Ushauri unahitaji kuhusu kozi hizi na vyuo hivi

Kwa hizo kozi na vyuo anavyotaka ku apply ushindani unakuwa mkubwa uwezekano wa yeye kukosa ni mkubwa kutokana na matokeo yake.

Ila vipo vyuo vingine kama SAUT ya mwanza anaweza akasoma bachelor of arts in Economics kwa mwaka wa tatu atakutana na hiyo AGROECONOMIC

Kuhusu swala la mkopo huwezekano upo wa yeye kupata kama atakuwa na uhitaji
Shukrani mkuu, ni vyuo gani vinatoa kozi ya kilimo na biashara au kilimo na uchumi
 
Amesoma EGM na amepata matokeo haya
Economics .....D
Geography ......D
Advanced Mathematics ....F

Matokeo ya O-level ni haya
Commerce ....C
Bookkeeping ...C
Mathematics ......C
Geography ........C
English .......A
Biology .........A
English .......A
Kiswahili ....C
Civics.....
Anataka ku-apply
1.Bachelor of science in Agricultural Economy and Agribusiness inayotolewa pale Sokoine University of Agriculture . Ina uwezo wa kidahili watu 311. Kwa ushindani uliopo na falsafa ya chuo anaweza akapata nafasi ya kudahiliwa hapo chuoni?

2.Bachelor of science agricultural and natural resources economics and business. Kozi hii inatolewa University of Dar es Salaam (UDSM), ambayo ina uwezo wa kudahili watu 205 . Je anaweza akapata nafasi ya kudahiliwa?

Ni kwamba ana-Interest na masomo ya kilimo na biashara ndio maana anataka asome kati ya hizo kozi.

Je anaweza akapata mkopo? Kwani amesoma shule binafsi O-level na kwa Advanced level amesoma shule ya Serikali.

Mwenye kutia neno, ushauri,pendekezo Karibu sana.
Ni DM nikupe maelekezo kaka kuhusu hiyo kozi UDSM
 
Mkopo anaweza pata kama akipata chuo, ila kwenda UD au SUA kwa matokeo hayo ni ngum sana,..afu anapenda course za science wakati MATH ana F, anazingua asee.
 
Kwa hayo matokeo, course zote mbil hawezi pata, had hapo aanze kutafuta diploma courses then akimaliza ndio aunge degree kwa hizo course anazohitaji
 
Agribusiness ndiyo most competetive pale SUA hivyo kwa matokeo hayo asahau, UDSM kozi hiyo ni mpya na bado hazijafahamika kwa wengi hivyo ushindani upo chini. Matokeo haya hayaridhishi ukilinganisha na ufaulu wa mwaka huu. Ningemshauri atupie jicho pia vyuo vya private vinavyotoa kozi hizo if any
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom