Ushauri unahitajika kumsaidia mdogo wangu

KingPower

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
1,098
1,745
Habari wakuu poleni na majukumu

Naomba ushauri mdogo wangu amemaliza chuo Bachelor degree in Electrical engineering mwaka 2018. MUST
Ila ana Diploma ya electrical engineering.

Baada ya kumaliza mwaka 2018, Mungu akamjaria akapata ajira Tanesco(2019) kwa cheti cha Diploma as (Technician) ila ni ya Temporary mkataba wa mwaka then ana renew sasa ivi ni mkataba wa 2 Now!

Analipwa around 790K,

Tamisemi waliopo Tangaza ajira za ualimu aliomba kwa cheti cha Bachelor na amepagwa Tanga Tech.

Ambapo analipwa around 750K ni ajira ya kudumu (permanent) vitu kama Bima ect viko offered ukilinganisha na hapo awali ambapo alikua hapati

Hapa ananiomba ushauri je aachane na Tanesco au aendelee

Maana akienda ualimu watu wa HESLB watapita nae na makoroni kibao
Salary itakua ndogo ila security ya kazi ni kubwa

Au abaki Tanesco apate take home ya 680,000/= pamoja na overtime + safari
Ila security ya kazi ni ndogo

Maana alisha niambia yeye na DM wake hawaelewani vzr ni Mtu anaemchukulia poa plus zengwe kibao

Nimshauri kipi karibuni
 
Nasota kurudi serikalini mpaka dk hii mambo ni Moto nimeenda utumishi wananiambia nikawe balozi kwa vijana niwambie wasiache kazi serikalini bila kufuata utaratibu ndiyo ujumbe niliopewa. Namshauri abaki kufundisha huku anatafuta connection ya kuhamia tanesco kwa kutumia taratibu za kuhama kutoka taasisi nyingine ndani ya serikali.​
 
Aende tu ualimu maana tunakoelekea hao watu wa Helsb watakua kama maji huwezi kuwakwepa huataki kajiajiri napo utapatwa tu so angalie penye fyucha,anyaway pia ajue huko kwenye ualimu kuna pensheni so achanganye za kuambiwa na zake,atachagua maisha yake maana kila mtu na staili yake ya kutafuta ugali
 
Shukrani mkuu nimekuelewa
Nasota kurudi serikalini mpaka dk hii mambo ni Moto nimeenda utumishi wananiambia nikawe balozi kwa vijana niwambie wasiache kazi serikalini bila kufuata utaratibu ndiyo ujumbe niliopewa. Namshauri abaki kufundisha huku anatafuta connection ya kuhamia tanesco kwa kutumia taratibu za kuhama kutoka taasisi nyingine ndani ya serikali.​
 
Thanks Mkuu nimekupata
I will consider this
Aende tu ualimu maana tunakoelekea hao watu wa Helsb watakua kama maji huwezi kuwakwepa huataki kajiajiri napo utapatwa tu so angalie penye fyucha,anyaway pia ajue huko kwenye ualimu kuna pensheni so achanganye za kuambiwa na zake,atachagua maisha yake maana kila mtu na staili yake ya kutafuta ugali
 
Kibarua na ajira vitu viwili tofauti

Kibarua kina umri kuna umri ukifika hatakuwa na uwezo wa kuwa kibarua na kuparamia juu ya nguzo

Pia ukibarua unategemea uzima ukiumwa imekula kwako siku haiingii!!!

Kazi ya kudumu ni bora kuliko kibarua kisicho na uhakika miradi ikikamilika atarudi kuwa jobless mitaani sababu vibarua Tanesco HUCHUKULIWA kazi zikiwa nyingi zikipungua wanapunguzwa na zikiisha wanabaki wale tu walioajiriwa kufanya routine maintanance.

Sasa hivi miradi ya kusambaza umeme mingi lakini ina muda muda si mrefu itakata hapo atakula jeuri yake ya kudharau ajira ya kudumu
 
Sorry point of correction

Ajira za mikataba ni tofauti kidogo na STE

Ila kuna favour hawazipata kama ambayo watu wa permanent (company number) hupata
Vitu kama Bima ya afya ect

Ila kweny mkataba wao kuna options ya PSSSF tu pension ambapo mwajiri anamchangia 18% ya mshahara wake.

Ila hawawi treated kama Permanent vitu kama sabuni, units za sawa na bure hawapati.
Kibarua na ajira vitu viwili tofauti..
 
Akusanye hela akajiajiri maana kapata pakuanzia tayari. Ama la arnde ualimu huku afungue ofisi yake ya mambo ya umeme au afanye partnership na mtu wa uhakika.

Achague mwenyewe anataka kuishi kibepari au kuishi kitumishi. Apo akili kumkuchwa.
 
Sorry point of correction

Ajira za mikataba ni tofauti kidogo na STE...
Viko vitu vingi vya kuangalia kama uwezekano wa kupanda mshahara,vyeo nk kibarua atabaki kibarua tu haji geuka kuwa meneja tawi la Tanesco!!! pia kuna suala la ulemavu akiparamia nguzo akadondoka nayo miguu yote ikabomoka ndio mwisho wa kibarua TANESCO!!!
 
Thanks hapa nimekuelewa
Viko vitu vingi vya kuangalia kama uwezekano wa kupanda mshahara,vyeo nk kibarua atabaki kibarua tu haji geuka kuwa meneja tawi la Tanesco!!! pia kuna suala la ulemavu akipoaramia nguzo akadondoka nayo miguu yote ikabomoka ndio mwisho wa kibarua TANESCO!!!
 
Hapo anawaza kuacha mshahara mkubwa ila job security hakuna na kwenda kwwnye mshahara mdogo wenye job security, aende tu akafundishe kwa sababu hakuna siku tanesco watamuajiri sababu alikua kibarua wao, kazi zote utumishi.
 
Temporary mkataba wa mwaka then ana renew sasa ivi ni mkataba wa 2 Now!
najua watu kadhaa walioanza na mkataba Tanesco na wote wakapata permanent
akae Tanesco, japo uvumilivu unahitajika,
uko Tamisemi panga la HESLB analijua ?
 
Kwa taarifa yako mkopo wa HESLB haushi watakukata mpk unastaafu
Injinia anayeenda ualimu lazima akasome ualimu mwaka mmoja ili aje apewe ajira ya kudumu ualimu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom