Ushauri: Utafanya nini kama umekosa mkopo na muda wa chuo umefika?

geniusMe

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
1,312
1,773
Hatua gani unaweza kuchukua endapo umekosa mkopo na muda wa kwenda chuo umefika?

1) Kuendelea kutolipa ada na kuendelea kusubiria mkopo ukiwa chuo.

Katika experience yangu niliyopitia niliona vijana wengi ambao walikuwa wanaendelea kusoma chuo huku wakisubiri mkopo kutoka. Kama wasemavyo mvumilivu hula mbivu. Kuna wanafunzi kadhaa walipata mkopo wakiwa chuo wanasubiria bodi kumaliza process za mkopo.

Njia hii inahitaji kuwa mjanja na kujichanganya na wenzio ambao wanaweza kukubeba kwa muda huo unaokuwa unasubiria maana kuna vyuo vingine hawakupi hostel kama haujalipa ada hata kama umelipia gharama za hostel, kwa hapa kwetu utaratibu huo ulikuwa katika college yetu, college nyingine ulikuwa unapata hostel kama kawaida hata kama haujalipa ada.

Njia hii huwa ngumu kwa mwaka wa kwanza kwani huwa wanapenda kuona wanaingia chuo wakiwa kamili kwa kila kitu wanasahau hata hao continuous student wengine kulipa ada ni mpaka pale wanaposubiria matokeo ya mitihani ya semester, mpaka pale matokeo yanapozuiliwa.

Kwa vyuo vya serikali usajili huendelea mpaka mitihani ya semester inapokaribia, japokuwa kuna sheria baada ya wiki tatu za usajili hakuna mwanafunzi anayeruhusiwa kusajiliwa lakini hizo ni sheria tu za kwenye makaratasi kwa vyuo vya serikali huwa hawazifuati.

2) Kulipa ada na kuendelea kusubiri mkopo ukiwa chuo.

Unaweza kulipa ada huku ukiendelea kusubiri mkopo. Kuna watu kadhaa nawafahamu ambao waliamua kulipa kuondokana na usumbufu huku wakisubiri mkopo.

Kuna baadhi ya wanafunzi walipata mkopo lakini hawakuwepo chuo hivyo walishindwa kupata taarifa kama wamepata mkopo baada ya batch kadhaa bodi husimamisha zoezi la kutoa mikopo kwa kituma majina katika mtandao, mikopo hutumwa moja kwa moja chuo.

Mfano mimi nilipata awamu ya tano huko nilikuja kupigiwa simu kwenda kusign ada na boom kipindi hicho majina yalikuwa yametoka kama week mbili hivi sikuweza kuyaona maana chuo majina ni mengi alafu nilikuwa nimekata tamaa ya kupata hivyo nikawa sina habari nao. Baada ya kufanya hivyo boom nikalipata semester ya pili ya mwaka wa kwanza, semester ya kwanza yote nilikuwa najitegemea mwenyewe.

Kuna majina mengi ambayo baadae bodi huleta mkopo lakini watu hao wanakuwa hawapo chuo kabisa hivyo yanarudishwa bodi kwamba jamaa hayupo chuo.
 
Yaah! Afu kuna jamaa alipataga loan batch ya mwisho huko, Sasa mwanzo hakuwa amefanya registration chuo yaani hakwenda alivyoona hana loan, after kupata loan anataka aende chuo akaanze usajili, ile kufika akaambiwa usajili umefungwa, yupo mtaa paka sasa.
 
Yaah! Afu kuna jamaa alipataga loan batch ya mwisho huko, Sasa mwanzo hakuwa amefanya registration chuo yaani hakwenda alivyoona hana loan, after kupata loan anataka aende chuo akaanze usajili, ile kufika akaambiwa usajili umefungwa, yupo mtaa paka sasa.
Kuna wakati hawa jamaa wa loan bord wanafanya mambo ambayo hatuyaelewi maana kwa changamoto kama hizo lazima wahusika wazijue ili watu wasiwe wanakwama kama hivyo ili hali kwa tafsiri halisi mkopo ni deni ambalo lazima ulipe bila kujalisha ni mtoto wa maskini au tajiri .kumbuka Leo ni kukopeshwa ni kipaumbele kwa Sera ya watoto wa maskini lakn kwenye kulipa hawazingatii hill
 
Back
Top Bottom