Ushauri: Vitabu vitakatifu vya Dini Viache kutumika kwenye Viapo vya masuala ya Siasa

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,231
Kwa Jinsi mchakato mzima Wa uchaguzi unavyoenda ngazi za majimbo mpaka Taifa ,watu wamekua wakidhulumiana ,kuoneana na mambo mengine mabaya yasiyopendeza ilihali tu mtu ashike uwongozi ,mbaya zaidi ni pale mtu anaposhika Kitabu cha Dininfulani na kula Kiapo kisha siku mda mchache baadae anakuja Kukutwa na kashafa ya ubadhilifu ,hii imekua niazoea na sasa watu hawaogopi tena viapo .

Nashauri,wakati wa Viapo naona ni vyema kutumia Ilani ya Chama husika kilichoshinda au Katiba ya Nchi .

Kufanya Mazoea na Vitabu Vitakatifu sioni kama ni sahihi .

Naomba kuwasilisha.
 
Na hakuna m
Kweli kabisa, nimeshangaa sana kuona shein ameapa huku ameshika qurian takatifu na viongozi wa dini wakiwepo huku wanaelewa kilichotokea zanzibar, huku ni kumtania Mungu
Na hakuna mtu ambaye haelewi kua Mchezo mzima wa Siasa ni Figisufigisu , Sasa sijui kwann tunahusisha Hivi Vitabu ....ndio maana tunasema Tumelaaniwa .. ,kumbe tumejilaani wenyewe.
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza...

Siasa ni maigizo ...uongo uongo. ..unafki unafki...hadaa haaaaa.

Chukua jembe ukapalilie mihogo yako usiumize kichwa kujua uhalali wa viapo
 
Methali yako
Usilolijua ni kama usiku wa giza...

Siasa ni maigizo ...uongo uongo. ..unafki unafki...hadaa haaaaa.

Chukua jembe ukapalilie mihogo yako usiumize kichwa kujua uhalali wa viapo

Methali yako haiendani na mada iliyopo Mezani .
 
upo sahihi kabisa Mkuu alichofanya Shein kama mtu asie na dini harafu anaapa kwa kitabu takatifu..
 
Kwaani unadhani hawajui kwamba wamenajisi ila hakuna namna zaidi ya kujificha kwenye kichaka cha dini mbaya zaidi viongozi wetu wanawasujidia wana siasa
 
Mizaha na Mungu ni jambo baya sana, waape kwa majina ya wazazi wao labda wataheshimu viapo hivyo
 
Na hakuna m

Na hakuna mtu ambaye haelewi kua Mchezo mzima wa Siasa ni Figisufigisu , Sasa sijui kwann tunahusisha Hivi Vitabu ....ndio maana tunasema Tumelaaniwa .. ,kumbe tumejilaani wenyewe.
Na hakuna watu wanao ongoza kwa unafiki kama viongozi wa dini tanzania wakati mwingine huwa naona sadaka yangu bora niwape yatima kuliko hawa watu
 
Kwa Jinsi mchakato mzima Wa uchaguzi unavyoenda ngazi za majimbo mpaka Taifa ,watu wamekua wakidhulumiana ,kuoneana na mambo mengine mabaya yasiyopendeza ilihali tu mtu ashike uwongozi ,mbaya zaidi ni pale mtu anaposhika Kitabu cha Dininfulani na kula Kiapo kisha siku mda mchache baadae anakuja Kukutwa na kashafa ya ubadhilifu ,hii imekua niazoea na sasa watu hawaogopi tena viapo .

Nashauri,wakati wa Viapo naona ni vyema kutumia Ilani ya Chama husika kilichoshinda au Katiba ya Nchi .

Kufanya Mazoea na Vitabu Vitakatifu sioni kama ni sahihi .

Naomba kuwasilisha.

Sasa ukitumia kiapo cha chama we unaona ni sahihi kweli? kwa haraka naona mawazo yako umekurupuka coz binadamu wote tunaamini katika maandiko tuliyoyakuta na tutakayoyaacha kwa Imani ya din zetu ndio maana kwenye kila jambo liwe zuri au baya tunamshirikisha Mungu yeye ndio anajua juu yetu wote sisi binaadamu
 
Back
Top Bottom