Ushauri: Umachinga haulipi; warudi vijijini kulima maisha yaendelee -- waache kusuguana na serikali

Rugaijamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2010
2,942
2,000
Wengi wamesema mengi. Wacha nami nitoe ushauri.

Kwanza nashangaa imekuwaje serikali yenye nguvu inasitasita kutoa maamuzi ya kimamlaka kushughulikia hawa wanaoitwa wamachinga. Serikali ina vyombo vya dola na mamlaka zote kuhakikisha Machinga wanaondoka maeneo yasiyo halali kufanyia biashara. Sheria za mipango miji ziko wazi.

Kama walivyoondolewa waliojenga kwenye maeneo hatarishi pale Magomeni Dar es Salaam inashindikana vipi kuwafurumusha hawa? Swala moja linachukua miezi sita? Why all these delays? Kwa wamachinga nawashauri wachane kusuguana na serikali kwani ina nguvu kuliko wao.

Warudi vijijini huko kuna mashamba yenye rutuba na yanafaa kwa kilimo na kuongeza tija ktk uzalishaji mali, biashara na ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja na hatimaye kwa Taifa.

Angalizo: Wamachinge msirudie tena kutumika kisiasa. Vinginevyo mtaendelea kuonja joto la Jiwe miaka nenda miaja rudi.

Kwa hiyo kilimo ni shughuli ya watu walioshindwa maisha ya utafutaji mijini?
Hii dhana ya kipuuzi mno,na haipo kwa watu wa chini (wa Aina Yako ) tu Bali Hadi juu kwa Watawala.
Sijapenda
 
Diazepam

Senior Member
Dec 3, 2020
172
500
Bro kama hiyo kazi ingekuwa haiwalipi wangeshaacha kufanya. So acha kujitoa ufahamu aisee.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,689
2,000
Wengi wamesema mengi. Wacha nami nitoe ushauri.

Kwanza nashangaa imekuwaje serikali yenye nguvu inasitasita kutoa maamuzi ya kimamlaka kushughulikia hawa wanaoitwa wamachinga. Serikali ina vyombo vya dola na mamlaka zote kuhakikisha Machinga wanaondoka maeneo yasiyo halali kufanyia biashara. Sheria za mipango miji ziko wazi.

Kama walivyoondolewa waliojenga kwenye maeneo hatarishi pale Magomeni Dar es Salaam inashindikana vipi kuwafurumusha hawa? Swala moja linachukua miezi sita? Why all these delays? Kwa wamachinga nawashauri wachane kusuguana na serikali kwani ina nguvu kuliko wao.

Warudi vijijini huko kuna mashamba yenye rutuba na yanafaa kwa kilimo na kuongeza tija ktk uzalishaji mali, biashara na ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja na hatimaye kwa Taifa.

Angalizo: Wamachinge msirudie tena kutumika kisiasa. Vinginevyo mtaendelea kuonja joto la Jiwe miaka nenda miaja rudi.
... si-support umachinga. Ila pamoja na hayo, kila mwaka Dar es Salaam ndio imekuwa kinara wa maisha bora nchini; nani asiyependa maisha bora hata kama ubora huo wa maisha unatokana na umachinga? Hii inaoenesha umachinga unalipa kuliko kilimo au shughuli nyingine za uzalishaji vijijini!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
125,012
2,000
Miaka 60 ya uhuru bado tu nchi haijitambui!!! Maccm ni maadui wakubwa wa Watanzania. Imagine nguvu ya machinga ikielekezwa kwenye Kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji nchi nzima. Nguvu kazi inapotea bure.

Tatizo huko vijijini hakuna barabara za uhakika za kusafirishia mazao kumfikia mlaji. Mazao yanaozea mashambani.

Hakuna soko la uhakika la mazao. Sasa hivi mahindi yamejaa na soko hakuna.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
53,496
2,000
Miaka 60 ya uhuru bado tu nchi haijitambui!!! Maccm ni maadui wakubwa wa Watanzania. Imagine nguvu ya machinga ikielekezwa kwenye Kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji nchi nzima. Nguvu kazi inapotea bure.
Na kujenga kiwanda cha kusindika nyanya,
 
  • Thanks
Reactions: BAK

nosspass

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
5,624
2,000
kuwarudisha vijijini ni ngumu mno........wote ni vurugu tuu.....wengi wao walikuwa wanalala mumo humo kwenye vibanda.....na huwa wanaitana mmoja baada ya mmoja........kila kona fujooooo......waende kwenye maeneo rasmi......rutawafuata huko........pale mbezi road ya kinyerezi naona wapo wapo....pale yaani ndio fujo balaa.....
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
125,012
2,000
Si nyanya tu kuna opportunities chungu nzima kwa investment ya trillion 1 na baada ya kipindi kifupi tu matokeo yake makubwa yataonekana na kuwanufaisha wengi sana lakini BONGOLALA ndivyo ilivyo na sera MUFILISI za maccm.

Na kujenga kiwanda cha kusindika nyanya,
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
58,426
2,000
Warudi wakalime,wamalimie meno ???

Iandaliwe mchakato bora wa kilimo

Kuanzia miundombinu shambani,mbolea,masoko nk

HII KUHUSU WATU KWENDA KULIMA
IMENIKUMBUSHA MIAKA YA 90 PALE MA.RASTA WALIPOAMUA KUONDOKA MJINI NA KWENDA KUISHI MASHAMBANI WAKALIME HUKO MORO
KWELI ENEO SHAMBA WALILIPATA,WALIPOFIKA HUKO KWANI WALIKAA WATU BADAYE WALIKIMBIANA

Ova
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom