Ushauri utakaomsaidia mama aliyejifungua kwa njia ya upasuaji kupona haraka, ili upate muda wa kutosha kumjua na kumlea mtoto wako

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Pata Mapumziko ya Kutosha,

Kujifungua kwa njia ya upasuaji ni upasuaji mkubwa. Kama ilivyo upasuaji mwingine, mwili wako unahitaji mda wa kupona baada ya hapo. Tegemea kubaki hospitali kwa siku tatu mpaka nne baada ya kujifungua (au zaidi ya hapo kama kulitokea tatizo lingine la kiafya), kisha upe mwili wako wiki sita kupona kabisa.

Ni rahisi kusema zaidi ya kutenda. Ni vigumu kwenda kulala kwa masaa kadhaa huku una mtoto anayehitaji uangalifu mwingi kutoka kwako.

Huenda umesikia ushauri huu wa “lala kila mtoto wako akilala” kwa marafiki na ndugu zako wa karibu. Wako sahihi. Jaribu kulala kila mtoto anapolala. Omba msaada wa kubadilisha nepi na kazi mbalimbali za nyumbani kwa rafiki na ndugu zako wa karibu ili upate muda wa kupumzika kidogo pale inapowezekana. Dakika chache za kupumzika hapa na pale katikati ya siku zinasaidia.

Uangalie Mwili Wako
Kuwa makini zaidi kila unachofanya huku ukiendelea kupona. Epuka kupanda na kushuka ngazi kadiri uwezavyo. Weka mahitaji muhimu ya mtoto na wewe (chakula, nepi, kanga,nguo zako na mtoto) karibu na wewe ili usiamke kila mara.

Usinyanyue kitu chochote kizito zaidi ya mtoto wako. Omba msaada kwa mpenzi/mme wako au rafiki au ndugu yako.

Ni vizuri ukashika sehemu ya kidonda kila unapokohoa au kupiga chafya.

Inaweza kukuchukua mpaka wiki nane kurudia ratiba zako za kwaida. Ni vizuri kumuuliza daktarin wako lini inafaa wewe kufanya mazoezi tena, kurudi kazini na kuendesha gari. Pia subiria mpaka daktari atakapo kuruhusu kujamiana tena.

Epuka mazoezi mazito, ila unaweza kufanya mazoezi mepesi kama kutembea taratibu kila unapoweza. Mzunguko huu utasaidia mwili wako kupona na kuzuia tatizo la kukosa choo na damu kuganda. Pia kutembea ni moja ya njia ya kumtambulisha mtoto katika ulimwengu.

Kama unavyoangalia afya yako ya mwili usisahau hali ya hisia zako. Kuwa na mtoto inaleta hisia ambazo hujawahi kutarajia. Kama ukisikia kuchoka,huzuni au kuvunjika moyo usizipuuzie hisia hizo. Ongea na rafiki yako wa karibu,mwenzi wako, daktari yako au hata mshauri nasaa.

Punguza Maumivu Yako ya Mwili
Katika wakati huu unaonyonyesha, ni vema kumuuliza daktari au mkunga wako dawa gani ya maumivu unaweza tumia.

Kulingana na kiwango cha maumivu, daktari atakuandikia dawa ya kupunguza maumivu au kukushauri utumie dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen (Advil,Motrin)

Unaweza kutumia mpira wa maji ya moto kupunguza maumivu katika eneo la mshono na tumbo la chini kwa ujumla, hakikisha unatumia maji ya uvuguvugu.

Lenga katika Ulaji wa Lishe Bora.
Lishe bora ni muhimu katika miezi baada ya kujifungua kama ilivyokuwa kipindi ukiwa mjamzito. Bado wewe ni chanzo kikuu cha virutubisho kwa mwanao kama unanyonyesha. Kula vyakula vya kila aina itasaidia mtoto kukua katika afya na nguvu.

Utafiti unaonyesha ulaji wa mbogamboga za majani wakati unanyonyesha unasaidia kuyapa maziwa ladha ambayo inaongeza kasi ya mtoto kunyonya na kufurahia maziwa ya mama kadiri anavyokua.

Pia kunywa vimiminika vingi, hususani maji. Unahitaji vimiminika vya ziada kuongeza upatikanaji wa maziwa na kuzuia kukosa choo.

Wasiliana na Daktari Endapo:
Bado utapata maumivu katika eneo la mshono, unaweza kutoka damu au kutoka usaha mpaka wiki ya sita baada ya upasuaji. Hii ni kawaida.

Lakini dalili zifuatazo zinakupa haki ya kuwasiliana na daktari wako, kwasababu zinaweza kuwa ishara za maambukizo:

Kuvimba, uwekundu, au usaha kutungika katika mshono
Maumivu kuzunguka mshono
Homa kali zaidi ya 38⁰C (100.4⁰F)
Usaha wenye harufu mbaya kutoka ukeni
Kutoka damu nyingi ukeni
Kuvimba au uwekundu katika ngozi ya miguuni
Kupumua kwa shida
Maumivu ya kifua
Maumivu ya matiti
Pia wasiliana na daktari wako kama unasikia huzuni na unyonge.

Mwisho kabisa, kama una rafiki au ndugu ambaye alipitia hali hii ya kujifungua kwa njia ya upasuaji, usijilinganishe nao. Kila mwanamke ana uzoefu wa tofauti katika njia hii ya kujifungua. Lenga katika kupona na upatie muda mwili wako kurudia hali yake ya awali.
 
Back
Top Bottom