Ushauri unahitajika: Rafiki yangu kafunguliwa kesi na mke wake

Tusipende kujudge upande mmoja ukute huyo jamaa ndo mwenye matatizo ndani ili awe safe side atajitetea kwa kutafuta hoja, binadamu tulivo, anaweza akawa na makosa 75% mkewe zilizobaki but Inaonekana mwanamke ndo mwenye makosa yake hajataja hapa
 
Kwanza mambo yakupigana ya nini jamani? huyo rafiki yako nae wa mwaka gani mpaka anapiga mwanamke? mwache akafungwe ana stahili kufungwa,kama mke mchafu mpaka amezaa nae mda wote huo hakuona akajipanga kabla haja zaa nae? alimuiba kwa mtu au alikua mwanamke wake kwanza mda wote huo hakuona uchafu wake sasaivi ndio kamuona kua anaoga mara moja kwa siku na msuwaki kupiga mgogoro? mbona wana seem kua wamezoweana tabia na mazingira,
ivi kweli mwanamke mchafu kama wewe kweli msafi huwezi kumstahmilia hata robo siku na sasa iweje yeye avumilie
kote huko sasa ndio kashindwa?...
 
Huenda housegirl alikuwa anauogesha na kumpisha mswaki ndio maana baada ya housegirl kuondoka akauona uchafu wa mkewe. Maana kama ni vyombo na kudeki wangesaidiana ukizingatia kuna mtoto wa miezi 3. Mmeishi zaidi ya mwaka hujaweza kumuinfluence mkeo kuongeza usafi unategemea kipigo kitambadilisha?
 
Huyo rafiki yako angeamka mapema wakati mkewe anahangaika na mtoto akasafisha nyumba ingekuwaje? Di inahitaji mikono 2 na miguu 2 kufanya usafi? Sioni sex organ ikitumika hapo. Halafu angekuwa anamualika mkewe kuoga pamoja haoni kama angembadilisha. Kuna njia zaidi ya moja kutatua tatizo, kupiga haijawahi fanya kazi kwa mtu mzima.
Huyo ashashindikana tu kama mtu hapendi kuoga ahata ukimualika......kazi ipo hapo na kibao kitamfundisha jamaa kuwa njia ya kibao sio sahihi kwa aina ya mwanamke aliyenaye
 
Hizo ni hasira tu za mkewe zikipungua atajutia uamuzi wake kwa kufikia hatua hiyo ni dhahiri mwanamke amechoka sana na kazi za nyumbani,ofcn,malezi ya watoto,jamaa alitakiwa kumsaidia mkewe kazi ndogo ndogo mpaka beki3 arudi lakini ukiendekeza ukubwa na maguvu mwisho ndio kama hivo.
 
Dah walimu kumbe nawenyewe wachafu hivyo vyombo vyasiku tano dah! alafu usikute huko shuleni anafundisha somo lasayansi
 
Hizo ni hasira tu za mkewe zikipungua atajutia uamuzi wake kwa kufikia hatua hiyo ni dhahiri mwanamke amechoka sana na kazi za nyumbani,ofcn,malezi ya watoto,jamaa alitakiwa kumsaidia mkewe kazi ndogo ndogo mpaka beki3 arudi lakini ukiendekeza ukubwa na maguvu mwisho ndio kama hivo.
Uliona wapi. Wanaume wa bara wakamsaidia mkewe kazi? ni full mfumo dume tu. Kwa kwenda mbele
 
Dah walimu kumbe nawenyewe wachafu hivyo vyombo vyasiku tano dah! alafu usikute huko shuleni anafundisha somo lasayansi
Usijudge upande mmoja maana kuna watu wanatabia ya kuongeza maneno ili yeye aonekane descent
 
Leo nilikuwa na rafiki yangu jioni alinipigia simu niende kwani alikuwa amegombana na mke wake.

Huyo mkewe akaondoka akamuacha na mtoto wa miezi 3 mpaka saa 3 usiku bado huyo mkewe hajarudi tokea saa 11.

Sasa kanpgia simu mkewe karudi but kwa maongez aliyoyaskia mkewe akiongea na mama yake ni kwamba huyo mwanamke kamfungulia kesi polisi na ana RB ya jamaa..but jamaa kasema haendi kokote anasubiri akamatwe may be tomorrow.

KOSA: huyo mkewe kwa maelezo ya jamaa ni mvivu sana na ni mchafu na wote wanafanyakazi.

Mkewe ni mwl..binti wa kaz amesafiri kdogo sasa jamaa anadai asbh nyumba ilikuwa chafu sana vyombo vinanuka vya siku tano vimerundkwa.

Mkewe mwenyewe kuoga ni shida mara moja per day, mswaki mzozo jamaa asbh akamuwakia mkewe akamjbu hana muda jamaa kamrushia kibao mkewe kwa maelezo ya jamaa akamtukana pumbavu jamaa aliwaka vibaya.

Ndo jion wamerud kazn mara mkewe nduki hakujua anaenda wapi at ze end ndo alchorudi nacho.
Hapo hakuna haja ya ushauri bali mwanamke akishakufungulia kesi huyo si mke tena pambana naye kama adui mwingine yeyote. Isitoshe ukiona hivyo ujuwe nyuma yake kuna mtu tayari
 
Hayo ndo madhara ya kukimbilia kufunga ndoa kabla hamjachunguzana ktka kpnd cha uchumba jaribu kuishi na mwenz wako japo miez 6 tu lazma utamjua tabia zake.Na wanawake wa dizain hyo ni wale mboga 7 utakuta mdada mzuri lakin hata kujisafisha kwa bibi hawez kazi kubandika mikucha mirefu kama mchawi karaba.
 
Eeh jaman kwan hd ana muoa hakumjua km mchafu,na huko police huwa wanajioneag vituko kwakweli
 
Back
Top Bottom