joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
- Thread starter
- #281
Sasa maana ya LAPSSET project ninini?,Sijui kati ya mimi na wewe nani anafahamu mradi wa lapsset kushinda mwingine. Obviously mradi wa lapsset inalenga Kenya kwanza kabla ya kulenga hizo nchi zingine. Halafu nyinyi Watanzania mlikuwa mnataka mradi huu usitishwe lakini serikali ya Kenya imeamua kutumia pesa yake kuijenga na sasa mradi unaisha. Wivu wenu haitazuia mradi kujengwa. Nimeshasema, Mombasa port inahitaji msaidizi. Mombasa port inahandle cargo nyingi kushinda port zote za Tanzania kwa hivyo ni ujinga mtupu kusema eti Lamu port haitapata cargo. Hio backlog ya Mombasa port itapungua Lamu port itakapoanza kazi. Turnaround ya Mombasa port itaimprove na Waganda watawacha kabisa kutumia port ya Dar. Mganda atakuwa anapokea mzigo wake masaa 24 baada ya kutua Kenya.
Hili tatizo lenu la kupenda kukaidi vitu vya wazi kabisa na kujifanya wajuaji ndio sababu mnaishia kufanya miradi mwisho mnaishia njiani. Mlionywa sana kuhusu SGR lakini mlizidi kung'ang'ana kama mnavyofanya sasa hivi katika Lamu Port.
Nilishawahi kukuambia siku za nyuma kwamba, katika projects za Kanya ambazo hazina faida ni hii Lamu port pamoja na Mombasa - Nairobi highway, na huku Tanzania ni mradi wa Bagamoyo Port pamoja na reli ya TANGA, Arusha hadi Musoma, kwasababu hii miradi ni duplication ya miradi iliyopo.
Bandari ya Mombasa na Dar es Salaam zinatosha sana kwa zaidi ya Miaka 50 ijayo kwa mahitaji ya hizi nchi, muhimu ni kuzipanua na kuongeza kasi ya kuondoa mizigo bandarini, ndio sababu wachina waliotaka kujenga Bagamoyo port walitaka bandari zingine zisiboreshwe ili kukwepa competition.
Ninakuhakikishia 100% Lamu Port haiwezi kutengeneza faida kama ilivyo SGR, itagawana mizigo na Mombasa Port mwisho bandari zote mbili zitapata hasara.
Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app