Ushauri: Umachinga haulipi; warudi vijijini kulima maisha yaendelee -- waache kusuguana na serikali

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
43,999
Wengi wamesema mengi. Wacha nami nitoe ushauri.

Kwanza nashangaa imekuwaje serikali yenye nguvu inasitasita kutoa maamuzi ya kimamlaka kushughulikia hawa wanaoitwa wamachinga. Serikali ina vyombo vya dola na mamlaka zote kuhakikisha Machinga wanaondoka maeneo yasiyo halali kufanyia biashara. Sheria za mipango miji ziko wazi.

Kama walivyoondolewa waliojenga kwenye maeneo hatarishi pale Magomeni Dar es Salaam inashindikana vipi kuwafurumusha hawa? Swala moja linachukua miezi sita? Why all these delays? Kwa wamachinga nawashauri wachane kusuguana na serikali kwani ina nguvu kuliko wao.

Warudi vijijini huko kuna mashamba yenye rutuba na yanafaa kwa kilimo na kuongeza tija ktk uzalishaji mali, biashara na ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja na hatimaye kwa Taifa.

Angalizo: Wamachinge msirudie tena kutumika kisiasa. Vinginevyo mtaendelea kuonja joto la Jiwe miaka nenda miaja rudi.
 
Tatizo huko vijijini hakuna barabara za uhakika za kusafirishia mazao kumfikia mlaji. Mazao yanaozea mashambani.

Hakuna soko la uhakika la mazao. Sasa hivi mahindi yamejaa na soko hakuna.
Sasa wakiwa na soko la uhakika sisi huku mjini si watatuuzia bei ghali?
 
Tunengekuwa na SERA bora ya Kilimo cha kisasa katika kila Halmashauri nchini - sidhani kuna kijana wa 18 - 25 angekuja mijini kuuza soksi, nguo za ndani, kupanga rangi kina dada nk.

Sera mbovu hasa za Kilimo ndizo zinatufikisha hapa, mtu anaona kijiji hakulipi anaikimbia ardhi ya bure anakuja mjini kuuza nguo za ndani. tujiulize tumekwama wapi.

Hata ningekuwa mimi kijana kwa hali iliyoko vijijini ni lazima ningekuja mjini tu kukimbizana na hawa migambo wa jiji hadi kieleweke, sababu sikioni kitu na kumvutia kijana abakie kijijini.
 
Halafu wakifika vijijini wanaambiwa pembejeo za kilimo ziko Dar, hilo bomu naamini iko siku litalipuka.
Wacha projections zisozokuwa na mantiki. Ni halmashauri gani hapa nchini ambayo haina facilities za kuuza viuatilifu, mbegu ya mazao na mbolea?

Tena kila mkoa TFA ina sales window ukiacha maduka ya watu binafsi. Kuna maeneo nchi hii hadi vijijini kuna maduka makubwa tu ya kuuza pembeo za Kilimo?
 
Halafu wakifika vijijini wanaambiwa pembejeo za kilimo ziko Dar, hilo bomu naamini iko siku litalipuka.
Huu Ushauri mzuri sanaa last month nilikuwa kijijini vijana wanapiga vizuri sana pesa ya mpunga, nyanya, vitunguu yaani wako njema sana tuu...
 
Tatizo huko vijijini hakuna barabara za uhakika za kusafirishia mazao kumfikia mlaji. Mazao yanaozea mashambani.

Hakuna soko la uhakika la mazao. Sasa hivi mahindi yamejaa na soko hakuna.
Watanzania asilimia 85 wako vijijini, hivi hao wote mnawaonaje?
 
Umachinga Haulipi Kabisa.

Kilimo Hakilipi Kabisa Tanzania (ingawa afadhali wakiwa hukio hawatakosa mkate wao wa kila siku, watakula wanacholima)

Kwa ufupi watunga sera they have lost the plot. Inabidi kuangalia upya ni vipi sekta tofauti zinaweza kwenda sambamba efficiently and sustainably
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom