Ushauri unahitajika: Mke wa rafiki yangu akutwa na VVU

Dezoizo52

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
527
1,064
Ni rafiki yangu wa utotoni mpaka sasa ni ndugu yamemkuta mazito ktk maisha yake.Hapo nyuma hakuwahi kuniambia jambo zito akiwa analia na hudhuni tele amechanganyikiwa.

Mke aling'ang'nia kwenda kusalimia kwao akakaa zaidi ya miezi sita tangu arejee hana hata miezi miwili amegundulika hospital kuwa ameumia na hii ni baada ya kuugua ghafla ndiyo akaomba majibu na yamekuwa haya.

Rafiki anampenda Ila amesalitiwa na ukimwi juu,amepima rafiki hajaambukizwa bado.
 
Ni rafiki yngu wa utotoni mpaka sasa ni ndugu yamemkuta mazito ktk maisha yake.Hapo nyuma hakuwahi kuniambia jambo zito akiwa analia na hudhuni tele amechanganyikiwa.Mke aling'ang'nia kwenda kusalimia kwao akakaa zaidi ya miezi sita tangu arejee hana hata miezi miwili amegundulika hospital kuwa ameumia na hii ni baada ya kuugua ghafla ndiyo akaomba majibu na yamekuwa haya.Rafiki anampenda Ila amesalitiwa na ukimwi juu,amepima rafiki hajaambukizwa bado.
Kwani ukimwi nao siku hizini ugonjwa wa kuugopa kiasi hicho?? Watu wanadunda nao tangu miaka ya 90hadi sasa , kwa sas nahofia cancer na kisukari kwanza sio ukimwi.
 
ni kwa muda gani wameshiriki tendo toka arudi?kama ni ndani ya miezi mitatu inawezekana yupo kwenye window period.alitumia kondom?cha msingi asishiriki nae tendo bila kinga na asubiri baada ya miezi mitatu apime tena.kuna watu huwa nawaambia waliopo kwenye risk kubwa ya kupata maambukizi ni wanandoa huwa hawaamini
 
Kwani ukimwi nao siku hizini ugonjwa wa kuugopa kiasi hicho?? Watu wanadunda nao tangu miaka ya 90hadi sasa , kwa sas nahofia cancer na kisukari kwanza sio ukimwi.
Duuh..! Haya maneno ya hatari kabisa.Ukimwi bado ni tatizo kwa kuwa linahusiana na kupoteza uhai.Kumbuka uhai ni tunu aliyotupa muumba mara moja na ukikutoka ndiyo basi tenaa.
 
Mkuu big IQ jamaa ni mkewe kumbuka kwa wanandoa kwa muda wa miezi miwili inawezekana wamedate mara nyingi tuuu
 
Ukimwi ni ugonjwa kama mengine tu, cha muhimu waishi kwa kufuata taratibu za kitabibu na ndoa yao itakuwa na amani kwa muda mrefu
Kwani magonjwa mengine haupotezi uhai? unaijua cancer,kisukari,homa ya ini au kufeli kwa figo? usiombe yakupate hayo kiongozi utaona ukimwi ni sawa na malaria tu. kwa hiyo sijaona sababu ya wewe kushtuka au kumpa ushauri wowote zaidi ya yeye kufuata ushauri wa kiafya ambao atapewa na madaktari.
 
Kwani ukimwi nao siku hizini ugonjwa wa kuugopa kiasi hicho?? Watu wanadunda nao tangu miaka ya 90hadi sasa , kwa sas nahofia cancer na kisukari kwanza sio ukimwi.
Ukimwi bado unaogopwa mkuu, kuna uhusiano kati ya kisukari na HIV, kuna uhusiano wa HIV na cancer kama Kaposi sarcoma, lymphomas, leukemia. Sipingi ulichokisema ila kwenye upungufu wa kinga due to HIV mwili unakuwa vulnerable kuwa attacked na ugonjwa wowote.
 
Sasa anataka nini hapo? Mungu kamponya dhidi ya hilo shetani, namuita shetani sababu ni mke ila kaenda beba ugonjwa maana yake alisaliti ndoa, apigwe chini huyo!! Labda awe aliambukizwa kwa vifaa vya ncha kali kinyume na hapo huyo hamfai hata kidogo!
Hivi unaishije na mtu baye awali hakuwa na ugonjwa tena ni mkeo alafu ghafla kaupata?? Yaani hakukujali dhidi ya tamaa zake mpaka akatiwa tena bila kinga?? Huyo hafai aisee, wafanye mchakato tu kama kuna watoto, maamuzi magumu yafanywe!
 
  • Thanks
Reactions: GUI
Back
Top Bottom