Ushauri: Ukweni wanataka kunipangia tarehe ya kuoa wao ya kwangu wameikataa wakati nishawaambia wazazi wangu

Kasinja jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
1,034
1,792
Habari za wanajamii za tangia mwaka Jana,

Naomba mnipe ushauri kwa suala ili linanisumbua akili yangu, mimi ni kijana nina umri wa miaka 29 ninaishi Ufaransa ndiko nimejaliwa kufanya shughuli zangu, nina mchumba wangu (miaka 25) ambaye tumepanga kuoana mwaka huu mwezi wa 12, yeye anafanya kazi shirika moja la waholanzi hapo Dsm tokea mwezi wa 11 mwaka jana.

Ilianza hivi kabla sijaenda kusema chochote nyumbani kwamba mwaka huu naoa nilimshirikisha akakubali kuwa niseme nyumbani naye ameshasema kwa ndugu zake kadhaa ambao ni wakubwa.

Nikafunga safari nikaenda zangu Tarime kutoa taarifa kwamba mwaka huu naoa na nikawashirikisha na kuwaambia wazee wa ukoo na mila, wakakubaliana na mimi na wakasema kwamba umri unaruhusu na hakuna kipingamizi.

Na sababu walizonipa kwamba kama nilivyowaambia mwaka huu ndo nioe ili ndugu zangu wengine pia waoe miaka ijayo maana tupo wengi wanaotarajia kufunga ndoa mwaka 2019, 2020 na 2021 kila mmoja ana ratiba yake na tumepeana miaka kila mmoja ili tusiingiliane miaka na gharama za kufanya hayo zikawa kubwa kwa mwaka mmoja ndo maana kila mmoja akatenga mwaka wake, baada ya hapo wameshaanza kutafuta mshenga wa kupeleka barua na wameshampata, nikashika safari yangu nikarudi zangu kazini, nafika sijamaliza siku hata tatu mchumba wangu ananipigia simu kwamba familia yake wamekaa kikao wanaona kwamba harusi ifanyike mwaka ujao siyo huu.

Nikamuuliza sababu wametaja zipi;

1. Kwamba ndo amemaliza chuo hivyo si vema kumaliza chuo gafla anaolewa.

2. Kwamba kwanza afanye kazi angalau mwaka mmoja ndo ataolewa.

3. Hawajajipanga kuwa na harusi mwaka huu hasa send off kwamba hawako vema financially.

Lakin kwa upande wangu nimeona kama vile points hizo si strong sana maana.

Mosi: Amemaliza chuo mwaka Jana mwezi wa 6 hivo mpaka mwezi wa 12 mwaka huu atakuwa na mwaka na nusu tokea amalize chuo.

Pili: Tumekuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne mpaka sasa hivi ingekuwa wanasema nimempata mwka huu wangesema wanachunguza.

Tatu: Aliwashirikisha baadhi ya ndugu nikapewa go ahead ya kuwapa habari hizo wazee, kuwa mwaka huu ni harusi.

Nne: Naanzaje kuwaweka tena wazee chini na kuwapelekea habari nyingine ambayo watasema nimekurupuka kuwaambia bila kukubaliana kwanza.

Tano: Utayari wa kufanya harusi uwa upo kwa anayeoa, labda anayeolewa awe mwanafunzi, au mgonjwa, au awe chini ya miaka 18 ndo ukweni wanaweza ingilia

Naomba ushauri please

Nifanye nini hapo nipo kwenye mtihani mgumu mno.

Habari hii bado sijawaambia wazee tena nashindwa cha kufanya.

Je inawezekana ukweni wanipangie siku ya kufanya harusi mimi?

Note that binti hana wazazi wametangulia mbele ya haki Mungu aziweke roho zao mahala pema amina, hivyo kasomeshwa na ndugu hao hao.
 
Tarehe ya kuoa mara nyingi huwa inapangwa na muoaji ila saa nyingine huwa unaweza kusikiliza hoja za upande wa pili.

Kama inawezekana wasaidie kidogo kwny bajeti ya send off
Ila hoja za upande wa pili hazina nguvu Sana wao wameamua Tu kwamba hakuna kubadilisha tena walichoamua full stop
 
Mimi nadhani angalau wangekuwa wamesogeza siku nyuma ningesema wanataka mahari chapu ila hii ya kusogeza siku mnele kwa kisingizio cha kwamba hawajajipanga kufanya send off mwaka huu mara mtoto wao akae mwaka mmoja zaidi baada ya kumaliza chuo hii be careful my friend mzee asije akawa alishakula mahari kwa msela mwingine na hapa anatafuta namna ya kumwambia binti akuteme kisha mzee aje na jina lake la mfukoni
 
Dah ya chimwagaa
 
Ye anaishi na ndugu Hana wazaz
 
Maybe wazazi wanataka wafaidi matunda ya mtoto wao i mean wale mshahara wake...maana ukishamuoa hawatafaidi vizuri
anyway muulize huyo binti msimamo wake uko vipi
kingine baada ya ndoa mtaishi vipi( utabaki ufaransa mwenzio umwache bongo??
Baada ya kuoa ninakuja naye maana nshamtaftia pa kujishkiza huku,

Ye anasema Hana la kuamua kutofautiana na ndugu zake , maana watamtenga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom