Ushauri wa bure kabisa kwa wale ambao kwa ' viherehere ' vyenu huwa mnapenda Kuwakamata na Kuwafungulia Kesi ' Wakosoaji ' wa Serikali hii

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,455
108,581
Kabla ya kwenda Kukamata muwe Kwanza mnapitia ama kwa Waganga au Watabiri ili wawaambieni kama mkiwakamata na Kuwafungulia Kesi mtashinda au mtaanguka. Huu ni mwaka wa Tatu ( 3 ) sasa nimefanya ' utafiti ' wangu mdogo tu na nimegundua ya kwamba 95% ya wale ambao huwa mnawakamata tena kwa mikogo mingi mkikutana nao Mahakamani katika ulingo wa Kucheza na Sheria huwa mnaanguka vibaya na kuitia tu aibu Serikali / Jamhuri na hata pengine kuitia hasara kwa namna moja au nyingine.

Ni matumaini yangu makubwa kwamba huu ushauri wangu ' Kuntu ' kabisa mtaufanyia Kazi ili msizidi Kuumbuka na Kudharauliwa.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom