yake ni ya hatari sana. Musio na macho hamuoni zaidi ya visingizio hivi mnavyovitoa. Naamini kwa kuwa nia zenu ni uovu, hamtafanikiwa kamwe. Walaaniwe wanaotumia fikra zenu kwa manufaa yao ya kisiasa.
 
Nyakageni. Hawa jamaa hawaijui Tanzania. Ukiondoa mkoa wa Tabora na maeneo ya mijini huku bara ni maeneo kama Ujiji,Mwanga,Kondoa na sehemu chache vijijini utawakuta Waislamu wengi. Hiyo mikoa ya pwani ukiondoa Tanga na Dsm iliyobakia ni kati ya mikoa yenye wakaazi wachache ktk Tanzania. Sasa hao Waislamu wengi kuliko wakristo wako wapi?

kutembea ni kujifunza. Kweli mkuu watu wako Dar wanafikiri wao ndo think la nchi
 
Tuna bahati mbaya ya kutokukubaliana na ukweli kwa sababu ya imani ya dini na hofu ya kuchomwa moto ambao hatuna uhakika kama upo kweli au la. Shida nyingine inatokana na wale walioipokea dini, kwa bahati mbaya sana nao hawakuwa na elimu dunia hata kidogo. Wakawa wamekariri mambo ya ahera tu ambayo waliwarithisha na vizazi vyao vilivyofuata. Kuna nchi ambozo wamenza kusoma elimu dunia tangu kale, mfano Misri. Wako wapi leo ki maendeleo, wamepiga hatua. Irani ni mfano mzuri, ni nchi ya kiislamu lakini mfumo wa elimu dunia wameuthamini tangu kale. Leo wanatengeneza maroketi na zana za hatari. Bado akili zetu zina ukungu ndani yetu. Tunahitaji mageuzi thabiti.

kweli kabisa mkuu. Wakipatikana kumi kama wewe tutasonga
 
Kuna dini zingine fahari yake ulalamishi na masononeko, mbona wapagani kila siku wakitukanwa na hizi dini zenu za kuletwa na wakoloni (waalabu na wazungu) lakini hawajawahi kunyanyua midomo yao kulalamika wala hawana wasiwasi na uwingi wala uchache wao! lakini kila siku utasikia wakristo wakisema hawa wapagani wanaamini mashetani na waislamu nao wakiwaita makhafir Achaneni na dini za kasumba za kikoloni ndiyo maana hamjiamini, ni infiliority complex hiyo. wapagani watakubali kgharamia sensa ya waumini wenu wakati mwawatukana kila siku?
Asante sana kwa kutambua uwepo wetu!
 
naamini ktk tz hakuna sensa ya waumini wa dini fulani ambayo imefanywa na serikali bali kwa wakristu huwa ni kawaida kufanya sensa yao ili kujua active members na non active members kila mwaka sasa kwa nini na wengine wasiige mfano huo? mfano kanisa Katoliki kuna jumuiya ndogondogo ambazo hukutana kimtaa na jumla yao injulikana ukijumlisha jumuiya zote katika parokia unapata idadi kamili ya waumini ktk parokia husika, sensa kama hiyo haihitaji mpaka serikali itoe pesa hata kanisa lenyewe halitoi pesa ila ni utaratibu tu Mungu amewapa uwezo wa kufikiri akawatunikia na akili kwa nini hamvitumii? kila kitu serikali iwafanyie aibu hiyo

hecko mtu wa mungu...ushauri wako ni mzuri viongozi hawa wa dini wakae chini kwan hawana mikakati yao waliojiwekea yakutambua waumini wao wako wangap kwa killa mtaa, hatimae mikoa na taifa kwa ujumla? Amken amken serikali'haina dini nyie.
 
Kwani lengo ni kuwaonyesha wengine kuwa sisi ni wengi kuwazidi?

Jumakidogo, nakubalina na wewe kabisa. Serikali ya Tanzania inataka kujua idadi ya "raia" sio "waumini". Anayetaka kujua idadi ya waumini wa dini yake ruksa lakini kwa gharama zake. Very simple.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom