Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Kwasasa Ofisi zote za kiserikali, achilia mbali Ikulu, zimehalia Dodoma katika utekelezi wa Sheria na agizo la kuhamia Makao Makuu ya nchi Dodoma. Lakini, bado kuna baadhi ya ofisi zinaendelea na huduma ndani ya Dar es Salaam.
Pia, bado kuna vikao mbalimbali vya kiserikali na kichama vinafanyika Dar es Salaam. Katika hilo, safari za viongozi na watumishi wa Serikali kwenda na kutoka Dodoma ni za mara kwa mara. Ni kwa ajili ya kuhudhuria vikao Dodoma au Dar es Salaam; kupeleka nyaraka na kadhalika.
Jana, kwa mfano, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alisafiri kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya CCM kinachotajwa kufanyika leo. Msafara wa Spika ulinipita jana jioni maeneo ya Kibaha. Hakika, ulikuwa kasi na 'ulifanya kila linalowezekana' uwahi Dar es Salaam.
Nashauri viongozi wetu wapewe taarifa za vikao au safari mapema ili wasafiri mapema na kwa utulivu. Hii itapunguza mwendo kasi wa viongozi wetu na watumishi wa umma na kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza.