Ushauri: Vijana wanaochangishana kumsaidia Sabaya wafuatiliwe, wana nia ovu ya kuzuia haki isitendeke(obstruction of justice), pia wanatukana Serikali

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,983
20,634
Hawa ni lile kundi ambalo mimi nimelichana hapa JF hivi karibuni, lina mambo ya hovyo sana. Hili kundi linachangishana pesa huku likitoa maneno ya kashfa kwa mkuu wetu. Nina wasiwasi wana lengo la kuzuia haki isitendeke.

Vyombo vya kisheria na vya kidola viwakamate, viwahoji na ikibidi wapelekwe mahakamani. Kukamatwa kwao hakutawashangaza kwa kuwa hata wao walikuwa wanachongea watu wengine wakamatwe.
 
Wanachangishaje wakati 7baya anapewa sehemu ya mshahara wake. Sabaya hajahukumiwa bado.

Wanaochangisha wanaleta taharuki kama Saya kaonewa wakati hukumu bado.Hao washughulikiwe Mara moja wachochezi
 
Mbona kina Mbowe na viongozi wengne wa Chadema tuliwachangia pale walipopatikana na hatia mahakamani na walikuwa wakikejeli na kudhihaki Serikali, kwann kwa Sabaya iwe nongwa?

Pili, michango kwa huyó Sabaya kunaathirije mwenendo wa kesi mpaka vyombo vya dola viwakamate?

Kwani kuchangia mtu pesa ni uvunjifu wa sheria?
 
Mbona kina Mbowe na viongozi wengne wa Chadema tuliwachangia pale walipopatikana na hatia mahakamani na walikuwa wakikejeli na kudhihaki Serikali, kwann kwa Sabaya iwe nongwa...
Huyu Sabaya ni mhalifu
 
Mbona kina Mbowe na viongozi wengne wa Chadema tuliwachangia pale walipopatikana na hatia mahakamani na walikuwa wakikejeli na kudhihaki Serikali, kwann kwa Sabaya iwe nongwa...
Bila shaka na we umo! Kumbe ni kweli.
 
Huyu Sabaya ni mhalifu
Ni swala la muda tu mkuu, ila nakwambia wazi Maza anajua beat anayopiga kapata dancers wa kutosha

Hivyo baada ya muda hii ishu ya huyu dogo itakuwa haina kiki tena kisha baadae utasikia 'DPP hana nia ya kuendelea na kesi..'
 
Hawa ni lile kundi ambalo mimi nimelichana hapa JF hivi karibuni, lina mambo ya hovyo sana. Hili kundi linachangishana pesa huku likitoa maneno ya kashfa kwa mkuu wetu. Nina wasiwasi wana lengo la kuzuia haki isitendeke.

Vyombo vya kisheria na vya kidola viwakamate,viwahoji na ikibidi wapelekwe mahakamani. Kukamatwa kwao hakutawashangaza kwa kuwa hata wao walikuwa wanachongea watu wengine wakamatwe.
Mimi si mshabiki wa Sabaya. Ila ni mshabiki wa uhuru wa watu.

Waachie wachangishane, ni haki yao ya kikatiba.

Kutoa maneno ya kashfa kwa mkuu pia ni haki yao ya kitatiba.

Una jingine?
 
Hawa ni lile kundi ambalo mimi nimelichana hapa JF hivi karibuni, lina mambo ya hovyo sana. Hili kundi linachangishana pesa huku likitoa maneno ya kashfa kwa mkuu wetu. Nina wasiwasi wana lengo la kuzuia haki isitendeke.

Vyombo vya kisheria na vya kidola viwakamate,viwahoji na ikibidi wapelekwe mahakamani. Kukamatwa kwao hakutawashangaza kwa kuwa hata wao walikuwa wanachongea watu wengine wakamatwe.
Mkuu usijali ,kila anaeshirikiana na Sabaya ambaye amefutwa katika pembe nne za dunia ,nae amefutwa ,ilisha kuwa ,wajinga tu waweza angaika na jambazi
 
Mkuu unazungumziaje Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar kuhamasisha wananchi wawachangie mashekhe wa Uamsho ambao kwa sasa wako nje??

Hilo hulioni?? Hukuliona??
 
Hawa ni lile kundi ambalo mimi nimelichana hapa JF hivi karibuni, lina mambo ya hovyo sana. Hili kundi linachangishana pesa huku likitoa maneno ya kashfa kwa mkuu wetu. Nina wasiwasi wana lengo la kuzuia haki isitendeke.

Vyombo vya kisheria na vya kidola viwakamate,viwahoji na ikibidi wapelekwe mahakamani. Kukamatwa kwao hakutawashangaza kwa kuwa hata wao walikuwa wanachongea watu wengine wakamatwe.
Umeliona wapi hilo kundi, mbona unaandika kama umelewa hivi!

Huwezi kueleza vizuri ni kundi gani hilo na wanachangishana pesa wapi na hizo pesa ni za kazi gani, kununua silaha za kupambana na polisi ili wamtoe Shabaha mahabusu?
 
Binafsi ninampenda KOMREDI SABAYA......

Ila hili linalofanyika ni sawa na KUTOZIAMINI MAMLAKA zilizomteua na zinazoendesha KADHIA HIYO......

Ukweli UTAJULIKANA TU...hamaniko la nini kwetu vijana ?!!!!

#KaziIendelee
#JMTKwanzaKablaYaChochote
 
Back
Top Bottom