Ushauri: UCHAGUZI WA CCM 2012 Usogezwe mbele...

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,913
23,075
Bashe ahimiza vijana kujitokeza kuwania uongozi uchaguzi CCM

Imeandikwa na Halima Mlacha, Nzega; Tarehe: 3rd October 2011 @ 15:30.

MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe amewataka vijana wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika mwakani.

Aliyasema hayo mjini Nzega alipozungumza na vijana wa Kata ya Mwakashanhala na vitongoji vyake ambapo aliwataka kushiriki kwenye ujenzi wa CCM bora itakayokwenda na wakati zaidi.

Aliwaomba vijana hao mwakani katika uchaguzi huo wajitokeze na kugombea nafasi hizo.

"Sisemi muwaondoe kabisa wazee wetu, lakini gombeeni jamani msiogope hizi nafasi kwenye
matawi kule gombeeni ili mwaka 2012 tujenge chama ambacho kitakua na vijana wengi," alisema Bashe.

Alisema bila vijana kujitolea, wataendelea kuwa wapigadebe wakati wanaokaa ndani kufanya
maamuzi ni wengine wasiozifahamu shida wala matatizo ya vijana...........................................................

Source:HabariLeo | Bashe ahimiza vijana kujitokeza kuwania uongozi uchaguzi CCM

USHAURI:

Kwa mvurugano huu wa vijana(UVCCM) na upinzani wa wazi wazi baina ya viongozi na makada wa CCM katika baadhi ya mambo ndani ya chama na serikali, ningependa kumshauri m/kiti wa CCM. Mimi ninamshauri Mwenyekiti wa CCM afuate taratibu za chama kuhairisha uchaguzi wa CCM 2012 kwa mwaka mmoja, ili kwanza kupunguza migongano hii,lengo likiwa wanachama waingie kwenye uchaguzi wakiwa kwa kiwango fulani wamoja. Endapo uchaguzi huu utafanyika katika hali hii ya "misuguano hii mikali" baina ya wanachama, huku baadhi ya viongozi wakipuuza kutatua matatizo halisi yanayokigharimu chama na kudandia matatizo ya ''kupikwa" ambayo yanazidi kukisambaratisha chama, basi Uchaguzi huo utasababisha hali ya mbaya zaidi si kwa chama pekee hata kwa serikali yenyewe.

Nilikuwa mkoa mmoja wa kaskazini wiki tatu zilizopita na kufanikiwa kukutana na ndugu wa karibu kabisa na Edward Ngoyai Lowasa,nilijaribu kumdadisi kuhusu fununu za EL kugombea uraisi mwaka 2015…Bila kuficha akaniambia bado jamaa ana hayo mawazo tena kwa asilimia 95…Na akaendelea kuniambia kuwa kwasasa EL ana michakato ya kutia mkono wake katika uchaguzi wa NEC-CCM mwakani…Hili kufanikisha hili siku za karibuni EL halikuwa Ujerumani,ambapo inasemekana mipango inasukiwa huko ili kukwepa watu wanaoweza kuingilia mpango huu kama ungefanyika hapa nchini..Jamaa huyu wa karibu na EL aliniambia kuwa kuna mpango madhubuti wa kuhakikisha kuwa NEC inashikwa na kambi yake na RA ili kuweza kufanikisha mpango wake wa kuingia ikulu..Jamaa huyu,japo kwa kusita nilipojaribu kumdadisi kuhusu 111 bilioni ambazo TANESCO wamehamrishwa kuilipa DOWANS kama fidia ya kuvunja mkataba,Je si mlolongo wa mipango iliyoandaliwa kukusanya pesa kwa ajili ya uchaguzi huo,akasema inawezekana ila hana uhakika sana,isipokuwa mipango ya kukusanya hela ipo na inendelea kupitia wafanyabiashara na watu wengine wenye uwezo…

Wazo langu:
Mimi naomba waendelee na uchaguzi ili tuone mengi mwakani,wapigane wao lakini watuachie nchi yetu na amani yake.
 
Wazo langu:
Mimi naomba waendelee na uchaguzi ili tuone mengi mwakani,wapigane wao lakini watuachie nchi yetu na amani yake.
Ni kweli tunaweza kuona mengi lakini ambayo yanaweza kukwamisha mipango ya kuwaletea maendeleo wananchi walio wengi. Kumbuka Serikali ya CCM kwa sasa ndiyo yenye kutekeleza mipango ya maendeleo nchini Tanzania. 2015 ni mbali sana.
 
nani anaye penda vurugu?CCM ni chama cha kihuni vijana hawakitaki tena mtu akiongea ukweli mnamchukia na kumfanya kuwa adui yenu mkubwa,cha kufanya labda muwahimize wamama ndio wagombee.
 
Who cares about CCM? Chama kimeshakufa tunasubiria kwenda kukizika huko baharini

Wasiwasi wangu ni kuwa endepo CCM itasambaratika kwa maneno mengine serkali ya sasa nayo itakuwa imesambaratika kiasi kwamba hata wale wanaopigiwa chepuo kuirithi CCM na serkali yake kimadaraka watakuta magofu. Warithi hao Watakuta serikali iliyoyumba kiuchumi kiasi kwamba inaweza kuwapa wakati mgumu kuwa na serkali imara ya kuwakwamua wananchi kutoka kwa adui wanne(Ujinga,maradhi,umaskini, na Ufisadi).Mimi nafikiri Inatakiwa kwa sasa CCM ituvushe salama mpaka 2015, kwa maana itulie ijaribu kutekeleza kupitia serikali yake hata yale watanzania wa vyama vingine wanayoyaeleza itekeleze. Migogororo ikiendelea ndani ya chama inayumbisha serikali kiasi hata haya yanayosemwa yarekebishwe itashindwa kuyarekebisha. Itakuwa sio sikivu tena kwa kiasi inachojaribu kuwa sikivu kwa sasa.
 
no one cares about CCM anymore. RIP CCM.
we shall bury you with the fraud cheque from DOWANS and see whether you can use that cheque in hell.
 
Bashe ahimiza vijana kujitokeza kuwania uongozi uchaguzi CCM

Imeandikwa na Halima Mlacha, Nzega; Tarehe: 3rd October 2011 @ 15:30.

MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe amewataka vijana wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika mwakani.

Aliyasema hayo mjini Nzega alipozungumza na vijana wa Kata ya Mwakashanhala na vitongoji vyake ambapo aliwataka kushiriki kwenye ujenzi wa CCM bora itakayokwenda na wakati zaidi.

Aliwaomba vijana hao mwakani katika uchaguzi huo wajitokeze na kugombea nafasi hizo.

"Sisemi muwaondoe kabisa wazee wetu, lakini gombeeni jamani msiogope hizi nafasi kwenye
matawi kule gombeeni ili mwaka 2012 tujenge chama ambacho kitakua na vijana wengi," alisema Bashe.

Alisema bila vijana kujitolea, wataendelea kuwa wapigadebe wakati wanaokaa ndani kufanya
maamuzi ni wengine wasiozifahamu shida wala matatizo ya vijana...........................................................

Source:HabariLeo | Bashe ahimiza vijana kujitokeza kuwania uongozi uchaguzi CCM

USHAURI:

Kwa mvurugano huu wa vijana(UVCCM) na upinzani wa wazi wazi baina ya viongozi na makada wa CCM katika baadhi ya mambo ndani ya chama na serikali, ningependa kumshauri m/kiti wa CCM. Mimi ninamshauri Mwenyekiti wa CCM afuate taratibu za chama kuhairisha uchaguzi wa CCM 2012 kwa mwaka mmoja, ili kwanza kupunguza migongano hii,lengo likiwa wanachama waingie kwenye uchaguzi wakiwa kwa kiwango fulani wamoja. Endapo uchaguzi huu utafanyika katika hali hii ya "misuguano hii mikali" baina ya wanachama, huku baadhi ya viongozi wakipuuza kutatua matatizo halisi yanayokigharimu chama na kudandia matatizo ya ''kupikwa" ambayo yanazidi kukisambaratisha chama, basi Uchaguzi huo utasababisha hali ya mbaya zaidi si kwa chama pekee hata kwa serikali yenyewe.

Yes ni kweli kama lilivyo jina lako hapa ni kelele tu .Mada hii haina msaada kwa Nchi hii n ushauri huu upeleke kule Lumumba kwa barua maalum au Vijana pale kwenye jengo lao .Hapa mkuu tunakata issues sasa hapa tunatakiwa kujadili nini? Sisi siyo CCM wala ofisi ya Chama hicho ?
 
Mpigakelele hapa kweli we unapiga kelele tu umeshaambiwa sikio la kufa halisikii dawa, hawa watu wanaoitwa ccm hata ukiwafunga mabomu halafu ukawapa ushauri huu kwa kuwatishia kuwaua watakwambia lipua
 
Ni kweli tunaweza kuona mengi lakini ambayo yanaweza kukwamisha mipango ya kuwaletea maendeleo wananchi walio wengi. Kumbuka Serikali ya CCM kwa sasa ndiyo yenye kutekeleza mipango ya maendeleo nchini Tanzania. 2015 ni mbali sana.
Serikali ya ccm ilishashindwa kuwaletea maendeleo wananchi kwa miaka 50, sasa hivi ndiyo unatarajia itakuwa na miujiza ya kuyaleta hayo maendeleo? To hell with ccm tulishazoea kuishi bila maendeleo wao wanyongane tu yetu macho.
 
Back
Top Bottom