Ushauri: Uboreshaji wa Shirika la Posta

kipenseli2021

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
829
781
Asante sana wana jukwaa wenzangu bado tunatumia fursa hii ya Uhuru wa kujieleza kulingana na katiba yetu kwa kuzingatia maadili na mipaka ya Democracy.

Leo napenda kujadili au kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya shirika letu la Posta

Kabla ya kuendelea nitoe pongezi ya dhati kwa Serikali jinsi inavyoboresha Shirika la Posta Tanzania hasa hasa katika nyanja ya kidigitali ukizingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa upande wa matumizi ya TEHAMA

Pendekezo langu ni kuboresha Shirika la Posta Tanzania hasa kwenye upande wa usafirishaji au usambazaji wa mizigo midogo na mikubwa katika nchi yetu na ikiwezekana nchi jirani

Je, fursa ya usafirishaji mizigo ipo?
Ukiangalia jiografia ya nchi yetu basi kuna fursa kubwa sana na uhitaji wa huduma ya kusafirisha mizigo kutoka malango yafuatayo

1: Lango la kwanza Toka Dar as Salaam, Tanga, Mtwara (Bandari)
Hapo uhitaji wa vitu toka katika bandari zetu na kuvisafrisha maeneo ya ndani, mikao ya ndani

2: Lango la pili toka mikoa ya mpakani (Boda) na kupeleka mikao ya ndani na pembezoni

JE, SERIKALI IFANYE NINI?
1: Kununua magari maalumu ya kubeba mizigo midogo na mikubwa ambayo yatakuwa na route katika mikoa yote kulingana na mahitaji mfano Serikali inaweza kununua magari kwa ajili ya Shirika la Posta ili kusafirishia mizigo ikiwezekana na mazao na kusambaza

2: Kutenga maeneo ya bandari kavu au kutunzia mizigo katika kila mkoa au baadhi ya mikoa

3: Kuweka mifumo ya kidigitali ya kufuatilia mzigo unavyo kwenda

4: Kununua ndege ya mizigo kwa ajili ya Shirika la posta ndege zaidi ya mbili

WALENGWA

1: Watu wote wenye uhitaji wa kusafirisha mizogo kuanzia uzito mdogo na kuendelea

2: Wenye kipato kidogo na kati

Je, kuna umuhimu gani Shirika la Posta kutumia fursa ya usafirishaji mizigo?
1: Kwa miaka ya sasa hivi huduma ya usafirishaji barua imekuwa ndogo hivyo ni bora Shirika la Posta likajikita zaidi kwenye usafirishaji wa mizigo nje na ndani ya nchi

Hitimisho
Serikali iimarishe Shirika la Posta Tanzania katika huduma ya usafirishaji mizigo midogo kwa kuna fedha nyingi sana

Imeandaliwa na Kp 2021
 
Nadhani waweke damu changa inyoendana na changamoto za karne ya 21st
Imagine unamkuta mhudumu umri wa mama yako unashindwa kumkazania afanye kazi chap chap kutokana na na umri
 
Nadhani waweke damu changa inyoendana na changamoto za karne ya 21st
Imagine unamkuta mhudumu umri wa mama yako unashindwa kumkazania afanye kazi chap chap kutokana na na umri
Salaam ziwafikie TTCL, nachagua wimbo wa revola, revola revola kusindikiza salaam zangu
 
Nadhani waweke damu changa inyoendana na changamoto za karne ya 21st
Imagine unamkuta mhudumu umri wa mama yako unashindwa kumkazania afanye kazi chap chap kutokana na na umri
kabisa maana mambo ya kutuma barua yamepungua hivyo lazima waangalie fursa katika usafirishaji wa mizigo mbalimbali
 
Back
Top Bottom