Ushauri wa Bure juu ya gari yako

mkuu hujui hata kubadili tairi ??..

Weka gari pembeni ya barabara penye usalama then weka jiwe kwenye tairi (kama pancha tairi ya mbele kulia basi jiwe weka tairi ya nyuma kushoto ) then chukua wheel spanner na jeki kwenye buti. Hiyo jeki iweke upande wa tairi ya pancha kumbuka kuiweka kwenye ule mzingo wa chasis pembeni kidogo ya tairi sio katikati ya gari.
Legeza kwanza nut za tairi zikilegea piga jeki gari iinuke mpaka tairi iweze zunguka then fungua nut toa tairi. Kama kuna maji karibu lowanisha kitambaa then futa kwanza bolt ukimaliza chukua spare tire iweke halafu funga ila usikaze kwanza.
Shusha jeki then kaza sasa nut za tairi mpaka unapoona yatosha, usikaze saana inaweza pelekea kuua tread zake!. Baada ya hapo upo huru kurudi barabarani.
NB: Kama ni hizi highway au sehemu zenye pilika inakubidi kabla hujaanza hizi mambo toa hazard light zako piga hatua moja toka kwenye gari then moja weka mbele nyingine nyuma, huna weka hata majani. Tairi za kulia zikipata pancha kumbuka kutoka sana nje ya barabara kuepuka gongwa ukiwa unabadili.

Kweli JF is never boring
 
gearbox oil (si ndio hydraulic oil ....nisahihishwe kama nakosea) nimebadili the same day nilipodadili engine oil na filter mkuu. possible courses nyingine itakuwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama umebadili gearbox oil hapo shida itakua kwenye vibati vya ku engage gia, vipi ukiweka kwenye L si inaanza kawaida na je gari ni nzito?
 
Gari langu inasumbua ukiwasha AC kwa muda mrefu ukiwa kwenye jam inakuwa inazima ghafla, pia muda mwingine huwa kama inatetemeka then unasikia kama kwenye gearbox inagonga. Msaada tafadhari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari yangu kila asubuh nikitaka kuiwasha switch inagoma kuxunguka kwenda kwenyr On. Hata nikitingisha usukani unajilock tu. Nikichezesha shana ndo inakubali kufika on na gari inawaka.baada ya hapo mchana kutwa haisumbui. Ikilala tu kesho asubuh inasumbua tena


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari yangu kila asubuh nikitaka kuiwasha switch inagoma kuxunguka kwenda kwenyr On. Hata nikitingisha usukani unajilock tu. Nikichezesha shana ndo inakubali kufika on na gari inawaka.baada ya hapo mchana kutwa haisumbui. Ikilala tu kesho asubuh inasumbua tena


Sent using Jamii Forums mobile app
switch inashida jaribu kubadilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwasha A/C kwenye gari baada ya muda kunakuwa na ukungu mwingi kwenye kioo cha mbele-windscreen mpaka nalazimika kutumia wiper. Je tatizo ni nini?
 
Mkuu kwanza asante kwa kujitolea muda wako kushare elimu yako na jamii. Gari yangu( corolla 5A ea100) kunamuda nikiweka switch on haswa engine ikiwa imepoa taa zote zinawaka katika dashboard na nikiwasha gari zinazima kama kawaida, ila nikishatembea nalo kidogo tu nikiweka tena switch on taa ya check engine haionekan katika dashboard na nikiwasha pia haionekani. Naomba ushauri wako
 
Back
Top Bottom