Ushauri wa Bure juu ya gari yako

popolon

Member
Jan 31, 2018
52
54
umiliki wa gari ukiwa haujui chochote juu ya gari yako ni tatizo kubwa sana,wengi hawana elimu yoyote juu ya magari ni mwendo wa kuweka gear na kuondoka.

ningependa kutoa nafasi hii kwa yoyote mwenye swali kuhusiana na magari alitoe hapa ili liweze kujibiwa hapa hapa kwa maana wapo wenye ufahamu zaid kwenye technology ya magari utawaza kupata ABC za magari hii itakusaidia ata unapopata tatizo la gari yako huwez kupata taharuki
Karibuni tupeane Elimu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna corolla ae100 sedan,break zake zipo mbali sana mkuu tatizo ni nini na juzi juzi tu nimefanya service
 
gari yangu escudo 1993 engine g16a tokea majuzi haipig starter nikipiga inalia "tap tap"
nikajua battery nikaja nikaboost lakin hivo hivo nimepark tokea majuzi natumia bodaboda..
Je inaweza ikawa ni starter
.???
umiliki wa gari ukiwa haujui chochote juu ya gari yako ni tatizo kubwa sana,wengi hawana elimu yoyote juu ya magari ni mwendo wa kuweka gear na kuondoka.

ningependa kutoa nafasi hii kwa yoyote mwenye swali kuhusiana na magari alitoe hapa ili liweze kujibiwa hapa hapa kwa maana wapo wenye ufahamu zaid kwenye technology ya magari utawaza kupata ABC za magari hii itakusaidia ata unapopata tatizo la gari yako huwez kupata taharuki
Karibuni tupeane Elimu.


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nifanyeje tairi likipata pancha?
mkuu hujui hata kubadili tairi ??..

Weka gari pembeni ya barabara penye usalama then weka jiwe kwenye tairi (kama pancha tairi ya mbele kulia basi jiwe weka tairi ya nyuma kushoto ) then chukua wheel spanner na jeki kwenye buti. Hiyo jeki iweke upande wa tairi ya pancha kumbuka kuiweka kwenye ule mzingo wa chasis pembeni kidogo ya tairi sio katikati ya gari.
Legeza kwanza nut za tairi zikilegea piga jeki gari iinuke mpaka tairi iweze zunguka then fungua nut toa tairi. Kama kuna maji karibu lowanisha kitambaa then futa kwanza bolt ukimaliza chukua spare tire iweke halafu funga ila usikaze kwanza.
Shusha jeki then kaza sasa nut za tairi mpaka unapoona yatosha, usikaze saana inaweza pelekea kuua tread zake!. Baada ya hapo upo huru kurudi barabarani.
NB: Kama ni hizi highway au sehemu zenye pilika inakubidi kabla hujaanza hizi mambo toa hazard light zako piga hatua moja toka kwenye gari then moja weka mbele nyingine nyuma, huna weka hata majani. Tairi za kulia zikipata pancha kumbuka kutoka sana nje ya barabara kuepuka gongwa ukiwa unabadili.
 
Asubuhi kabla ya kuanza safari kumbuka kucheki hivi:-
• Nyaya za betri kama zipo loose
• Maji ya Wiper kama yapo stahili
• Maji kwenye Radiator kama yamepungua
• Maji kwenye rejeta kama yapo stahili
• Mafuta ya brake kama yatosha
• Upepo kwenye tairi kama upo vizuri
• Washa gari isikilizie dakika kadhaa
• Inashauriwa fungua vioo kwanza then washa AC baadae ukishaanza safari ndo uvifunge!.
 
Gari ikichemsha:
Usikimbilie kuizima, iache ikae ikiunguruma then fungua boneti. Tafuta kitambaa kizito au kikubwa na maji safi mengi. Ukiwa umeshika kile kitambaa fungua Radiator valve taratibu (usiifungue kwa mara moja kuna mvuke unaweza kukuua) zungusha mpaka mwisho raditor valve then usiiitoe ila uwe unafanya kama kuinua na kurudisha chini taratibu (mantiki nzima ule mvuke upate nafasi ya kutoka).
Utakapoona hakuna mvuke unaotoka tena ndio ondoa sasa huo mfuniko, chukua maji yako uwe unamimina kwenye radiator usiogope kutokota baada ya muda yataacha (maji yawe mengi sio hizi chupa za lita 1).
Maji yakiacha tokota na yakawa yamejaa basi funga mfuniko wako na hakikisha boneti imejilock ndio ondoa gari!.
NB: Gari ikichemsha usikimbilie kuizima!.
 
Back
Top Bottom