johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 82,754
- 139,571
Pamekuwepo na utaratibu usio rasmi ambapo ama katika nyumba za Ibada au ofisi za viongozi wa dini kupeperushwa bendera ya taifa. Utakuta ofisini kwa mchungaji au sheikh mezani kwake kuna bendera ya taifa inapepea kama ilivyo kwa viongozi wa serikali. Na katika baadhi ya makanisa utakuta bendera ya taifa inapepea pale madhabahuni. Sasa mada yangu ni kuishauri tu serikali iweke utaratibu mzuri kwa wote wanaopeperusha bendera ya taifa wakiwemo viongozi wa dini kuwa " kioo" cha maadili mema mbele ya jamii. Haiwezekani kukuta kiongozi wa dini aliyepungukiwa maadili na jamii inamuelewa hivyo akipeperusha bendera yetu ya taifa na sisi tukakaa kimya, tumnyang' anye! Ni hayo tu, asubuhi njema!